Ni kwanini Rais Samia anashikwa na "kigugumizi" kuunda Tume ya Majaji kumchunguza Biswalo Mganga, aliyekuwa DPP?

Tatizo ni muda au content??

Maana kuna watu hapa kama mleta mada tatizo lake sio sheria bali ni nani kaitunga ndio maana hata wewe umeuliza imetungwa lini?

Malengo hapa ni kutafuta kila njia mradi Magufuli atachafuliwa.

Tatizo ni muda, kwani sheria huangalia muda. Magufuli hakuwa msafi, atachafuliww vipi? Kama mngekuwa na uhakika na usafi wake msingeogopa hatua kuchukuliwa sasa.
 
Kelele zote hizi Mlengwa ni Magufuli tu.
 
Zipo tuhuma nzito Sana zinazomkabili aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga, kuhusiana na kile kinachoitwa "plea bargaining" mtindo uliobuniwa wakati wa utawala wa awamu ya 5, ambapo watuhumiwa "waliobambikiwa" makosa, wakati wa utawala wa awamu ya 5, "walilazinishwa" kukiri makosa na hivyo kukamuliwa mabilioni ya pesa, ambapo inadaiwa kuwa mabilioni hayo hayakufikishwa kwenye hazina ya Taifa hili na badala yake ziliishia kwenye mifuko ya Biswalo Mganga na washirika wake!

Hizi ni tuhuma nzito Sana kumkabili mtumishi wa Umma, tena mwenye hadhi ya ujaji, Biswalo Mganga, ambapo anadaiwa kuwa Kati ya shilingi bilioni 51, alizokusanya kwa njia hiyo ya "plea bargainining" mabilioni mengi, hakuyafikisha hazina, kwa mujibu wa taarifa ya CAG, Charles Kicheere, na badala yake, mabilioni hayo yanasemekana, yaliishia kwenye mifuko ya Biswalo Mganga na washirika wake.

Watuhumiwa hao waliobambikiziwa Kesi, Ili hatimaye walazimishwe kukiri makosa hayo wanayotuhumiwa nayo na baadaye "wakamuliwe" mabilioni hayo ya pesa, wametoa wito kwa Rais wetu, aweze kuunda Tume ya Majaji, kuchunguza tuhuma hizi nzito, wakati huo huo akimsimamisha Kazi ya ujaji, aliyomteua mapema mwaka jana.

Ni utaratibu wa kawaida sana, unaotumika Katika nchi za Jumuiya ya Madola, ambayo nchi yetu ipo, ambapo tunalazimika kufuata.

Swali kubwa ninalojiuliza, ni kwanini hadi hivi sasa, Rais Samia, anashikwa na "kigugumizi" kuunda Tume hiyo ya Majaji, ambayo itatafuta ukweli wa kujua kama tuhuma hizo ni za kweli au la?

Ni vyema Rais Samia, akatambua kuwa kushikwa kwake na "kigugumizi" cha kuunda Tume hiyo ya Majaji,, kutatoa tafsiri kwa wananchi wengi kuwa, yeye Rais ana mpango wa kumwewekea kinga dhidi ya tuhuma anazokabiliwa nazo huyo aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga.

Vile vile itatoa tafsiri kuwa kuna baadhi ya watu hapa nchini, hususani viongozi waandamizi wa Serikali hii ya CCM, wanapewa kinga ya "impunity" ya kutoshtakiwa, hata kama wamefanya makosa makubwa ya jinai, jambo ambalo halitendi haki kwa wananchi, kwa kuwa Katiba yetu inaeleza wazi kuwa wananchi wote, wapo sawa mbele ya sheria.
Achana uchochezii

Kwa kosa ganii

Kwani yote aliyoyafanya alifanya kwa matakwa yake au sharia ilimuelekezaa .

Shida kubwa ya watanzania Sheria ikisimamiwA anaona wanaona wanaonewaa.

