Ni kwanini Mkoa wa Pwani unaongoza kwa kutoa viongozi wa kitaifa?

Ni kwanini Mkoa wa Pwani unaongoza kwa kutoa viongozi wa kitaifa?

Kwema ndugu zangu. I hope kila mtu ni mzima.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Mkoa wa Pwani pamoja na kwamba wenyeji wa mkoa huo wengi hawana elimu ya kutosha, lakini ndio unaoongoza kwa kutupa watanzania viongozi wakuu wa kitaifa haswa kwa upande wa ukuu wa nchi.

Toka Tanzania ipate uhuru mkoa wa Pwani umeshatupatia watanzania maraisi watatu nao ni:

1) Rais mstaafu wa awamu ya pili ndugu Ali Hassan Mwinyi (mzanzibara) kutoka Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.

2) Rais mstaafu wa awamu ya nne ndugu Jakaya Mrisho Kikwete kutoka chalinze mkoa wa Pwani.

3) Rais wa Zanzibar ndugu Hussein Ali Mwinyi (mzanzibara) mwenye asili ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.

Hapo sijazungumzia mawaziri kama kina Mchengerwa, Jafo, Ridhiwani, Kawambwa na wengineo.

Lakini pia Mkoa wa Pwani ndio uliokuwa unaongoza kutoa viongozi wengi katika vuguvugu lile la vyama vya kupigania uhuru hapa Tanganyika.

Sasa swali je ni kwa nini mkoa huu huwa na bahati ya kutoa viongozi wengi wakuu wa kitaifa.

a) Kwa sababu ya upendo wao, ucheshi wao, utu wao, huruma yao, ukarimu wao, utanashati wao na usmart wao?

b) Au ni kwa sababu ya uaminifu wao, upole wao, uzoefu wao, umaarufu wao na ujanja ujanja wao?

Naomba tujadili kistaarabu bila matusi, kejeli wala dharau kwa wengine.
Ila mkoa ule ulitoa kiongozi mmoja tu mkubwa ukaandamwa wee zaidi hata ya wamakua

Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
 
Kuhusu viongozi wakuu Nyerere na Magufuli hawakutoka Pwani.
Ila kwa kweli kwenye upigania Uhuru nakuunga mkono Dossa Azizi,Rupia,Familia ya kina Sykes,Chaurembo,Jumbe Tambaza,Ramia,bibi Titi Mohamed,Mshumi kyate na wengine wengi na zaidi ya yote walikuwa waislamu.
 
Kwani akijenga kwao huko kwao ni nchi jirani?au huko kwao wanaishi wahamiaji.
Barabara ya tamco kibaha mpaka njia panda ya vikawe pale baobab.ile barabara NI ya kukosa Rami miaka yote mpaka leo?
Kwahiyo unashauri kila raisi awe anakimbilia kwanza kujenga kwao badala ya ku deal na nchi nzima?
 
Kuhusu viongozi wakuu Nyerere na Magufuli hawakutoka Pwani.
Ila kwa kweli kwenye upigania Uhuru nakuunga mkono Dossa Azizi,Rupia,Familia ya kina Sykes,Chaurembo,Jumbe Tambaza,Ramia,bibi Titi Mohamed,Mshumi kyate na wengine wengi na zaidi ya yote walikuwa waislamu.
Asante mkuu kwa list hii ya wapigania uhuru wetu.
 
Kwani akijenga kwao huko kwao ni nchi jirani?au huko kwao wanaishi wahamiaji.
Barabara ya tamco kibaha mpaka njia panda ya vikawe pale baobab.ile barabara NI ya kukosa Rami miaka yote mpaka leo?
Nafikiri hii inategemea na maono ya mtu. Nyerere hakuwahi kujenga kwao Butiama, Mwinyi hakujenga kwao Mkuranga, Mkapa hakujenga kwao Masasi, Kikwete hakujenga Msoga, ni Magufuli pekee ndio alikuwa na maono ya kujenga kwao.

Hata hivyo alishambuliwa sana na wanasiasa kwa kuonekana kuwa anapendelea kwao nk.
 
Hao ndo wakali wa donta,nyinyi wengine asili yenu ni kulima na kufuga maporini huko.
 
Back
Top Bottom