Hili la watuhuhumiwa kubambikiwa kesi, na kukamuliwa, karma imeisha lishughulikia
Mkuu
Mystery , maadam ni inadaiwa, then acha tuu idaiwe, ila pesa za plea bargain zililipwa kwa maandishi tena kupitia a control number, pesa hizo ziliingia serikalini na pesa ukiisha ingia serikalini, haiwezi kutoka bila maandishi!. Hivyo maandishi ya every cent yapo!.
Fedha kukusanywa na kutofikishwa kwenye mfuko mkuu wa hazina, haina maana ndio zimetafunwa!, ni utaratibu tuu ndio haukufuatwa, hivyo CAG hakuziona ila sio lazima kila fedha ambazo CAG hakuziona ni zimetafunwa!. Enzi za CAG Prof. Asad kuna 1.5B hazikuonekana!. Mbona hakusimamishwa mtu kupisha uchunguzi?. Tulinunua ndege kwa cash cash kwa kuchota kutoko mfuko mkuu hazina na kulipa tulikolipa bila kufuata utaratibu!, mbona hamkuomba uchunguzi?.
Tume ya nini kuchunguza nini wakati maandishi yote ya makisanyo hayo yapo na matumizi yapo?.
Niliwahi kushauri, kama JPM, aliyafanya yote aliyoyafanya na hatukumpangia, basi na Samia tusimpangie!.
Kumefanyika mangapi ndivyo sivyo na hamkuomba uchunguzi, why hili?, nilidhani labda sasa ndio mngeomba uchunguzi wa shambulizi la Lissu ndio ufanyike!, mnaomba uchunguzi wa kitu very systematic kama fedha zilizolipwa kwa control number?. Acheni hizo!.
Usichanganye tuhuma na makosa, hizi ni tuhuma tuu, maadam ni Mama mwenyewe kaamua kuzichunguza bila kupangiwa na yeyote, mwacheni Mama afanye kazi, tuhuma zikithibitishwa, hatua stahiki zitachukuliwa!.
Mungu ibariki Tanzania,
Kazi iendelee...
P