Ni kwanini Makonda anakagua miradi iliyotekelezwa na Serikali na kisha kuikabidhi kwa CCM?

Ni kwanini Makonda anakagua miradi iliyotekelezwa na Serikali na kisha kuikabidhi kwa CCM?

Bumunda
Chama cha mapinduzi ndicho kinaisimamia serikali kwa hiyo ikikamilika serikali inakabidhi ripoti na miradi kwa chama kuwa sisi kazi mliyoyututuma serikali tufanye hiyo hapo tunawakabidhi.
 
Serikali ni ya chama gani?
Kuwa mwelewa acha kupotoshwa! Serikali ya Tanzania na siyo serikali ya ccm! Huko mashuleni mmesomea vitu gani Hadi ushindwe kutofautisha Kati ya serikali na chama? Differentiate between party and government!
 
Chama cha siasa kinaongoza nchi kupitia serikali na ndio maana viongozi wa chama wananguvu kuliko viongozi wa serikali

‘Naliwe’ kikwetu ni kuliwa, wewe unaliwa!

Pia unaweza kuikata hiyo ‘l’ iwe ‘t’ [emoji1493][emoji1493][emoji1493]
 
Hii ni PR tuu, kingine ni kwa sababu yeye ni mteule wa Rais mwnye majukumu ya kusimamia ilani ya CCM ktk mkoa wake hivyo anachofanya ni kuonyesha utekelezaji wa ilani na sio kivingine
 
Chama cha siasa kinaongoza nchi kupitia serikali na ndio maana viongozi wa chama wananguvu kuliko viongozi wa serikali
Hivyo ndivyo Katiba inavyosema?Yaani viongozi wa chama cha siasa wanakuwa na nguvu kulikoni serikali? Mbona Mimi hapo sielewi,tutakuwa na nchi ya ajabu sana tukiruhusu hali hii iendelee.Watawala wanashindwa kutofautisha kati ya kuku na yai,nini kilianza?
 
Hii ni PR tuu, kingine ni kwa sababu yeye ni mteule wa Rais mwnye majukumu ya kusimamia ilani ya CCM ktk mkoa wake hivyo anachofanya ni kuonyesha utekelezaji wa ilani na sio kivingine
Hivyo akishasimamia na kukamilika anaikabidhi kwa CCM?Mnacganyikiwa sasa,hamfahamu mnachokifanya.Mnatafuta namna ya kuhalalisha kampeni za mapema.Bunge lilipovunjwa inaashiria kukamilika kwa utekelezaji wa ilani ya 2015-2020,mnakwama wapi CCM?
 
Chama cha mapinduzi ndicho kinaisimamia serikali kwa hiyo ikikamilika serikali inakabidhi ripoti na miradi kwa chama kuwa sisi kazi mliyoyututuma serikali tufanye hiyo hapo tunawakabidhi.
Acheni kupotosha.... Ilani inaingizwa kwenye mpango wa taifa wa miaka 5 hivyo kazi ya utekelezaji inafuatiliwa na bunge bila kujali chama. Kwahiyo mradi ukitekelezwa if wa serikali ni serikali hao CCM watakabidhiana ripoti ndani kwa ndani kwa watendaji wao ila sio eti mradi uliopitishwa na bunge eti ukabidhiwe kwa CCM hyo ni propaganda tu ila utaratibu haupo hivyo.
 
Kwani hiyo Miradi inasimamiwa na Serikali ya Chama gani? Hivi Upinzani wa Tanzania unaunda Serikali ya sasa? Swali lako ni la Kitoto sana na sikudhani kama ungeliuliza wakati lipo tu wazi na majibu yake yapo hadharani. Yaani umeshindwa tu hata kujua ya kwamba Chama Cha Mapinduzi ndicho Kinaunda Serikali Kuu hii iliyopo ya hawa Watendaji akina Mkuu wa Mkoa Makonda na kwamba yote haya unayomshangaa Mkuu wa Mkoa Makonda kuyafanya na hadi kuyazindua hivi ni sehemu ya Utekelezaji wa yale yaliyokuwa katika ILANI ya Chama Tawala ( CCM ) Ndugu? Umenishangaza mno!
Mkuu kuna nyuzi umedai upo neutral ila kwa comment hii nimeelewa upande wako!!

