Ni kwanini Jina la YESU linafukuza mapepo tofauti na Jina Allah au Yehova?

Ni kwanini Jina la YESU linafukuza mapepo tofauti na Jina Allah au Yehova?

Unafikiri Yehova angetaka pepo
Zitolewe Kwa jina lake, Mchango wa damu ya Yesu msalabani ungeonekana vipi?

Kwani ukipewa mamlaka unakua cheo cha juu zaidi ya aliyekupa cheo?
Hujiulizi kwanini mamlaka ya Jina YESU lisingeishia duniani pekee na Mbinguni mamlaka ya we Kwa Jina YEHOVA?

Unafikiri kwanini Kila goti Mbinguni na duniani lipigwe Kwa Yesu?

Kwamba ikiwa Yesu Si Baba, kwamba Mungu Baba atampigia Yesu goti huko Mbinguni?

Stuka, Yesu ndiye huyo huyo Baba, Neno, mwana na Roho mtakatifu.

Mungu ni MMOJA na YESU KRISTO/YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake. Amen
 
Umeniambia Mimi mwongo, ninatafsiri maandiko tofauti.

Ikiwa unaamini Yesu Hana baba kimwili, unashindwa vipi kujua kuwa Yesu ndiye Mungu aliyekuja katika mwili wa mwanadamu ikiwa unaamini Mungu ni MMOJA NAFSI Moja?
Unafuata maandiko au unatumia utashi wako wa kiroho?
 
Soma kitabu Cha ufunuo wa Yohana chote Kisha uje useme ikiwa ninadanganya.
Hayo maneno ya Yesu mwenyewe tuachane nayo?
Unajua km ufunuo ni kitabu cha kinabii?
Km aliyoongea Yesu mwenyewe ni magumu kwako kuyaelewa, utawezaje kuelewa ufunuo wa Yohana?
 
Salaam, shalom!!

Mods acheni mjadala huu upate majibu Toka Kwa wadau.

Nimeishi miaka mingi duniani Hadi sasa, na sijawahi kukutana na shehe au pastor akifukuza Roho chafu zilizowapagaa watu Kwa Jina la YEHOVA au Allah!!

Kwanini Jina YESU Lina nguvu kiasi hicho?

Karibuni🙏
Ata Bikira Maria mama yake Yesu, tena sana yani. Mapepo hawalipendi hatari. Ila jaribu Moody 🤣🤣
 
Hayo maneno ya Yesu mwenyewe tuachane nayo?
Unajua km ufunuo ni kitabu cha kinabii?
Km aliyoongea Yesu mwenyewe ni magumu kwako kuyaelewa, utawezaje kuelewa ufunuo wa Yohana?
Yesu mwenyewe ndiye mwalimu wangu kupitia Roho MTAKATIFU ndani yangu.

Yeye ndiye anifunuliaye Siri zake.

Ingia jukwaa la dini, soma thread isemayo ;

Revealed: MUNGU Ni mmoja, na Jina lake ni Yesu Kristo/YESHUA HAMASHIACH - Rabbon

Itatusaidia sana kufahamu Yesu ni nani🤔
 
Ata Bikira Maria mama yake Yesu, tena sana yani. Mapepo hawalipendi hatari. Ila jaribu Moody 🤣🤣
Maria aliyemzaa Yesu,alikuwa mwanafunzi wa Yesu na alimwamini Yesu, na Yuko Mbinguni.

Usitumie Jina Maria kukemea Pepo, hayo ni makufuru, Mariamu alikuwa mtu tu aliyeumbwa na NENO ambaye ndiye Yesu.

Jina ni Moja tu. YESU,

Mungu ni MMOJA na YESU KRISTO/YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake. Amen
 
Maria aliyemzaa Yesu,alikuwa mwanafunzi wa Yesu na alimwamini Yesu, na Yuko Mbinguni.

