Ni kwanini sasa miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika iadhimishiwe jijini Mwanza?


Wenye Maono makali na yaliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu nikiwemo GENTAMYCINE ni Siku Tatu sasa zimepita nilianzisha Uzi hapa hapa JamiiForums Kuzungumzia hili na Kuelezea wasiwasi wangu mkubwa juu ya Sherehe hizi Kufanyika Mkoani Mwanza na Mheshimiwa Kukubali kuwa Mgeni rasmi tofauti na miaka mingine ambapo alikuwa akiihairisha kwa kile alichokiita Kubana Matumizi ila wapo ambao kwa ' Upopoma ' Wao tu hawakunielewa, lakini bila Shaka baada ya Wewe nawe kuja na huu Uzi basi wenye Akili wataongezeka na watatuelewa pia. Kuna tatizo mahala na ' Usukumaism ' sasa ' Umetamalaki ' nchini Tanzania na katika Sekta mbalimbali na hasa hasa Makao Makuu Upanga na Makao Makuu Oysterbay.
 
Huna akili wewe
 
Mkuu, wanabisha jambo ambalo wanajua wazi kuwa Rais anafanya hivi kama kupeleka fadhila kwa wasukuma kama ambavyo amekuwa akifanya. Wanataka kupindisha ukweli kwa hoja zao za kijinga kabisa!
 
Achen porojo! Mwanza nisehemu ya Tanganyika mnasema hivo kwasababu ametokea kanda ya ziwa zaidi ya hapo hamnahoja yoyote
Hivi Mkapa alishindwa kufanya haya huko Mtwara tena eneo hasa lololotumika kwa ukombozi?
 
Mkuu G Sam, unamsaidia huyo unayesema anaibomoa Tanzania kwa bandiko lako hili; huenda bila ya kukusudia kufanya hivyo.
Hebu yatafakari tena vizuri haya uliyoyaandika hapa juu.
 
Nimekuelewa Sana mtoa uzi nami niliposikia kwamba sherehe za Uhuru zitafanyika mwanza kwenye uwanja wa CCM kirumba nikajua tayari Jiwe kaendeleza ukanda na ukabila wake,leo Nyerere road yote nyeupee peee Machinga wote wameondolewa
 
Mleta mada nadhani ubongo wake haukufanya kazi ipasavyo pindi alipofikiria kuleta mada yake. Mada ingekuwa na mashiko kama angezungumzia gharama za kufanya sherehe mwanza kuliko kuzungumzia ukabila kitu ambacho kimefanya mada yake kukosa nguvu kihoja
 
Nimekuelewa Sana mtoa uzi nami niliposikia kwamba sherehe za Uhuru zitafanyika mwanza kwenye uwanja wa CCM kirumba nikajua tayari Jiwe kaendeleza ukanda na ukabila wake,leo Nyerere road yote nyeupee peee Machinga wote wameondolewa
Halafu anatuambia kuwa anakwepa gharama.Sijui wasukuma walimpa nini? Nakumbuka aliposema walimpa kura nyingi hivyo wasibomolewe ila huko kwingine tunaambiwa ukisogelea road reserve umejipelekea umasikini.
 
Imekuwa ni tabia ya Nchi ya Tanzania kuendesha sherehe za kitaifa kwa kuzunguka toka mkoa au kanda fulani kwenda nyingine, na ndio ilisaidia ujenzi wa viwanja vya mpira mikoa mingi kama uwanja wa majimaji, wa singida, nk, hivyo hata hizi kufanyika Mza ni sawa tu na ndio inatakiwa kuwa in rotate, au wewe hilo halikupendeziiiiiii.
 
Kwahiyo mzunguko uanze 2019 tens nyumbani kwa Rais..Haya bwana! Ninachojua ni kuwa ameenda kubembeleza kura za wasukuma kama kawaida yake maana sherehe zijazo tutakuwa tumemaliza uchaguzi mkuu.
 
Wahenga husema kuna 'mtu kuamkia upande mbaya'.
G Sam ninayemfahamu kwa michango yake humu JF, leo ni tofauti na G Sam mwenye mada hii.

Kama ni kulaumu, elekeza lawama hizo kwa huyo aliyeamua kupeleka sherehe hizo huko kwao. Hii itaeleweka, na inaeleweka kabisa kwa tabia anazoonyesha. Hata huko kuzungumza kilugha tu kwenye mikutano hiyo ni kero tosha.

Sasa G Sam, kuhusisha watu wote wa 'ukanda' kana kwamba ndio waliochukua madaraka ya kuhamisha sherehe hizi, kweli inakuwa ni sawa?

Mimi siamini kamwe kwamba Tanzania hii itabomolewa na mtu mmoja. Sikubali kabisa mawazo hayo. Ila ninachkiamini ni kwamba hilo litawezekana endapo kama tutakuwa na watu kama G Sam huyu mpya, atakayesaidia kutia kichocheo cha kuibomoa Tanzania.
 
Sina shida na watu wa kabila lile mkuu. Mbona hata wapinzani wakienda kule wanapokewa vizuri tu? Nina shida na huyo aliyepeleka sherehe huko! In fact anafanya wasukuma wenzake waanze kufikiriwa tofauti ingawa najua wapo wasiopendezwa na haya. Nakupa mfano wachaga, wahaya, wanyakyusa na wasukuma Nyerere aliwahi kutuonya kuwa wametawaliwa na ubinafsi. Sasa hatukuwahi kumpata Rais kwenye makabila hayo hapo kabla ila sasa tumempata Magufuli na ameenda mulemule alikoonya Nyerere. Hii inajenga taswira kwamba tumeshakanyaga nyoka sasa siku tukiona jani tushtuke! Kusema kweli hapo kabla sikutegemea kuona haya ninayoyaona. Mpaka huwa najiuliza hivi kuna watu huwa hawaoni aibu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…