Ni kwanini unajenga nyumba ya ghorofa?

Ni kwanini unajenga nyumba ya ghorofa?

Kwani nondo mmenunua tani moja shilingi ngapi? 12mm
Nondo tumetumia mchanganyiko kutokana na mahitaji. Mm 8, 12 na 16 zote. Sikumbuki specific price ila kuna za mil 2 per tone ila tulitumia za mil 18-22. Tofali 10 kwenda chini. Mifuko 150 ya cement kwa jamvi. Kuna mawe, vifusi vya kutosha kwenye jamvi pia
 
Hakikisha una mchoro uliochorwa na wataalam (Architect & Engineer), kisha ukapitishwa manispaa au Halmashauri husika. Usikariri gharama, angalia hesabu. Kwa mfano, nyumba ya ghorofa ya familia moja (vyumba 3-4) itatumia nondo kati ya tani 3-4. Na bei za nondo tani moja ni kati ya 1,600,000-2,200,000.

Pia kumbuka. Kwa mujibu wa taratibu wa ujenzi. Ili ujenzi ufanyike lazima uwe na bango la ujenzi, hii itapelekea umlipe Architect, Engineer na Quantity Surveyor Kama Consultants. Kisha Mkandarasi ajenge jengo huku akisimamiwa na Consultants. Huo mzunguko wote hapo ndipo wengine wanapigwaa pesa saana. Ila kama ukipata mtu wa kukuongoza vizuri hapo utafanya saving nzuri tu.

Msikariri msingi mzuri wa 14m,25m na kadharika. Pia msikariri kuwa nyumba ya ghorofa lazima iwe na nguzo. Maana jengo linaweza kujengwa hadi ghorofa nne bila hata nguzo. Maana kuna framed structure (ambapo nguzo ndio hubeba uzito wote) na Load bearing wall (hii ukuta hujengwa kwa kulazwa tu na uzito wote hubebwa na ukuta) ukienda Darajani-Zanzibar kuna majengo mengi yana ghorofa nne yalijengwa na Rais Karume Senior, hayana nguzo. Kwa hiyo tusiishi kwa kukariri, ila tafuteni wataalamu kwa ushauri zaidi
Labda niwe sijakuelewa vizuri. Kwani load bearing wall huwa haihitaji nondo kwenye footings za msingi au kama msingi umetumia beams kwani unaondoa matumizi ya nondo?
Au inapunguza?
Unaposema load bearing wall, unataka kutuambia ni less costly? Kivipi kwa mfano.
Ungenielewesha ningeshukuru.
 
Kuhusu slab gharama zake ziko hivi

1.Zege 1m2=40,000/= (premix grade 20)
2.Formwork 1m2=25,000 (na milunda au unaweza Kodi steel plate)
3.Nondo za 1m2=15kg x 2,000=30,000/=
4. Kufunga formwork 1m2=5,000

Jumla ni 100,500 kwa mita 1 ya mraba

Wakati huo gharama za kupaua ziko hivi:-

Mabati ya Decra/Fortiza mita moja ya mraba Ni 100,000/=(pamoja na mbao)

Mabati migongo mipana (IT4&5) mita moja ya mraba ni 50,000(Pamoja na mbao)

Halafu gharama ya gypsum board kwa mita moja ya mraba Ni 20,000 (pamoja na mbao)

Hapo nimejaribu kukokotoa gharama zote kwa eneo la ukubwa wa mita moja ya mraba. Kama utahitaji ufafanuzi zaidi sehemu yoyote nijurishe, ili nikipata nafasi nikupe jibu.

Yote kwa yote narudia kusema kuwa, Ni Economical kujenga Ghorofa kuliko nyumba ya kawaida. Tofauti kubwa naiona kwenye ufundi tu.

Kwenye Nyumba ya kawaida unaweza okoteleza fundi yeyote hata kutoka nyumba ya 2 toka kwako (wa 10,000 kwa siku). Hajui hata maana ya mix ratio ya mortar na zege. Nyumba haina hata msingi wa zege chini.Matokeo yake nyumba nyingi za kitaa huchakaa kabisa kabla hata ya miaka 50.

