Ni kwanini unajenga nyumba ya ghorofa?

Ni kwanini unajenga nyumba ya ghorofa?

Mkuu 55mil ni kibosi sana, au mazingira yanachangia pia, manake gharama za nyumba inayojengwa Masaki ni tofauti kabisa na ile inayojengwa Kiluvya, hata ukiweka vitu vingi constant.
Hapana.
Kwa mfano, aina za foundations zinatofautiana.
Eneo Moja ukubwa mmoja Ila inategemea labda footings zako ni ngapi na zinabeba column ya ukubwa gani each. Ukubwa wa nondo na ngapi unahitaji.
Beams zitaenda chini kiasi gani na nondo zake utasuka ngapi na kwa ukubwa upi (diameter).
Slabs (kumbuka zipo mbili, Moja reinforced).
Sanasana utakula nondo nyingi na hapo ndiyo wengine wanaamua kupunguza nondo mradi awe na ghorofa.
 
Hongereni mkuu, 55mil kwa budget zetu za mtaani nyumba ingekuwa imefika mbali mno. Ningeweka roughly 20-25mil kwa foundation tu mkuu, japo landscape inachangia, aina ya udongo, mafundi unaotumia, mazingira uliyopo nk. Factors ni nyingi.
Yes. Mazingira huchangia pia. Sana tu.
 
Hapana.
Kwa mfano, aina za foundations zinatofautiana.
Eneo Moja ukubwa mmoja Ila inategemea labda footings zako ni ngapi na zinabeba column ya ukubwa gani each. Ukubwa wa nondo na ngapi unahitaji.
Beams zitaenda chini kiasi gani na nondo zake utasuka ngapi na kwa ukubwa upi (diameter).
Slabs (kumbuka zipo mbili, Moja reinforced).
Sanasana utakula nondo nyingi na hapo ndiyo wengine wanaamua kupunguza nondo mradi awe na ghorofa.
Na nondo ndo tumeweka ile yenyewe ya msauzi mkuu. Nondo yenye ujazo wa kutosha
 
Tanua mabawa mkuu, utanishukuru baadaye ,winners don't do different things , they just do things differently
Sijakuelewa kuhusu kutanua mabawa Ila hapo itakuwa ume-do a thing different.
There's being "like" and looking "alike".
And sometimes when you loose, you win. When you win, you actually loose.
 
Sijakuelewa kuhusu kutanua mabawa Ila hapo itakuwa ume-do a thing different.
There's being "like" and looking "alike".
And sometimes when you loose, you win. When you win, you actually loose.
Sorry Kama nitakuwa nimemaanisha kitu tofauti cha kukukwaza , nilikuwa unamaanisha jifunze vitu kwa watu tofauti tofauti , that's all , kama imemaanisha kitu offending kwako tuishie hapa na unisamehe bure.
 
Milion 5 kiwanja labda uende chanika

Nenda Goba ukipata kiwanja cha sqm 600+ kwa milion 10 niite ninunue..viwanja hata hapa bongo bado vipo juu..goba kiwanja kizuri kinaanzia milion 15+
Mkuu unamaanisha? Watu tuna njaa zetu ujue?
 
Sorry Kama nitakuwa nimemaanisha kitu tofauti cha kukukwaza , nilikuwa unamaanisha jifunze vitu kwa watu tofauti tofauti , that's all , kama imemaanisha kitu offending kwako tuishie hapa na unisamehe bure.
No not at all.
Ningekuwa nimejifunza Jambo la maana maishani mwangu kama ungefafanua jinsi ya kujenga msingi wa ghorofa kwa Bei nafuu.
Angalau roughly.
 
Ukiwa ghorofani unaona mengi hasa uswahilini, wenye vyoo vya passport kazi kwenu. Ndio manana walimuondoa huyo kijana ili asiwachungulie
 
Usikubali kujengewa foundation ya ghorofa kwa 14mil. Ghorofa ni foundation.
Ukiharibu hapo, utajuta.
Hakikisha una mchoro uliochorwa na wataalam (Architect & Engineer), kisha ukapitishwa manispaa au Halmashauri husika. Usikariri gharama, angalia hesabu. Kwa mfano, nyumba ya ghorofa ya familia moja (vyumba 3-4) itatumia nondo kati ya tani 3-4. Na bei za nondo tani moja ni kati ya 1,600,000-2,200,000.

Pia kumbuka. Kwa mujibu wa taratibu wa ujenzi. Ili ujenzi ufanyike lazima uwe na bango la ujenzi, hii itapelekea umlipe Architect, Engineer na Quantity Surveyor Kama Consultants. Kisha Mkandarasi ajenge jengo huku akisimamiwa na Consultants. Huo mzunguko wote hapo ndipo wengine wanapigwaa pesa saana. Ila kama ukipata mtu wa kukuongoza vizuri hapo utafanya saving nzuri tu.

Msikariri msingi mzuri wa 14m,25m na kadharika. Pia msikariri kuwa nyumba ya ghorofa lazima iwe na nguzo. Maana jengo linaweza kujengwa hadi ghorofa nne bila hata nguzo. Maana kuna framed structure (ambapo nguzo ndio hubeba uzito wote) na Load bearing wall (hii ukuta hujengwa kwa kulazwa tu na uzito wote hubebwa na ukuta) ukienda Darajani-Zanzibar kuna majengo mengi yana ghorofa nne yalijengwa na Rais Karume Senior, hayana nguzo. Kwa hiyo tusiishi kwa kukariri, ila tafuteni wataalamu kwa ushauri zaidi
 
Km 37 kutoka town centre mbali sana hapo ni sawa na mtu atoke arusha mjini akanunue kiwanja kikatiti huko ndani ndani halafu aseme amenunua mjini, Hapo no sawa na kupoteza ela yako sababu hata ukija kutaka kuuza au kutaka uiweke dhamana wale watu wanaofanya valuasheni huwa wanaangalia nyumba kiwanja kiko umbali gani kutoka city centa kwa hio jinsi nyumba kuwanja chako kinavyokua mbali na mji ndivyo unavyojiweka mbali na mafanikio. Nunua kiwanja mjini.
ucsahau miji inakua kwa kasi
 
Baaas baba , huko ambapo kila kitu kipo overated just kwa sababu ya status ya eneo ? Nna chalii yangu amenunua kiwanja huko kwa mil 80 , hata hakifanani.
Ila tumalize tu ubishi kuwa gharama za ujenzi zinategemeana na status mjenzi mwenyewe
Hapana. Material sanasana, kwani ukijenga mbezi beach material ndo unanunulia mbezi beach? Maduka yako kibao. Unaweza ununue mturuki, mjerumani, mchina ama mbongo. Na pia mafundi bora. Si kila fundi ni fundi bora
 
Kwa wanaojua wandamba wa mofu ifakara. Ghorofa ni jadi yao na ni asili tu yao. Wanajenga ghorofa za udongo au tofali za kuchoma. Kwao ni kulinda eneo na nikwaajili ya privacy.
Alafu ww unayesema mijini roughly milioni tano kiwanja upo mji gani ww?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Back
Top Bottom