Uzitumie Jina Maria kukemea Pepo, hayo ni makufuru, Mariamu alikuwa mtu tu aliyeumbwa na NENO ambaye ndiye Yesu.

Jina ni Moja tu. YESU,

Mungu ni MMOJA na YESU KRISTO/YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake. Amen
Waislamu wanashambulia ukristo kwaajili ya mtu km wewe.
Unajinasibu kuwa ni mkristo huku hufuati maneno ya kristo.
Umekaririshwa mafundisho ya mashetani.
Muombe Mungu atakufunulia iliyo kweli.
Yesu bado anakupenda
 
View attachment 3081037
Kwasababu Yesu alikubali kujitoa uhai wake kwa ajili yetu, Yehova Mungu akamlipa kwa kumpandisha cheo (akampa mamlaka) juu yetu na juu ya viumbe vyote..

Kwakua Mungu amempa Yesu mamlaka juu yetu lazima jina lake liwe na nguvu ya kutenda miujiza..

Kabla Yesu hajajitoa sadaka pale msalabani hakua na mamlaka yeyote, Mamlaka ilikua haina msimamizi zaidi ya Yehova Mungu mwenyewe ..

Unajua dhima ya Yehova ni kutumikiwa lakini dhima ya yesu ni Kutumikia

View attachment 3081038

Kwakua dhima yake ni kutumikia, Sasa amepewa mamlaka, Na anafanyika daraja kupeleka dua zetu kwa Yehova.. Yeye ni njia, kweli na Uzima..

Kwakua alijitoa sadaka, Yehova amemheshimu na kumpa Mamlaka kama Zawadi, Lazima umuombe Yesu then yeye ndio apeleke kwa baba..
View attachment 3081039 Unadhani asingepewa hayo mamlaka , Sadaka yake pale msalabani nani angeona umuhimu?

Kwa lugha nyingine Yesu amepewa Ukuhani mkuu kule mbinguni.. View attachment 3081040

Nadhani umeelewa au lah umepata mwanga, kwamba kwanini Tusali kwa jina la Yesu ..
Mungu ni MMOJA tu. Jina lake ni Yesu.

Akiwa kitini pa enzi, anaitwa Baba, Yesu yule yule.

Akiwa ulimwenguni kuwahudumia WATAKATIFU kupitia Roho mtakatifu ambaye ni ROHO wa Yesu yule yule.

Akiwa duniani kuukomboa Ulimwengu msalabani anaitwa Mwana, ni Yesu yule yule.

Mungu ni MMOJA na YESU KRISTO/YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake. Amen
 
Waislamu wanashambulia ukristo kwaajili ya mtu km wewe.
Unajinasibu kuwa ni mkristo huku hufuati maneno ya kristo.
Umekaririshwa mafundisho ya mashetani.
Muombe Mungu atakufunulia iliyo kweli.
Yesu bado anakupenda
Yesu akamwambia Filipo,

Anionaye Mimi, amemwona BABA. Yesu ndiye Mungu baba akiwa kitini pa enzi.

Yesu ndiye Mungu aketiye katika KITI Cha enzi.

Mungu ni MMOJA na YESU KRISTO YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake. Amen
 
Ongeza na hii:

Yohana 14:6-7
KJV

Yesu akasema, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba yangu;

Yn 14:7 Yesu akasema, “Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.” Lakini wanafunzi wake hawakumwelewa anamaanisha nini, hivyo Filipo akamwambia tuonyeshe Baba. Na Yesu akawaambia “Aliyeniona mimi amemwona Baba”, kisha akafafanua zaidi kwamba, ni kwa sababu “mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. Yn 14:10, Akaweka wazi kwamba, “la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.” Yn 14:11
Hapa Yesu anasema wazi Mimi ndiye Mungu, watu Bado wanashangaa!!

Hata siku ya mwisho, Hawa wanaomkataa Yesu Leo, watashangaa kumwona aketiye katika KITI Cha enzi Mbinguni kuhujumu Ulimwengu atakuwa na matundu yavujayo Damu ktk viganja mikononi mwake.

