Ni kwanini Rais Samia anashikwa na "kigugumizi" kuunda Tume ya Majaji kumchunguza Biswalo Mganga, aliyekuwa DPP?

"Zilitakiwa kuwa deposited kwenye mfuko mkuu wa hazina ndipo CAG azione" sasa kam hilo halikufanyika huo kwangu ndio wizi wenyewe, na hayo ndio matumizi mabaya ya fedha za serikali.
Pascal Mayalla anatulisha matango pori...eti zililipwa kwa pin namba, ngoja nicheke...!

1666240709647.png

Je ni kweli hizo kweli zililipwa kwa pin number...?
Hata hivyo tume hiyo haiwezi kuundwa na serikali hii. Si busara kukata tawi ulilolikalia na huo ndio ukweli.
 
Pascal hata manispaa wanakupa control number na hela zinaishia mifukoni mwa wakurugenzi.

Mheshimiwa aliwahi kusema yeye na mwendazake ni kitu kimoja. Na kutokana na kazi nzuri iliyotukuka ya Jaji Biswalo akapata promotion ya ujaji. Haitakuwa na logic kumuundia tume wewe uliyempromote tena eti uchunguze tuhuma za ubadhirifu.

Hili nadhani litaisha hivihivi. Ccm wanajuana hali zao na tamaduni zao inapokuwepo nafasi ya kuliletea taifa mapato ghafi. Nimeangalia Uingereza habari asubuhi hii kweli wazungu wako na akili yaani prime minister wao wote wanampa makavu hafai itabidi ajiuzulu tuu hakuna namna.
 
Pascal Mayalla anatulisha matango pori...eti zililipwa kwa pin namba, ngoja nicheke...!

View attachment 2392462
Ni kweli hizo kweli zililipwa kwa pin number...​
Hata hivyo tume hiyo haiwezi kuundwa na serikali hii. Si busara kukata tawi ulilolikalia na huo ndio ukweli.
Kuna watu hawana akili aisee, kwa hiyo kutumia pesa bila idhini stahiki sio wizi? Em kwanza ncheke..... [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Akina Pasco na wenzie wanatufanya wajinga sana kana kwamba wao ndio walikuwepo wakati uhuni huu unafanyika, dpp alilipwa cash sio control no.
Mnawatetea wezi...

Aliekua anatupigia kelele za kua ataunda mahakama ya mafisadi kumbe ndio alikua fisadi mkuu ndio maana hakuwahi kuunda hiyo mahakama wala kumfunga fisadi yeyote.
 
Judiciary yetu IMO mifukoni mwa politicians ndio maana maamuzi yao ni ya kisiasa sio haki, Adv.Mayala anatambua hili ila kwa hofu ya njaa ya utumbo haongei ukweli, nchi yetu fedha nyingi mno zimeliwa na zinaendelea kuliwa na familia chache ambazo zipo well connected na systems, katiba mpya ndio mwarobaini maana all judges watawajibika kuomba nafasi hizo sio kutegemea fadhila za number .
 
Zipo tuhuma nzito Sana zinazomkabili aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga, kuhusiana na kile kinachoitwa "plea bargaining" mtindo uliobuniwa wakati wa utawala wa awamu ya 5, ambapo watuhumiwa "waliobambikiwa" makosa, wakati wa utawala wa awamu ya 5, "walilazinishwa" kukiri makosa na hivyo kukamuliwa mabilioni ya pesa, ambapo inadaiwa kuwa mabilioni hayo hayakufikishwa kwenye hazina ya Taifa hili na badala yake ziliishia kwenye mifuko ya Biswalo Mganga na washirika wake!

Hizi ni tuhuma nzito Sana kumkabili mtumishi wa Umma, tena mwenye hadhi ya ujaji, Biswalo Mganga, ambapo anadaiwa kuwa Kati ya shilingi bilioni 51, alizokusanya kwa njia hiyo ya "plea bargainining" mabilioni mengi, hakuyafikisha hazina, kwa mujibu wa taarifa ya CAG, Charles Kicheere, na badala yake, mabilioni hayo yanasemekana, yaliishia kwenye mifuko ya Biswalo Mganga na washirika wake.

