Ni kwanini Mkoa wa Pwani unaongoza kwa kutoa viongozi wa kitaifa?

Ni kwanini Mkoa wa Pwani unaongoza kwa kutoa viongozi wa kitaifa?

Akilihuru

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2022
Posts
1,512
Reaction score
2,980
Kwema ndugu zangu. I hope kila mtu ni mzima.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Mkoa wa Pwani pamoja na kwamba wenyeji wa mkoa huo wengi hawana elimu ya kutosha, lakini ndio unaoongoza kwa kutupa watanzania viongozi wakuu wa kitaifa haswa kwa upande wa ukuu wa nchi.

Toka Tanzania ipate uhuru mkoa wa Pwani umeshatupatia watanzania maraisi watatu nao ni:

1) Rais mstaafu wa awamu ya pili ndugu Ali Hassan Mwinyi (mzanzibara) kutoka Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.

2) Rais mstaafu wa awamu ya nne ndugu Jakaya Mrisho Kikwete kutoka chalinze mkoa wa Pwani.

3) Rais wa Zanzibar ndugu Hussein Ali Mwinyi (mzanzibara) mwenye asili ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.

Hapo sijazungumzia mawaziri kama kina Mchengerwa, Jafo, Ridhiwani, Kawambwa na wengineo.

Lakini pia Mkoa wa Pwani ndio uliokuwa unaongoza kutoa viongozi wengi katika vuguvugu lile la vyama vya kupigania uhuru hapa Tanganyika.

Sasa swali je ni kwa nini mkoa huu huwa na bahati ya kutoa viongozi wengi wakuu wa kitaifa.

a) Kwa sababu ya upendo wao, ucheshi wao, utu wao, huruma yao, ukarimu wao, utanashati wao na usmart wao?

b) Au ni kwa sababu ya uaminifu wao, upole wao, uzoefu wao, umaarufu wao na ujanja ujanja wao?

Naomba tujadili kistaarabu bila matusi, kejeli wala dharau kwa wengine.
 
Watu wa Pwani ni wabinafsi hujiona wao ni bora kuliko wengine ukizingatia na dini yao huamini wao ndio wenye haki ya kutawala.
Kwahiyo mzee Mwinyi na Kikwete walichaguliwa na watu wa Pwani peke yao ili wawe maraisi wa Tanzania?
 
Kuna advantage ya kutawaliwaa na mtu dhaifu. unaweza mpeleka unavyotaka
Kwahiyo wamefanikiwa kushinda katika chaguzi mbali mbali za uraisi na kuwa maraisi wetu sababu ya udhaifu wao? Hili nilikuwa silijui.
 
Back
Top Bottom