Chama kikishinda uchaguzi kinapewa ridhaa kuongoza serikali

Chama kinakabidhi ilani kwa serikali

Serikali inaingiza ilani kwenye mpango wa taifa wa miaka 5

Bajeti za halmashauri/serikali kuu zinatengenezwa kufuata mpango wa taifa

Utekelezaji wa miradi ukifanikiwa ni mafanikio ya serikali ambayo inajumuisha mpaka wasio na chama yaani watumishi wa umma

Kwahiyo hao CCM wanasifiwa au kulaumiwa sababu wanaongoza serikali yaani wametoa Rais ambaye ndio amegeuka kiongozi mkuu wa nchi/mwenyekiti wa tume ya MIPANGO na sababu CCM imetoa mawaziri ila sio sababu ni mwenyekiti wa CCM!!

Ndio maana siku ikitokea mawaziri na wakuu wa mikoa kutokua na chama kma ilivyotaka rasimu ya warioba ndio utaelewa CCM na serikali ni vitu viwili tofauti kabisa.

So utekelezaji ni SERIKALI ila hao watekelezaji wana kadi ya CCM but isiwe other way round!!
 
zitto junior
Asante sana mkuu kwa elimu kubwa umedadavua hapo juu, tuvumilie tu tumepatikana awamu hii... yaani ni kama hatukuwahi kuwa na serikali hapo awali.
 
SI vyema kumhusisha mtu na HISIA mbaya zisizoeleweka...si utu kwa kweli...acha KUTIA CHUKI MIOYONI MWA WATU

Hayo aliyosema huyo jamaa ni ukweli mtupu. Hajatia chuki bali kaweka ukweli hadharani fullstop.
 
Ya "akutukanaye".....
Acha kuunganishaunganisha picha ili upate mtiririko uutakao.....

Makonda ni mwanasiasa kijana na alianza kuandamwa siku nyingi huko toka akiwa TAHLISO...
Jiwe la kumshambulia kuliko kukubwa LILISIMIKWA pale aliposimama kidete kuyaongelea machafu ya upigaji juu ya lile jengo letu la vijana UVCCM....
IKUMBUKWE ALIKUWA ANAPAMBANA NA WATU WALIOKUWA NYUMA YA MAGOGO WA UPIGAJI NCHINI HAPA.

HAYO YAKAPITA

CHUKI ikaendelea dhidi yake pale alipokuwa anasimama KISIASA na baadhi ya wale "mitume 12 wa BUNGE".......

Makonda AMEKUWA mhanga wa mashambulizi YANAYORATIBIWA VYEMA kutoka kwa wale watu wenye NGUVU zisizoeleweka.....
Nakukumbusha tu uwezo wa HAO WATU....

Mh.Mizengo Kayanza Peter Pinda alishawahi kulalamika bungeni kuwa
"majitu hayo Yana mitandao mipana yenye propaganda na udundumwizi mwingi,si majitu mepesi hata KIDOGO"
Sasa km waziri mkuu....mtendaji mkuu wa serikali...mtu ambaye anaijua nchi zaidi ya kijana mwenzetu makonda ANAYAPWAGA HAYO HADHARANI.....
Je akitokea kijana mkakamavu na jasiri wa kuyasema hayo,ATABAKI SALAMA?!!!
TUWENI WAKWELI JAMA...

Makonda anashambuliwa kukubwa na wengi ambao wamekodisha "wapiga miluzi ya CHUKI" wasio na IDADI....

Mnyonge mnyongeni,Haki yake mpeni.

THINK THRICE

Kaa hapa umtetea mtu muovu kwakuwa unafaidika na madaraka yake, ila huwezi kubadilisha hata nukta ya ukweli unaosemwa juu yake. Saa hii amebaki kufanya siasa chafu akidhani atabadilishana ukweli unaosemwa juu yake. Ukweli uko palepale, hata alipe Kundi la majobless wote wa nchi hii kumtetea, ukweli uko kama unavyosemwa.
 
Back
Top Bottom