Watuhumiwa hao waliobambikiziwa Kesi, Ili hatimaye walazimishwe kukiri makosa hayo wanayotuhumiwa nayo na baadaye "wakamuliwe" mabilioni hayo ya pesa, wametoa wito kwa Rais wetu, aweze kuunda Tume ya Majaji, kuchunguza tuhuma hizi nzito, wakati huo huo akimsimamisha Kazi ya ujaji, aliyomteua mapema mwaka jana.

Ni utaratibu wa kawaida sana, unaotumika Katika nchi za Jumuiya ya Madola, ambayo nchi yetu ipo, ambapo tunalazimika kufuata.

Swali kubwa ninalojiuliza, ni kwanini hadi hivi sasa, Rais Samia, anashikwa na "kigugumizi" kuunda Tume hiyo ya Majaji, ambayo itatafuta ukweli wa kujua kama tuhuma hizo ni za kweli au la?

Ni vyema Rais Samia, akatambua kuwa kushikwa kwake na "kigugumizi" cha kuunda Tume hiyo ya Majaji,, kutatoa tafsiri kwa wananchi wengi kuwa, yeye Rais ana mpango wa kumwewekea kinga dhidi ya tuhuma anazokabiliwa nazo huyo aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga.

Vile vile itatoa tafsiri kuwa kuna baadhi ya watu hapa nchini, hususani viongozi waandamizi wa Serikali hii ya CCM, wanapewa kinga ya "impunity" ya kutoshtakiwa, hata kama wamefanya makosa makubwa ya jinai, jambo ambalo halitendi haki kwa wananchi, kwa kuwa Katiba yetu inaeleza wazi kuwa wananchi wote, wapo sawa mbele ya sheria.
Mimi naona Rais na kipenzi chetu mama SSH angeunda timu ya kuchunguza EPA, ESCROW, RICHMOND, DOWANS, MIKATABA YA GESI, MIKATABA YA MADINI, WAHUSIKA WA WATUMISHI HEWA n.k ili tuje tuifikie plea bargain maana vinahusiana.
 
Unaweza kuta we kichwa cha familia kabisa...Hakika watoton na mke wamekosa kichwa cha familia
Haya wewe "Binamu" yake Biswalo, naona unamtetea kwa nguvu zote, kwa hizo pesa alizozitafuna huyo Ndugu yako!
 
Mimi naona Rais na kipenzi chetu mama SSH angeunda timu ya kuchunguza EPA, ESCROW, RICHMOND, DOWANS, MIKATABA YA GESI, MIKATABA YA MADINI, WAHUSIKA WA WATUMISHI HEWA n.k ili tuje tuifikie plea bargain maana vinahusiana.
Aunde kwa lengo gani? Kukata tawi alilokalia? Au unaamini yeye hajui pesa za plea bargain zilipo? Mara hii umeshasahau alikuwa ni Vice President wa United Republic of Tanzania? Hivi si yeye aliyempa ujaji Biswalo kati ya Watanzania 65,000,000? Tuacheni utani jamani!
 
Haya wewe kada wa CCM, tueleweshe, jinsi hiyo sheriia ya "plea bargaining" inavyofanya Kazi.

Hata hivyo hapa hatuongelei namna sheria hiyo inavyofanya Kazi, bali tunaongelea, namna hayo mabilioni yaliyokusanywa, yalivyotafunwa na huyo Biswalo Mganga na washirika wake.
Kajifunze mwenyewe.

Ukishaielewa utafahamu kama ni kweli alitafuna au la.
 
Ndugu yangu mtoa hoja;UPIGAJI wa namna hii ni mtandao mkubwa wa wengi.Tena hao hao huko juu.Sasa ukifukua hapa panafumuka pale.Hakuna wa kumfunga paka kengele.
 
Ukweli ni huu HORSE POWER ...wote waliokuwa viongozi wa juu katika serikali ya Magufuli bado wapo, wengine wao katika nyadhifa za juu zaidi Serikalini, Mahakamani na Bungeni. Tena Bungeni ndio usiseme, wapo kwa asilimia 99%.