Ghorofa lazima utumie professional fundi ambao Ni wachache saana. Na nyumba itakuwa imara zaidi na itadumu zaidi ya miaka 100.

Hata kwenye nyumba ya kawaida ukitumia professional fundi itakuwa imara zaidi na kudumu zaidi. Tazama majengo mengi ya serikali yalivyo imara
Ok
 
Bujibuji kwa uvutaji bangi kwa kweli hajambo huyu kijana. Wewe umetishia watu kurogwa kama wangejenga mansions tukahisi kuwa bado unaishi kwenye nyumba ya udongo, kumbe umetupotosha tu.
Niko vizuri. Siku hizi unarogwa kwa kutupiwa magonjwa ya kiharusi, presha, kisukari nk. Kisha anakuja kukufariji aliyekuroga, anakupa pole, anakwambia haya ni magonjwa ya kitajiri, vumilia tu utapona
 
Kimsingi ujenzi wa ghorofa sio gharama sana kama mnavyofikiria ,maana kuna watu wanajenga uderground ambazo ni sawa na ghorofa tu na hawalalamiki ,kikubwa ni ukubwa wa nyumba unayotaka kujenga na ramani yako ghorofa sio hatari ni zile nondo tu na cement , kama mtu ana bungalow mivyumba kama nane na vyote master kuna utofauti gani na ghorofa?
 
Niko vizuri. Siku hizi unarogwa kwa kutupiwa magonjwa ya kiharusi, presha, kisukari nk. Kisha anakuja kukufariji aliyekuroga, anakupa pole, anakwambia haya ni magonjwa ya kitajiri, vumilia tu utapona
Kwa maana hiyo unataka kutuambia kuwa huku uchaggani ule uchawi wa Kigoma na Tanga umehamia hapa? Maana haya magonjwa uliyotaja ndiyo magonjwa makubwa ya huku Uchaggani.
 
Labda niwe sijakuelewa vizuri. Kwani load bearing wall huwa haihitaji nondo kwenye footings za msingi au kama msingi umetumia beams kwani unaondoa matumizi ya nondo?
Au inapunguza?
Unaposema load bearing wall, unataka kutuambia ni less costly? Kivipi kwa mfano.
Ungenielewesha ningeshukuru.
Kuna somo pana saana hapa sijui kama litaeleweka kwa kuchat tu. Lakini nitajaribu ku share kile ninachokijua kadri ninatakavyoweza.

Kwanza tambua Engineer ndiye atakayeamua structural design ya jengo kutegemeana na bearing capacity of the soil. Kama akijiridhisha kuwa load bearing wall approach inafaa, maana yake idadi ya nondo itapungua. Maana hakutakuwa na Pad foundation, starter columns,Ground level columns na First level columns. Kumbuka gharama ya kuitengeneza nguzo moja tu kwa kila level ina range 250,000-350,000. Kwa hiyo kama jengo lina nguzo 11 na lina ghorofa moja iwapo ukitumia load bearing wall approach unaweza save si chini ya 11x3x250,000=8,250,000/=. Hapo bado sijaongelea Engineer whether ameweka au ameondoa Plinth/ground beam. Design ya slab huwa haibadiriki kwa sababu ya framed structure approach au load bearing wall approach.
 
Mkiwa watu 6 mnataka kukodi gari kwenda kula bata moshi, Ni economical kukodi Toyota Noah, kuliko kukodi tax 2.Kama unamzigo tan 35. Ni vyema kukodi Scania tractor au behewa la train kuliko kukodi fuso 5. Ukiwa una function ya watu labda 50 kuwasafirisha toka mikoani Ni vyema kukodi bus 1 kuliko Costa 2 ,hiece 4 au Noah 8. Unit cost inapungua pale mzigo unakuwa mkubwa. Hata bei ya mafuta ya kula lita moja na ukichukua dumu la lita 20 utakutana na saving flani. Ni kwa sababu ya sharing factor.