Nakuomba Mungu leo hadi kesho na najua Mungu atatupa Kiongozi mzalendo wa kweli kama JPM

Tupate na DPP bwana BWISALU MGANGA Awonyoshee tuheshimiane hapa mjini

Jaribu tujibu ulozi nikulipua
 
Mkuu kolola , usitukane watu wapuuzi, hawa ni wajinga tuu, kwa kutokujua, hivyo kazi yetu ni kuwaelimisha huo ujinga uwatoke!, wajinga wanaoelimishwa lakini ujinga hauwatoki na kuwa werevu, sasa hawa ndio ...
P
Wanaboa
Una umri Gani? Kama ni under 30yrs basi hujui lolote kuhusu tegeta escrow na nani wamiliki halali! Unakumbuka Kikwete alisema Nini juu ya pesa zile kuwa ni Mali ya nani na kwanini alisema vile mbele ya wazee wa Dar? Au basi tuache TU.
zidisha mara mbili na uongeze mingine. Tegeta escrow huijui ila wenzako tunaijua ipasavyo! Hizi sredi na mahangaiko ya biswalo ni mkakati wa walamba asali tu! Inaudhi kuona chadema wanaingia kitoto kwa vile TL naye kalambishwa. Ukiona anayemchukia JPM ujue alikuwa fisadi
 
Mijizi inapaswa kupelekwa mahakamani ili ichukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria, na sio kuporwa fedha zao na genge la Magufuli kwa kichaka cha kupambana na wezi. Sasa pesa zilizokusanywa haifahamiki nyingine ziko wapi. Huwezi kupambana na majizi kwa ujizi.
Tatizo nyie ni wapuuzi tu! Lini majizi yalishinda mahakamani? Kiongozi bora ni yule aliyejitahidi kuzirudisha hizo hela na zikafanya kazi ikaonekana.
 
Unaambiwa 34b hazionekani ziko wapi, unasema zimefanya kazi ikaonekana?! Ni mahakama gani dhalimu alikuwa anaiheshimu mpaka useme majizi wangeweza kushinda mahakamani? Kiongozi jizi anawezaje kuwa bora, au wewe ulikuwa ni mfaidika wa uporaji wake?
 
Biswalo hapo alipo kwa sasa ni Jaji, hii kashfa inamfanya hata atashindwa kufanya majukumu ya ujaji. Kila mtu atakuwa anawasi wasi na uwezo wake kimaadili (integrity), hichi ni kitanzi kibaya sana kwake.

Labda apangiwe majukumu mengine, ila kusikiliza na kuamua kesi mahakamani hapa kashafeli tayari, kashfa zitamfanya asiwe mtu wa kuaminika.
 
Hujui kitu hivyo siwezi poteza muda wangu bure.
Huna unachojuwa zaidi ya kusoma na kuandika na kuhesabu. Muda ulioutumia kupinga nilichoandika laiti ungekuwa "Literate" ungejibu hoja ila kwa vile wewe ni mbumbumbu unaishia majibu mkato
 
Biswalo hapo alipo kwa sasa ni Jaji, hii kashfa inamfanya hata atashindwa kufanya majukumu ya ujaji. Kila mtu atakuwa anawasi wasi na uwezo wake kimaadili (integrity), hichi ni kitanzi kibaya sana kwake.

Labda apangiwe majukumu mengine, ila kusikiliza na kuamua kesi mahakamani hapa kashafeli tayari, kashfa zitamfanya asiwe mtu wa kuaminika.
Absolutely true👏👏👏

Lakini kwa kuwa ndani ya nchi yetu, ni kuwa kitu kufanyika ni lazima Rais ndiyo aridhie na siyo Katiba inavyotaka!

Very sad🥺
 
Hiyo ni integrated system... Ni mfumo wenye chain ya wengi, kutaka kumgusa mmoja ni kutaka kuuchezesha mfumo wote.. Nani atakubali?
Hiki ndio kinachoendelea kuzididimiza Nchi nyingi za Africa. Linatokea tatizo unafanya uchunguzi, mwisho inaletwa ripoti, wahusika karibu wote ni marafiki zako.
 
Rais wa awamu ya 6 ni sehemu ya Uongozi wa awamu iliyopita (awamu ya5),waswahili wanasema ni Vigumu mno kupata jino zima kwenye mdomo uliooza.
 
Unaambiwa 34b hazionekani ziko wapi, unasema zimefanya kazi ikaonekana?! Ni mahakama gani dhalimu alikuwa anaiheshimu mpaka useme majizi wangeweza kushinda mahakamani? Kiongozi jizi anawezaje kuwa bora, au wewe ulikuwa ni mfaidika wa uporaji wake?
Tatizo mnaongea bila tangible evidence! Aziibe JPM azipeleke wapi? Hamna akili nyie, kazi kuzusha tu mkilishwa mauongo na mafisadi yaki na sethi, Kabendera (huyu namfahamu sana)! JPM fought for this nation! Hivi unajua hata Nyerere alipotoka madarakani wengi walizusha? Michadema kujiunga na mafisadi ili kumnang’a JPM hainishangazi ila kuna siku ukweli utajulikana. Let me assure you, JPM mwingine ataibuka hapa Tanzania miaka ijayo
 
Hiki ndio kinachoendelea kuzididimiza Nchi nyingi za Africa. Linatokea tatizo unafanya uchunguzi, mwisho inaletwa ripoti, wahusika karibu wote ni marafiki zako.