Magufuli aliwaagiza watu kutekeleza matakwa yake hata pale yalipopishana na Katiba ya nchi. Watekelezaji hao wote bado wapo na wengine wamepandishwa vyeo. Hizi zote ni katika jitihada za kulindana ambayo ni sera kuu ya CCM.

Kumbuka kazi iendeleeee!
 
Zipo tuhuma nzito Sana zinazomkabili aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga, kuhusiana na kile kinachoitwa "plea bargaining" mtindo uliobuniwa wakati wa utawala wa awamu ya 5, ambapo watuhumiwa "waliobambikiwa" makosa, wakati wa utawala wa awamu ya 5, "walilazinishwa" kukiri makosa na hivyo kukamuliwa mabilioni ya pesa, ambapo inadaiwa kuwa mabilioni hayo hayakufikishwa kwenye hazina ya Taifa hili na badala yake ziliishia kwenye mifuko ya Biswalo Mganga na washirika wake!

Hizi ni tuhuma nzito Sana kumkabili mtumishi wa Umma, tena mwenye hadhi ya ujaji, Biswalo Mganga, ambapo anadaiwa kuwa Kati ya shilingi bilioni 51, alizokusanya kwa njia hiyo ya "plea bargainining" mabilioni mengi, hakuyafikisha hazina, kwa mujibu wa taarifa ya CAG, Charles Kicheere, na badala yake, mabilioni hayo yanasemekana, yaliishia kwenye mifuko ya Biswalo Mganga na washirika wake.

Watuhumiwa hao waliobambikiziwa Kesi, Ili hatimaye walazimishwe kukiri makosa hayo wanayotuhumiwa nayo na baadaye "wakamuliwe" mabilioni hayo ya pesa, wametoa wito kwa Rais wetu, aweze kuunda Tume ya Majaji, kuchunguza tuhuma hizi nzito, wakati huo huo akimsimamisha Kazi ya ujaji, aliyomteua mapema mwaka jana.

Ni utaratibu wa kawaida sana, unaotumika Katika nchi za Jumuiya ya Madola, ambayo nchi yetu ipo, ambapo tunalazimika kufuata.

Swali kubwa ninalojiuliza, ni kwanini hadi hivi sasa, Rais Samia, anashikwa na "kigugumizi" kuunda Tume hiyo ya Majaji, ambayo itatafuta ukweli wa kujua kama tuhuma hizo ni za kweli au la?

Ni vyema Rais Samia, akatambua kuwa kushikwa kwake na "kigugumizi" cha kuunda Tume hiyo ya Majaji,, kutatoa tafsiri kwa wananchi wengi kuwa, yeye Rais ana mpango wa kumwewekea kinga dhidi ya tuhuma anazokabiliwa nazo huyo aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga.

Vile vile itatoa tafsiri kuwa kuna baadhi ya watu hapa nchini, hususani viongozi waandamizi wa Serikali hii ya CCM, wanapewa kinga ya "impunity" ya kutoshtakiwa, hata kama wamefanya makosa makubwa ya jinai, jambo ambalo halitendi haki kwa wananchi, kwa kuwa Katiba yetu inaeleza wazi kuwa wananchi wote, wapo sawa mbele ya sheria.
Kwa hiyo mumemuona Rais ,wa sasa mnaweza kumupangia ujinga na upumbavu wenu mnaofikiri.Tatizo timu Msoga wengi vilaza.Uwezo wa kufikiria upo chini sana.Wakati Biswalo anafanya kazi alikuwa chini ya JPM na Samia.Sasa Samia atajichunguza vipi?Elimu !!Elimu!Lowasa,2015.
 
Mama Samia ni mwana CCM kwanza, hawezi kuandaa mchakato wa kudhalilisha chama chake.

Nchi zote zimefanya mambo kama haya baada ya mabadiliko ya vyama. Hapa tusahau
 
Zipo tuhuma nzito Sana zinazomkabili aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga, kuhusiana na kile kinachoitwa "plea bargaining" mtindo uliobuniwa wakati wa utawala wa awamu ya 5, ambapo watuhumiwa "waliobambikiwa" makosa, wakati wa utawala wa awamu ya 5, "walilazinishwa" kukiri makosa na hivyo kukamuliwa mabilioni ya pesa, ambapo inadaiwa kuwa mabilioni hayo hayakufikishwa kwenye hazina ya Taifa hili na badala yake ziliishia kwenye mifuko ya Biswalo Mganga na washirika wake!

