Ni kwanini Jina la YESU linafukuza mapepo tofauti na Jina Allah au Yehova?

Ni kwanini Jina la YESU linafukuza mapepo tofauti na Jina Allah au Yehova?

Hebu tujikumbushe kwa Unabii wa Nabii Isaya.
........
Isaya 9:6
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake,
1. Mshauri wa ajabu,
2. Mungu mwenye nguvu,
3. Baba wa milele,
4. Mfalme wa amani.
........
Hapo Isaya anasema Jina lake na sio Majina yake.
Hapo anamaanisha huyo ni mmoja tu.
Naona hapa wa upande wa pili Wana maswali mengi sana.
Swali moja wapo ni
1. Mtoto wa kiume anawezaje kuwa Mungu.
2. Halafu awe Baba
Huu Unabii hawawezi kabisa kuuelewa, ndio maana wanakimbilia kusema. Biblia imetiwa mikono na Waandishi na kuiharibu.
 
Wafilipi 2:6.,7.,8.,9.,10.,11.

6. ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;

7. bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;

8. tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.

9. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;

10. ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;

11. na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Tusomeni maandiko..
 
Sijasoma comments zenu,ila nishuhudie jambo, nimewahi fukuza Pepo kwa kutumia jina la Mungu ,nilikuwa namuombea mtu,nikamkumbusha Mungu maajabu aliyoyafanya,ikiwemo Ile nguvu ya Elia na manabii wa baali mia nne, nikagusia nguvu ya Mungu na ujiti wa Musa Kisha nikamalizia na kifungu ambacho Mungu mwenyewe alijitambulisha kama yehova, Mungu wa vita,,,,,baada ya hapo,nilichokishuhudia ndio msukumo wa Mimi kulog-in Sasa hivi, maana nilikuwa nasoma kama guest user
We ikiwa umefikia mpaka uwezo wa kumkumbusha Mungu maajabu yake sasa unashangaa nini tena? si ajabu hata hao mapepo wenyewe wanaogopa kukufuru pamoja na wewe!
 
Kuna watu wanatumia imani kwa njia za Kiudanganyifu kwa faida zao wenyewe ndio lakini haifanyi imani katika Yesu Kristo kuwa ni uongo, porojo au upotoshaji..

Na wanadanganywa ni kwasababu ya kutokujua na wanaojua hawataki kufata principles..

Yesu alipo kuwa dunia alisema yeye ndio njia kweli na uzima
 
Marko 16:15.,16.,17.,18.,19.
15. Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

16. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

17. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;

18. watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.

19. Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.
 
Sijui kwanini nashindwa kuelewa.. Mtu yupo radhi aamini kwamba duniani tumeumbwa mateso, kutenda dhambi..

Unashindwa kuamini kwamba Mungu alimtoa Yesu Kristo kwa dhambi za watu wote.. Kwamba wewe can literally live without sinning.. Bila magonjwa..

Nini ambacho ni kigumu kiamini
Mambo mengine kidogo mjiongezege ndugu zangu! kwahiyo ukimkiri Yesu huumwi? ... kweli? zile spitali za kikiristo zinamtibu nani sasa?

Halafu unaposema Yesu alitolewa kwa dhambi za watu, sasa ni kwamba saivi hakuna dhambi ama? na kama dhambi zipo sasa faida ya yeye kutolewa ni ipi? ... mi ninavyoelewa kabla ya Yesu walikuwepo watu waliomuabudu Mungu na walikuwepo waliomkufuru, pia baada yake wapo wote aina mbili.

Sasa yeye alisulubiwa kuokoa watu gani hapo?
 
Hayo maneno hatuyatoi sisi kama sisi ni Biblia ndio imeandika hivyo.
Tito (Tit) 2:13
tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
.........
Wanafunzi wake walipo mtambua kama yeye ni nani walianza kumsujudia na yeye hakuwakataza.
Mathayo 28:16
Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu.
17 Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka.

Kumbukeni ni yeye alimwambia Shetani wakusujudiwa ni Mungu tu.
Mathayo 4:10
Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
 
Hebu tujikumbushe kwa Unabii wa Nabii Isaya.
........
Isaya 9:6
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake,
1. Mshauri wa ajabu,
2. Mungu mwenye nguvu,
3. Baba wa milele,
4. Mfalme wa amani.
........
Hapo Isaya anasema Jina lake na sio Majina yake.
Hapo anamaanisha huyo ni mmoja tu.
Naona hapa wa upande wa pili Wana maswali mengi sana.
Swali moja wapo ni
1. Mtoto wa kiume anawezaje kuwa Mungu.
2. Halafu awe Baba
Huu Unabii hawawezi kabisa kuuelewa, ndio maana wanakimbilia kusema. Biblia imetiwa mikono na Waandishi na kuiharibu.
Carnal mind.. Kwa carnal mind Bible ni ngumu kumeza
 
Kuna watu wanatumia imani kwa njia za Kiudanganyifu kwa faida zao wenyewe ndio lakini haifanyi imani katika Yesu Kristo kuwa ni uongo, porojo au upotoshaji..

