Ni kwanini unajenga nyumba ya ghorofa?

Ni kwanini unajenga nyumba ya ghorofa?

Hujafanya vizuri cost analysis kati ya nyumba za kawaida na ghorofa. Naomba nikupe mwongozo kidogo tu. Kwa mfano unahitaji nyumba 2 zinazofanana. Itakuwa faida kwako ukijenga katika mfumo wa ghorofa au ujenge moja moja?

Faida za Ghorofa.
-ukijenga ghorofa ni sawa na kupata eneo jingine bure kabisa (Saving)
-Ukijenga ghorofa, ni kweli gharama ya msingi itaongezeka (Kwa 120%-150%) ukilinganisha na nyumba ya kawaida. Lakini kumbuka huo msingi unabeba nyumba 2 (hiyo ni saving)
-Kumbuka floor iliyopo ina serve kazi mbili.1 Ni paa kwenye nyumba ya chini,2 ni msingi kwenye nyumba ya juu. (2 in 1 hiyo ni saving)
-kwenye ghorofa, huhitaji kuweka ceiling kwenye nyumba ya chini (Hiyo ni serving)

Hayo ni Kwa uchache tu faida za Ghorofa. Lakini ukijenga nyumba 2 tofauti, gharama zitakuwa Mara 2 , tofauti na kwenye ghorofa hazitakuwa double kwa sababu ya baadhi ya vitu kuwa shared. Hata waswahili walisema umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu.

Pia chukulia familia mbili tofauti zenye watu watatu watatu. Zikiungana kuwa moja, gharama za matumizi zitakuwa ndogo ukilinganisha na pale Kila familia inaishi kivyakevyake.

Kwa hiyo "Sharing factor" siku zote hupunguza gharama (unit cost) kwenye mambo mengi hata kwenye ujenzi pia (ghorofa).

Nimeeleza kwa uchache ngoja niishie hapo. Lakini pia na declare interest kuwa Mimi Ni Quantity Surveyor (QS) kwa hiyo nimesomea ujenzi, na ninauzoefu wa kutosha kwenye ujenzi wa majengo na barabara kwa zaidi ya miaka 10.
Hapo saving ipo kwenye eneo la bure tu hapo juu. Kwingine haufanyi saving yoyote,mfano jamvi la kati gharama zake zinazidi msingi na kupaua nyumba ya kawaida pamoja na ceilling.piga hesabu kuanzia gharama zote za selemala na fundi wa chuma (nondo).
 
View ya bahari.

Mfano mzuri Pemba Mnazi saa hizi ni kama Mbweni mpya. Watu wenye beach Front wana ghorofa kwa hiyo ukisogea nyuma kidogo na ukajenga ghorofa moja unaiona bahari ingawa kiwanja siyo beach front.

Hata Salasala hivyohivyo.

Ukitoka balcony unaiona bahari, au ukiwa bedroom.
Mbona hata tukiwa china tunatembea tunaona bahari sasa!
 
View ya bahari.

Mfano mzuri Pemba Mnazi saa hizi ni kama Mbweni mpya. Watu wenye beach Front wana ghorofa kwa hiyo ukisogea nyuma kidogo na ukajenga ghorofa moja unaiona bahari ingawa kiwanja siyo beach front.

Hata Salasala hivyohivyo.

Ukitoka balcony unaiona bahari, au ukiwa bedroom.

Mkuu unaweza kunipa namba za dalali wa pemba mnazi? Kuna mzungu mtalii alikuwa anataka plot karibu na beach amjengee mjengo demu wake.
 
Wazungu walijenga nyumba za ghorofa kutokana na uhaba wa ardhi kwao. Nimekutana na Wafrika Magharibi pia mawazo yao ni ya kujenga ma ghorofa. Nikipowauliza sababu waliniambia kwao ardhi ni ghali sana. Kupata kiwanja cha kujenga nyumba inakulazimu uwe na kuanzia milioni 20 kwa pesa ya Tanzania. Wanasema ukijenga ghorofa hukosi mpangaji na wewe unapata na sehemu yako ya kuishi kwa amani.

Wengine wanasema wanajenga ghorofa kuyaona matunda ya mafanikio yake kwa macho. Sasa ninajiuliza sisi ardhi tunayo kubwa sana. Mpaka sasa bei ya kiwanja ni wastaniwa milioni tano mijini. Ni kwanini unawaza kujenga ghorofa kama una wazo hilo au ni kwanini ulijenga ghorofa?


Wengi wanajenga kwa ajili ya kula Upepo mwanana na view.

GHF CONTEMPORARY.jpg
 
Hapo saving ipo kwenye eneo la bure tu hapo juu. Kwingine haufanyi saving yoyote,mfano jamvi la kati gharama zake zinazidi masingi na kupaua nyumba ya kawaida pamoja na ceilling.piga hesabu kuanzia gharama zote za selemala na fundi wa chuma (nondo).
Kweli kabisa slab inakula sana hela maana form work ujue usuke nondo alafu ujue umwage zege...mifuko ya cement inaisha huku unashangaa.

Ghorofa bwana kama sio la biashara ni waste of resources na ni majivuno ya kibinadamu tuu ambayo yote ni ubatili
 
Chief umenigusa kidogo, nina mpango wa kujenga fremu ya ghorofa lakini nahofia gharama za ujenzi mpaka sasa.. Eneo ni linatosha fremu 5 hivi, unaweza kunisaidia hata kupiga hesabu za rough?
Twende PM
 
Kweli kabisa slab inakula sana hela maana form work ujue usuke nondo alafu ujue umwage zege...mifuko ya cement inaisha huku unashangaa.

Ghorofa bwana kama sio la biashara ni waste of resources na ni majivuno ya kibinadamu tuu ambayo yote ni ubatili
Kweli kabisa.mi naona hiden roof ukipata yenye mchoro mzuri ni bora zaidi kuliko ghorofa.
 
Hapo saving ipo kwenye eneo la bure tu hapo juu. Kwingine haufanyi saving yoyote,mfano jamvi la kati gharama zake zinazidi masingi na kupaua nyumba ya kawaida pamoja na ceilling.piga hesabu kuanzia gharama zote za selemala na fundi wa chuma (nondo).
Nitakuja kujibu mkuu. Maana hapa tunaeleweshana tu
 
Aliyekwambia upost nyumba yangu bila kunitaalifu ni nani ??, [emoji23][emoji23]
 
Mkuu kujenga gorofa kwa sasa inaweza kuwa cheap kuliko kujenga nyumba flat yenye ukubwa sawa.

Mfano unapojenga gorofa ile cost ya mabati, mbao, sealing board zinakuwa hazipo katika fllat ya kwanza na hii cost inaweza kuwa ni chini ya ile cost ya kupiga jamvi, slubs na finishing yake
 
Back
Top Bottom