Ni kwanini Makonda anakagua miradi iliyotekelezwa na Serikali na kisha kuikabidhi kwa CCM?

Ni kwanini Makonda anakagua miradi iliyotekelezwa na Serikali na kisha kuikabidhi kwa CCM?

Chama cha mapinduzi ndicho kinaisimamia serikali kwa hiyo ikikamilika serikali inakabidhi ripoti na miradi kwa chama kuwa sisi kazi mliyoyututuma serikali tufanye hiyo hapo tunawakabidhi.
Tutarajie SGR, Nyerere Dam nk nk navyo kukabidhiwa kwa CCM? Hiki kinachoendelea Dsm ni kitu cha ajabu sana!

Anyway kwa hiyo lini CCM wataikabidhi hiyo miradi kwa wananchi? Maana hela na rasilimali zote zilizotumika kujenga hiyo miradi si za CCM.
 
Kazi ya bunge ni kuijadiri iyo milandi iliyo ndani ya ilani ya chama
CCM ndio huandaa miradi halafu miradi ile inaiweka kwenye Ilani ya CCM Kwenye kampeni CCM hunadi hiyo miradi ikishinda inaipa serikali inaitekeleza ikiitekelrza serikali inaikabidhi kwa CCM ili ikabidhi wanachi kampeni za uchaguzi mwinginr zikianza

Chadema wanabwata kwenye kampeni vitu visivyokuwepo ohhh tunataka demokrasia Ohhh tume huru !!! Mtu anataka barabara, hospital, shule,maji Safi nk wao wanabwata vitu ambavyo mwananchi hata haielewi sababu sio hitaji lake !! Mfano demokrasia ya kuongea mtu wa kawaida huongea popote Hadi kwenye soko au daladala au mitaan nki na hasumbuliwi na mtu wa serikali wanaporomosheana Hadi matusi ya nguoni hakuna anayewasumbua labda washitakiane wenyewe.Sasa ukimwambia Tanzania Hakuna Uhuru wa kuongea anakushangaa Sana tu anakwambia mbona sisi tunaongea Sana Hadi kutukanana na serikali haitusumbui?
Ndio maana CCM huenda na wanachohitaji wananchi sio vitu vya kubuni vya wazungu
 
CCM ipo Dar es Salaam pekee?
Utekelezaji wa kila mtu inatofautiqna na mwenzake ndio maana wewe unaona Dar tu na kwa sababu ya Makonda ila wengi wanafanya hayo Ila kwa njia tofauti
 
Mimi naona anafanya tu kampeni zake na kuwaponda wapinzani...mbona wakuu wa mikoa wenzake hawafanyi hiki anachofanya yeye saiz?
 
Unapokuwa mkuu wa mkowa, wewe sio ccm, unapokuwa kiongozi wa serikali wewe sio ccm na ukivuka mipaka yako huo sio utawala bora

Siku hizi ni kinyume, watumishi na viongozi wanavaa mavazi ya chama hadharani... zamani yalibakia sirini!
 
Pesa za serikali lakini utekelezaji wa CCM.

Ukiwa mkubwa halafu hamnazo inaumiza jamii. Hivi kweli dhamira yako inakwambia ulichosema ndivo kilivyo?? Unaweza kumkabidhi mtu mali yake tu, sio hisia kuwa ni mali yake!!

Serikali ni umma wa watanzania na wala si CCM, Chadema, TLP na wengine!!
 
Ndugu zangu, au mimi tu sielewi hii kitu!

Nauliza ili nipate kujua, nimekuwa nikishangaa huu mkakati wa Paulo Makonda, RC Dar es Salaam. Sijawahi kuona kabla, pengine ni kwa vile sijui!

Kama hiyo haitoshi, anatumia nafasi hiyo kuwadhihaki watu na kuwananga ikiwa mbunge wa eneo la mradi hatokani na chama chake.

Pamoja na ukweli kuwa serikali iliyopo madarakani inatekeleza ilani ya chama chake, ni nini kinawapa umiliki namna hii?

Miradi ya maendeleo, miradi ya serikali, ni vipi inakabidhiwa kwa chama? Je, ni mali ya chama?

Maendeleo hayana vyama!

Wasalaam,

Ncha Kali.

Kwani hiyo Miradi inasimamiwa na Serikali ya Chama gani? Hivi Upinzani wa Tanzania unaunda Serikali ya sasa? Swali lako ni la Kitoto sana na sikudhani kama ungeliuliza wakati lipo tu wazi na majibu yake yapo hadharani. Yaani umeshindwa tu hata kujua ya kwamba Chama Cha Mapinduzi ndicho Kinaunda Serikali Kuu hii iliyopo ya hawa Watendaji akina Mkuu wa Mkoa Makonda na kwamba yote haya unayomshangaa Mkuu wa Mkoa Makonda kuyafanya na hadi kuyazindua hivi ni sehemu ya Utekelezaji wa yale yaliyokuwa katika ILANI ya Chama Tawala ( CCM ) Ndugu? Umenishangaza mno!
 
Ndugu zangu, au mimi tu sielewi hii kitu!

Nauliza ili nipate kujua, nimekuwa nikishangaa huu mkakati wa Paulo Makonda, RC Dar es Salaam. Sijawahi kuona kabla, pengine ni kwa vile sijui!

Kama hiyo haitoshi, anatumia nafasi hiyo kuwadhihaki watu na kuwananga ikiwa mbunge wa eneo la mradi hatokani na chama chake.

Pamoja na ukweli kuwa serikali iliyopo madarakani inatekeleza ilani ya chama chake, ni nini kinawapa umiliki namna hii?

Miradi ya maendeleo, miradi ya serikali, ni vipi inakabidhiwa kwa chama? Je, ni mali ya chama?

Maendeleo hayana vyama!

Wasalaam,

Ncha Kali.
Kama kawaida yao wanajiona kuwa wapo juu ya sheria
 
Back
Top Bottom