Mungu akubariki 🙏
 
Ni kwanini wanafunzi wa Yesu walikuwa wanamsujudia?
Je ni kwakuwa walibaini ya kwamba ni Mungu ?
..............
Mathayo 28
17 Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka.
18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
..........
Hapa Yesu anathibitisha kuwa ana mamlaka yote Mbinguni na Duniani.
Wajameni Bado hamjagundua tu kuwa Yesu ndiye Mungu Mwenyezi.
.......
Mwenye mamlaka yote ya Mbinguni na Duniani ni nani ?
 
Hivi nyie watu mnatatizo gani?
Hapo mwenyewe umenukuu maandiko yesu anasema "amepewa" mamlaka.
Kwanini hujiulizi 'kapewa' na nani?
Kwamba hujui maana ya kupewa?
 
Hata mimi nashangaa sana hii kitu, Ukisoma biblia sehemu kadhaa yesu anasema nimetumwa na Baba

Lakini Yesu mwenyewe alikua anapandisha mlimani kusali kwa Baba yake..

Hata sala Rasmi inaanza na "Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe"

Hata sheria inasema "Wakujue Mungu wa pekee wa kweli na Yesu kristo uliyemtuma"

Bado tena Yesu alisema katika Marko
View attachment 3081015

Ukisoma hapo vizuri inaeleza Baba pekee ndo anaujua mwisho , Yesu haujui..

Sasa hua nashangaa sana kukuta Mkristo saa nyingine Mtumishi anatangaza kwamba Yesu ni Mungu na anajua Mwisho na hapo Yesu mwenyewe kakilii kwamba kuna aliemzidi uwezo na huyo ndio aijuae siku hiyo...

How comes wawe kitu kimoja? Wakristo mjitafakari?

Thats why siamini dini ..
Achana naye maana hiyo ndio imani na tafsiri yake.
 
Hivi nyie watu mnatatizo gani?
Hapo mwenyewe umenukuu maandiko yesu anasema "amepewa" mamlaka.
Kwanini hujiulizi 'kapewa' na nani?
Kwamba hujui maana ya kupewa?
Tatizo kubwa la baadhi ya Muslims wanaisoma Biblia kimtazamo wa Qurani.

Mungu wa katika Biblia alisha kuja duniani kuongea na watu kwa maumbile tofauti tofauti.

Aliongea na Musa akiwa kama Kijinga cha Moto, na kumwamrisha avue viatu sehemu takatifu, jambo ambalo Waislamu mnatekeleza Hadi hii leo.
Alisha mtembelea Nabii Ibrahimu kama mtu soma Mwanzo 18:1....
Hivi nyie watu mnatatizo gani?
Hapo mwenyewe umenukuu maandiko yesu anasema "amepewa" mamlaka.
Kwanini hujiulizi 'kapewa' na nani?
Kwamba hujui maana ya kupewa?
Naomba unijibu swali moja tu.

Leo Waislamu mkiingia Msikitini kuswali mnavua viatu na kuviacha nje kwakuwa Msikiti na pahali Patakatifu.

Amri hii mnaitii kwakuwa Mungu alimwambia hivyo Nabii Musa alipomtokea katika Bonde la Tua kama mnavyosema.

Tukitizama tukio lile maandiko yanasema kuwa siku hiyo Mungu alimtokea Musa akiwa katika Umbo la Kijinga cha Moto.
Swali
1. Hivi Mungu ni Kijinga cha Moto?
2. Je Kijinga cha Moto ni Mungu Mwingine ?

Nasubibiri jibu
 
Nadhani alimtokea Ibrahimu hapa
Mwanzo 18:1
Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari.
2 Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi,
3 akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako.
..........
Hivi Mungu ni Mtu kama sisi ?
 
Ndio mana nika devorce dini, Bible is complicated
 
Back
Top Bottom