Hizi ni tuhuma nzito Sana kumkabili mtumishi wa Umma, tena mwenye hadhi ya ujaji, Biswalo Mganga, ambapo anadaiwa kuwa Kati ya shilingi bilioni 51, alizokusanya kwa njia hiyo ya "plea bargainining" mabilioni mengi, hakuyafikisha hazina, kwa mujibu wa taarifa ya CAG, Charles Kicheere, na badala yake, mabilioni hayo yanasemekana, yaliishia kwenye mifuko ya Biswalo Mganga na washirika wake.

Watuhumiwa hao waliobambikiziwa Kesi, Ili hatimaye walazimishwe kukiri makosa hayo wanayotuhumiwa nayo na baadaye "wakamuliwe" mabilioni hayo ya pesa, wametoa wito kwa Rais wetu, aweze kuunda Tume ya Majaji, kuchunguza tuhuma hizi nzito, wakati huo huo akimsimamisha Kazi ya ujaji, aliyomteua mapema mwaka jana.

Ni utaratibu wa kawaida sana, unaotumika Katika nchi za Jumuiya ya Madola, ambayo nchi yetu ipo, ambapo tunalazimika kufuata.

Swali kubwa ninalojiuliza, ni kwanini hadi hivi sasa, Rais Samia, anashikwa na "kigugumizi" kuunda Tume hiyo ya Majaji, ambayo itatafuta ukweli wa kujua kama tuhuma hizo ni za kweli au la?

Ni vyema Rais Samia, akatambua kuwa kushikwa kwake na "kigugumizi" cha kuunda Tume hiyo ya Majaji,, kutatoa tafsiri kwa wananchi wengi kuwa, yeye Rais ana mpango wa kumwewekea kinga dhidi ya tuhuma anazokabiliwa nazo huyo aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga.

Vile vile itatoa tafsiri kuwa kuna baadhi ya watu hapa nchini, hususani viongozi waandamizi wa Serikali hii ya CCM, wanapewa kinga ya "impunity" ya kutoshtakiwa, hata kama wamefanya makosa makubwa ya jinai, jambo ambalo halitendi haki kwa wananchi, kwa kuwa Katiba yetu inaeleza wazi kuwa wananchi wote, wapo sawa mbele ya sheria.
Mkuu kwa mimi.. twende pole pole.. hii ni nchi, kuna mambo kutokana na msingi wake hayawezi kufanyika kwa haraka tena kwa mlipuko, kwani kama hili jambo ni kweli basi ujue wahusika ni wengi mno mno, kwa sababu vilio vya watu ni vingi hii lazima Mungu atasikia.. kweli watalipa uovu huo.. huyu mheshimiwa hawezi tenda hilo peke yake na hao unao waita sijui "washirika" futa usemi wako.. hao ni vingunge "NGOMBALE MWIRU" wakitajwa hutokaa uamini......
 
Mkuu haya majibu yako ni kama ya wale wanaosemaga "kwanini hamkusema wakati mwendazake akiwa hai?". Wakati ule hadi picha zilikuwa zikipostiwa watu wakiwa na maburungutu ya pesa wakilipa DPP hukuwa ukiona? Majibu yako yote sijaona point kabisa uliyoandika.
Heheheeeee.. kazi kweli kweli.... haya.. mie napita tu..
 
Mshana Jr
Sasa kama Rais ataendelea kushikwa na "kigugumizi" cha kuunda Tume ya Majaji, wananchi tutabaini kuwa kumbe wote hao viongozi wa CCM, wapo kwenye mkumbo mmoja, wa kutaka kuendelea kutuibia sisi watanzania! Full Stop
kwani mpaka leo hujui?umeambiwa huo ni mfumo ukitaka kuutikisa umetikisa system yote kwa hiyo nani anataka system ipalaizi?katiba ndo mbadala wa yote hayo vinginevyo tutacheza sindimba tu hapa.
 
Back
Top Bottom