Ni kwanini ukikutana na Wanaotoka Tamasha la Mwakasege na Mwamposa Kawe unaiona tofauti hii Kubwa?

Jifunze kuelewa
 
Siku nyingine umuongeze na Mch. Mgogo utagundua hawa wafuasi wake wanaongoza kwa kupewa madongo huku wanachekeshwa huku wanaambiwa ukweli. Neno la Mungu ni chache, Zinaongelewa inshu za Matatizo ya maisha yetu ya kilasiku na Saikolojia.

Kwa Mwakasege kuna upako wa Mungu wa kiuhalisia. Unatoka kwake ukiwa umebarikiwa na ukiwa na amani

Kwa Mwamposa ni full miujiza. Ni rahisi kuona kama hawa watu wanaandaliwa kuongea ushuhuda. Hawa wa hivi kuna siku ukweli utakuja kubainika kama ni nguvu ya Mungu au la.
 
Mungu ndo ajuaye ukweli
na mtazamo wako siyo kipimo cha ukweli
vigezo ulivyotumia ni vya hovyo sana, vya chuki binafsi
afadhali hata ungetumia biblia kama kipimo
 
Waumini wa mwamposa wanavurugu sana majuzi mama mmoja alinipiga ngumi ili nipishe mlango aingie kwenye daladala, wachunguzwe sana maana ni wababe mno
 
Mwenyezi mungu azidi kutusaidia asee na akusaidie mfalme wa jamii forum uendelee kutupa madini
Amina sana Mkuu, Ubarikiwe na tuko pamoja. Kikubwa ashukuriwe Mwenyezi Mungu kwa Tunu / Shani zake Kwangu.

Asanteni nanyi pia kwa Kuutambua Mchango na kuona Umuhimu wa Kiuwasilishaji wa Kimasuala hapa JamiiForums.
 
Pompoma mchambuzi wa mchongo,chuki zako kwa bulldoza zimevuka viwango,ila cha kusikisha utaendelea kumuona ana stawi kila uchwao huku wewe ukiendelea kupatwa na sonona kila uchwao.
Wewe ni jiwe chakavu na wala siyo angavu [emoji16][emoji16]
 
Hao wote wanaamini mtoto wa bikira Maryam,yule fundi seremala kuwa ni Mungu!?
 
Ubarikiwe kwa kujua utumishi wa kweli haunaga mazingaumbwe mtumishi wa Bwana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…