Ni kwanini Makonda anakagua miradi iliyotekelezwa na Serikali na kisha kuikabidhi kwa CCM?

Bumunda
Chama cha mapinduzi ndicho kinaisimamia serikali kwa hiyo ikikamilika serikali inakabidhi ripoti na miradi kwa chama kuwa sisi kazi mliyoyututuma serikali tufanye hiyo hapo tunawakabidhi.
 
Serikali ni ya chama gani?
Kuwa mwelewa acha kupotoshwa! Serikali ya Tanzania na siyo serikali ya ccm! Huko mashuleni mmesomea vitu gani Hadi ushindwe kutofautisha Kati ya serikali na chama? Differentiate between party and government!
 
Chama cha siasa kinaongoza nchi kupitia serikali na ndio maana viongozi wa chama wananguvu kuliko viongozi wa serikali

‘Naliwe’ kikwetu ni kuliwa, wewe unaliwa!

Pia unaweza kuikata hiyo ‘l’ iwe ‘t’ [emoji1493][emoji1493][emoji1493]
 
Hii ni PR tuu, kingine ni kwa sababu yeye ni mteule wa Rais mwnye majukumu ya kusimamia ilani ya CCM ktk mkoa wake hivyo anachofanya ni kuonyesha utekelezaji wa ilani na sio kivingine
 
Chama cha siasa kinaongoza nchi kupitia serikali na ndio maana viongozi wa chama wananguvu kuliko viongozi wa serikali
Hivyo ndivyo Katiba inavyosema?Yaani viongozi wa chama cha siasa wanakuwa na nguvu kulikoni serikali? Mbona Mimi hapo sielewi,tutakuwa na nchi ya ajabu sana tukiruhusu hali hii iendelee.Watawala wanashindwa kutofautisha kati ya kuku na yai,nini kilianza?
 
Hii ni PR tuu, kingine ni kwa sababu yeye ni mteule wa Rais mwnye majukumu ya kusimamia ilani ya CCM ktk mkoa wake hivyo anachofanya ni kuonyesha utekelezaji wa ilani na sio kivingine
Hivyo akishasimamia na kukamilika anaikabidhi kwa CCM?Mnacganyikiwa sasa,hamfahamu mnachokifanya.Mnatafuta namna ya kuhalalisha kampeni za mapema.Bunge lilipovunjwa inaashiria kukamilika kwa utekelezaji wa ilani ya 2015-2020,mnakwama wapi CCM?
 
Chama cha mapinduzi ndicho kinaisimamia serikali kwa hiyo ikikamilika serikali inakabidhi ripoti na miradi kwa chama kuwa sisi kazi mliyoyututuma serikali tufanye hiyo hapo tunawakabidhi.
Acheni kupotosha.... Ilani inaingizwa kwenye mpango wa taifa wa miaka 5 hivyo kazi ya utekelezaji inafuatiliwa na bunge bila kujali chama. Kwahiyo mradi ukitekelezwa if wa serikali ni serikali hao CCM watakabidhiana ripoti ndani kwa ndani kwa watendaji wao ila sio eti mradi uliopitishwa na bunge eti ukabidhiwe kwa CCM hyo ni propaganda tu ila utaratibu haupo hivyo.
 
Mkuu kuna nyuzi umedai upo neutral ila kwa comment hii nimeelewa upande wako!!

Chama kikishinda uchaguzi kinapewa ridhaa kuongoza serikali

Chama kinakabidhi ilani kwa serikali

Serikali inaingiza ilani kwenye mpango wa taifa wa miaka 5

Bajeti za halmashauri/serikali kuu zinatengenezwa kufuata mpango wa taifa

Utekelezaji wa miradi ukifanikiwa ni mafanikio ya serikali ambayo inajumuisha mpaka wasio na chama yaani watumishi wa umma

Kwahiyo hao CCM wanasifiwa au kulaumiwa sababu wanaongoza serikali yaani wametoa Rais ambaye ndio amegeuka kiongozi mkuu wa nchi/mwenyekiti wa tume ya MIPANGO na sababu CCM imetoa mawaziri ila sio sababu ni mwenyekiti wa CCM!!

Ndio maana siku ikitokea mawaziri na wakuu wa mikoa kutokua na chama kma ilivyotaka rasimu ya warioba ndio utaelewa CCM na serikali ni vitu viwili tofauti kabisa.

So utekelezaji ni SERIKALI ila hao watekelezaji wana kadi ya CCM but isiwe other way round!!
 
zitto junior
Asante sana mkuu kwa elimu kubwa umedadavua hapo juu, tuvumilie tu tumepatikana awamu hii... yaani ni kama hatukuwahi kuwa na serikali hapo awali.
 
SI vyema kumhusisha mtu na HISIA mbaya zisizoeleweka...si utu kwa kweli...acha KUTIA CHUKI MIOYONI MWA WATU

Hayo aliyosema huyo jamaa ni ukweli mtupu. Hajatia chuki bali kaweka ukweli hadharani fullstop.
 

Kaa hapa umtetea mtu muovu kwakuwa unafaidika na madaraka yake, ila huwezi kubadilisha hata nukta ya ukweli unaosemwa juu yake. Saa hii amebaki kufanya siasa chafu akidhani atabadilishana ukweli unaosemwa juu yake. Ukweli uko palepale, hata alipe Kundi la majobless wote wa nchi hii kumtetea, ukweli uko kama unavyosemwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…