Hata ujenzi una obey hiyo principal. Nyumba 2 za kawaida, ukizi-merge into 1(ghorofa), lazima upate saving. Kwa sababu kuna vitu vitakuwa shared (msingi,suspended slab, ceiling) na vingine kuwa omitted kabisa .
 
[
Hapo bado sijaongelea Engineer whether ameweka au ameondoa Plinth/ground beam. Design ya slab huwa haibadiriki kwa sababu ya framed structure approach au load bearing wall approach.
Unaweza kuondoa beams totally na ukawa na load bearing wall
Kwa kutumia cement blocks peke yake?
Hapo top floor itakuwa ya materials gani na Psi ngapi labda kama unaweza kutuelezea.
Yaani hamna frame kabisa?[/QUOTE]
 
Kimsingi ujenzi wa ghorofa sio gharama sana kama mnavyofikiria ,maana kuna watu wanajenga uderground ambazo ni sawa na ghorofa tu na hawalalamiki ,kikubwa ni ukubwa wa nyumba unayotaka kujenga na ramani yako ghorofa sio hatari ni zile nondo tu na cement , kama mtu ana bungalow mivyumba kama nane na vyote master kuna utofauti gani na ghorofa?
unanishauri nijenge ghorofa na engineer au fundi tu wa mtaani?
 
Mie miwili iliyopita nilisimamia ujenzi wa jengo la ghorofa 1, liko Mwandege mkuranga. Ina vyumba vi4 na nguzo 11, Kama sikosei msingi haukuzidi 14,000,000 . Sasa huo msingi wa 45,000,000 Duh!!!!!!!, Anyway labda material yanatoka California
humu JF kumekuwa na exaggeration nyingi sana siku hizi. Ila ukiwa muelewa wa suala husika ama kuwa na exposure ya kutosha ni rahisi kuchuja pumba na mahindi
 
[
Unaweza kuondoa beams totally na ukawa na load bearing wall
Kwa kutumia cement blocks peke yake?
Hapo top floor itakuwa ya materials gani na Psi ngapi labda kama unaweza kutuelezea.
Yaani hamna frame kabisa?
[/QUOTE]Hebu soma vizuri post yangu namba 233. Nimesema kuwa, utumie framed structure au load bearing wall approach haibadirishi uwepo wa suspended slab. Tena nikakutajia vitu pekee vitakavyopungua kwenye load bearing wall approach Ni 1. Pad foundation 2. Starter Columns 3. Ground Level Columns na 4. First floor level columns.

Sikuandika suspended slab au beams zinatoka. Bali nilitoa tahadhari kwenye Plinth/ground beam kuwa inaweza iwepo au isiwepo. Lakini pia Tambua kuwa Plinth/ground beam ni sehemu ya msingi. Ni ule mkanda unaozungushiwa juu ya kuta za msingi. Kwa lugha nyingine vinaenda sambamba na jamvi (Concrete bed).

Lakini pia umeibua kitu kingine ambacho nilikuwa sitaki kukiongelea maana kinaweza kuibua maswali mengi ,na muda wa kuyajibu nikakosa kabisa maana nina jambo flani limenibana saana.

Jambo lenyewe ni kwamba, ni kweli unaweza kujenga suspended slab bila beams. Hiyo approach inaitwa flat slab. Ambacho kwenye slab wanatumia nondo kama kawaida na wakati mwingine wanatumia steel I-section. Ujenzi wa aina hii ni wa nadra saana nchini mwetu. Lakini ukipita mradi mkubwa wa NHC pale Morocco utaona hii kitu. Ninaufahamu kiasi mradi huo maana kipindi cha zabuni za mradi huo nilikuwa mfanyakazi wa NHC, japokuwa nilitoka NHC mradi huo haujaanza, ila michoro yake naikumbuka vzr, lakini pia nikipita barabarani maeneo hayo huwa naziona hizo flat slab.
 
Back
Top Bottom