Na hata kama sio marafiki zako, unakuta wanaujua uchafu wako wote, hivyo inabidi utoe kwanza boriti kwenye jicho lako!
 
Zipo tuhuma nzito Sana zinazomkabili aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga, kuhusiana na kile kinachoitwa "plea bargaining" mtindo uliobuniwa wakati wa utawala wa awamu ya 5, ambapo watuhumiwa "waliobambikiwa" makosa, wakati wa utawala wa awamu ya 5, "walilazinishwa" kukiri makosa na hivyo kukamuliwa mabilioni ya pesa, ambapo inadaiwa kuwa mabilioni hayo hayakufikishwa kwenye hazina ya Taifa hili na badala yake ziliishia kwenye mifuko ya Biswalo Mganga na washirika wake!

Hizi ni tuhuma nzito Sana kumkabili mtumishi wa Umma, tena mwenye hadhi ya ujaji, Biswalo Mganga, ambapo anadaiwa kuwa Kati ya shilingi bilioni 51, alizokusanya kwa njia hiyo ya "plea bargainining" mabilioni mengi, hakuyafikisha hazina, kwa mujibu wa taarifa ya CAG, Charles Kicheere, na badala yake, mabilioni hayo yanasemekana, yaliishia kwenye mifuko ya Biswalo Mganga na washirika wake.

Watuhumiwa hao waliobambikiziwa Kesi, Ili hatimaye walazimishwe kukiri makosa hayo wanayotuhumiwa nayo na baadaye "wakamuliwe" mabilioni hayo ya pesa, wametoa wito kwa Rais wetu, aweze kuunda Tume ya Majaji, kuchunguza tuhuma hizi nzito, wakati huo huo akimsimamisha Kazi ya ujaji, aliyomteua mapema mwaka jana.

Ni utaratibu wa kawaida sana, unaotumika Katika nchi za Jumuiya ya Madola, ambayo nchi yetu ipo, ambapo tunalazimika kufuata.

Swali kubwa ninalojiuliza, ni kwanini hadi hivi sasa, Rais Samia, anashikwa na "kigugumizi" kuunda Tume hiyo ya Majaji, ambayo itatafuta ukweli wa kujua kama tuhuma hizo ni za kweli au la?

Ni vyema Rais Samia, akatambua kuwa kushikwa kwake na "kigugumizi" cha kuunda Tume hiyo ya Majaji,, kutatoa tafsiri kwa wananchi wengi kuwa, yeye Rais ana mpango wa kumwewekea kinga dhidi ya tuhuma anazokabiliwa nazo huyo aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga.

Vile vile itatoa tafsiri kuwa kuna baadhi ya watu hapa nchini, hususani viongozi waandamizi wa Serikali hii ya CCM, wanapewa kinga ya "impunity" ya kutoshtakiwa, hata kama wamefanya makosa makubwa ya jinai, jambo ambalo halitendi haki kwa wananchi, kwa kuwa Katiba yetu inaeleza wazi kuwa wananchi wote, wapo sawa mbele ya sheria.
Mkuu Mystery huu ndiyo muda mwafaka wa mada yako. njoo huku
 
Nikusaidie wewe bush lawyer. Sheria Ile ilitungwa na kufanya kazi kabla ya kuwekewa kanuni zake na hapo ndipo kwenye utata! Uwe unatafiti kabla ya kupata hewani!

Sio kila Sheria inatungiwa kanuni wewe kilaza
 
Mkuu Mystery huu ndiyo muda mwafaka wa mada yako. njoo huku
Kwa kauli hii ya Rais wetu hapo Jana kuhusiana na pesa za "plea bargaining" ni muhimu Jaji Biswalo ajiuzulu mara Moja Ili apishe uchunguzi.

Hilo siyo ombi, Bali anawajibika kufanya hivyo, kama Bado anapenda kulinda hadhi yake, Ili baadaye asije aibika
 
Back
Top Bottom