Ni kwanini Rais Samia anashikwa na "kigugumizi" kuunda Tume ya Majaji kumchunguza Biswalo Mganga, aliyekuwa DPP?

Yaani aunde tume kumchunguza mtu aliyekuwa anawasaidia wao katika kutekeleza mambo waliyokuwa wanafanya!? Haiji kutokea hiyo
 
Hahaaa unajitahidi sana kukitetea chama!.

Sijui kwanini hawakuoni, au bado wanakupima. Keep it up!.

Sasa anatetea nini Hapo na kakuambia simple fact. Kasome kwanza. Acha kuwa na mambo ya Vyama Vyama kwenye mijadala ya kimantiki.
 
Mag3
Hapa Solution ni kupata Katiba mpya, tena ile Rasimu ya Jaji Warioba, ambayo ndiyo maoni ya wananchi
 
Huyu anasiri nyingi. Si faida kwa Serikali kumfungulia mashtaka. Ni hatari kwa serikali yenyewe.
 
Tanzania wasomi ni wachache ukimtoa utampata wapi mwingine? Huoni hata mawaziri wanajirudia rudia hatuna nafasi ya kutengeneza nguvu kazi mpa
 
Huyu anasiri nyingi. Si faida kwa Serikali kumfungulia mashtaka. Ni hatari kwa serikali yenyewe.
Zawadi Ngoda
Kuna msemo wa kiswahili unaosema,.. mficha ficha maradhi, mwisho kilio kitamwumbua...........

Kama Hawa CCM, wanaona hiyo ndiyo njia muafaka, watambue kwamba na sisi wananchi, tumebaini ukwapuaji mkubwa wa mabilioni ya shilingi, unavyofanywa na Serikali hii ya CCM

Kwa hiyo solution pekee ni kuwaondoa jumla jumla, hao wakwapuaji, kwenye sanduku la kura, muda ukiwadia.
Time will tell
 
Tanzania wasomi ni wachache ukimtoa utampata wapi mwingine? Huoni hata mawaziri wanajirudia rudia hatuna nafasi ya kutengeneza nguvu kazi mpa
Hizo nafasi kujirudia rudia, siyo k sababu watanzania wasomi hawapo, la hasha, bali inatokana na mfumo wa kiutawaka wa CCM, ambao wanaogopa kuweka sura mpya zenye kutaka kuleta mageuzi kisiasa na kiuchumi
 
Elewa kwanza sheria ya plea bargaining ndio uje kulalamika hapa.

Maana unaweza leta lawama out of ignorance.
Nikusaidie wewe bush lawyer. Sheria Ile ilitungwa na kufanya kazi kabla ya kuwekewa kanuni zake na hapo ndipo kwenye utata! Uwe unatafiti kabla ya kupata hewani!
 
Mna mawazo ya kijinga! Na utoto mwingi. Tume ya nini na wakati mijizi kama Kabendera na akina sethi walishikishwa adabu. Umesahau mara hii Tegeta escrow wajinga nyie
Una umri Gani? Kama ni under 30yrs basi hujui lolote kuhusu tegeta escrow na nani wamiliki halali! Unakumbuka Kikwete alisema Nini juu ya pesa zile kuwa ni Mali ya nani na kwanini alisema vile mbele ya wazee wa Dar? Au basi tuache TU.
 
Nikusaidie wewe bush lawyer. Sheria Ile ilitungwa na kufanya kazi kabla ya kuwekewa kanuni zake na hapo ndipo kwenye utata! Uwe unatafiti kabla ya kupata hewani!
Bora unemfafanulia ukweli huyo jamaa🤝
 
Vipi kuhusu walioumizwa? Hawana haki ya kupoozwa?
Kumgusa Jaji ni kugusa maslahi ya wengi sana wafaidikaji. Hawawezi kukubali na yuko hapo alipo kwasababu...
 
Elewa kwanza sheria ya plea bargaining ndio uje kulalamika hapa.

Maana unaweza leta lawama out of ignorance.

Kwamba hiyo sheria inapeleka hela kwa watu binafsi, hakili ya hovyo sana hiii
 
Mshana Jr
Sasa kama Rais ataendelea kushikwa na "kigugumizi" cha kuunda Tume ya Majaji, wananchi tutabaini kuwa kumbe wote hao viongozi wa CCM, wapo kwenye mkumbo mmoja, wa kutaka kuendelea kutuibia sisi watanzania! Full Stop

Mkuu iwapo nchi itapinduliwa, au chama kingine kuingia madarakani hilo linaweza kufanyika. Lakini CCM iliyoko madarakani kwa maagizo ya Magufuli usitegemee hilo.
 
Ilitungwa lini ?
Tatizo ni muda au content??

Maana kuna watu hapa kama mleta mada tatizo lake sio sheria bali ni nani kaitunga ndio maana hata wewe umeuliza imetungwa lini?

Malengo hapa ni kutafuta kila njia mradi Magufuli atachafuliwa.
 
Mna mawazo ya kijinga! Na utoto mwingi. Tume ya nini na wakati mijizi kama Kabendera na akina sethi walishikishwa adabu. Umesahau mara hii Tegeta escrow wajinga nyie

Mijizi inapaswa kupelekwa mahakamani ili ichukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria, na sio kuporwa fedha zao na genge la Magufuli kwa kichaka cha kupambana na wezi. Sasa pesa zilizokusanywa haifahamiki nyingine ziko wapi. Huwezi kupambana na majizi kwa ujizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…