Na wanadanganywa ni kwasababu ya kutokujua na wanaojua hawataki kufata principles..

Yesu alipo kuwa dunia alisema yeye ndio njia kweli na uzima
Sasa nyinyi mbona hamumtumii kama njia badala yake mnamfanya kuwa ndo destination?
 
Ila waafrika Mungu atusaidie tu, bible inaongelea wayahudi na waisrael tu hakuna jina la Mwaisa, Masawe, Shayo, wala hata Mbwambo.

Tumeshikilia vitabu vya dini as if sisi ndiyo tumeandikiwa wakati hata havituhusu hata kidogo.

Dini ni strategy ya kiutawala duniani ndy maana Roman Empire iliweza kuitawala dunia nzima kwa kupitia vitabu vya biblia na kueneza dini, wachina wameondoa maswala ya udini tangu Mao tse tung au Mao ze dong alipoichukua nchi na sasa waone kwenye uchumi wa dunia unavyowategemea, wamarekani na waingereza wameshaondoka kwenye sana za udini na ukabila sisi bado tunamijadala ya kuhusu jina la Yesu, mapepo yapo na yanaondolewa hata kwa matambiko ya kiafrika, NaN kwa majina ya mababu wa kiafrika Acha kuwa mtumwa wa kifikra bana
Tatizo Ukristo sio dini maisha halisi.. wanaofanya kuwa dini ndio wanatawaliwa..

Waefeso 2:1.,2.,3.,4.,5.,6.,7.,8.,9.,10.
1. Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;

2. ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;

3. ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.

4. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda;

5. hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.

6. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;

7. ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.

8. Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;

9. wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.

10. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
 
Jina la yesu lingeponya magonjwa hospital zisingejengwa, hospital zimejengwa kuanzia na wamisionari wageni hadi wazawa,hao wanaojifanya kuombea wakiumwa huenda hospital
Nguvu ya Jina Lina fanya kazi Kwa Imani, so tatizo ni Imani.
 
Mapepo ndio akina nani na kwanini asilimia kubwa ni wanawake
Africa aliyeturoga Kweli alituweza Yaan karne ya 21 bado unaamini katika mapepo duu
 
Sasa nyinyi mbona hamumtumii kama njia badala yake mnamfanya kuwa ndo destination?
Yohana 14:6.,7.,8.,9.,10.,11.,12.,13.
6. Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

7. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.

8. Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.

9. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?

10. Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.

11. Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.

12. Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.

13. Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
 
Mambo mengine kidogo mjiongezege ndugu zangu! kwahiyo ukimkiri Yesu huumwi? ... kweli? zile spitali za kikiristo zinamtibu nani sasa?

Halafu unaposema Yesu alitolewa kwa dhambi za watu, sasa ni kwamba saivi hakuna dhambi ama? na kama dhambi zipo sasa faida ya yeye kutolewa ni ipi? ... mi ninavyoelewa kabla ya Yesu walikuwepo watu waliomuabudu Mungu na walikuwepo waliomkufuru, pia baada yake wapo wote aina mbili.

Sasa yeye alisulubiwa kuokoa watu gani hapo?
4. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda;

5. hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.

6. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;

7. ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.

8. Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;

9. wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.

10. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
 
Wagalatia 2:16.
16. hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki.
 
Wagalatia 3:11.,12.,13.,14.
11. Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani.

12. Na torati haikuja kwa imani, bali, Ayatendaye hayo ataishi katika hayo.

13. Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;

14. ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.
 
Nguvu ya Jina Lina fanya kazi Kwa Imani, so tatizo ni Imani.
Cheney nguvu jina au mtu mwenyewe!?..lazaro alikua na imani gani akiwa mfu mpaka akafufuliwa?..hao wachungaji imani hawana?.. maana wakiumwa huenda hospital
 
Hebu tujikumbushe kwa Unabii wa Nabii Isaya.
........
Isaya 9:6
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake,
1. Mshauri wa ajabu,
2. Mungu mwenye nguvu,
3. Baba wa milele,
4. Mfalme wa amani.
........
Hapo Isaya anasema Jina lake na sio Majina yake.
Hapo anamaanisha huyo ni mmoja tu.
Naona hapa wa upande wa pili Wana maswali mengi sana.
Swali moja wapo ni
1. Mtoto wa kiume anawezaje kuwa Mungu.
2. Halafu awe Baba
Huu Unabii hawawezi kabisa kuuelewa, ndio maana wanakimbilia kusema. Biblia imetiwa mikono na Waandishi na kuiharibu.
Mtoto huyo tuliopewa ni Mungu mwenyewe nguvu,

BABA WA milele.

Halafu ukimwambia mtu Yesu ndiye huyo huyo Mungu BABA aketiye KITI Cha enzi haelewi.

Mungu atusaidie.
 
Back
Top Bottom