Ni kwanini walimu wanadharaulika sana mitaani?

Taifa lolote linalopuuza walimu ni taifa la watu wajinga. Mleta mada ni mjinga asiyejua hata kuandika. Someni vizuri uandishi wake mtangundua hana lolote.
Tupo hapa kama taifa sababu ya aina ya walimu tulionao.
Tunataka wstu wakabadilikie vyuoni na kuwa na IQ kubwa wakati tokea primary, secondary walikutana na walimu vilaza.
Leo hii hatuna uthubutu wowote wa Teknolojia sababu ya msingi mbovu.

Kosa kubwa sana lililofanywa na serikali ni kukubali watu wanaofeli kwenda kuwa walimu(hili hata mama Samia alisema kule Zanzibar)
 
Mimi lawama nzangu nazipeleka kwa Serikali, kwanini waruhusu walio feli au walio patata alama ndogo ndiyo wawe walimu ? Hii hata akili tu ya kawaida inakataa.

Kingine, hili jambo ni Serikali tu waamue kupindua meza, waweke mishahara minono kwa Walimu na alama ziwe juu ili mtu awe mwalimu, ila sasa nawaza tatizo kwenye ualimu hakuna dili za kupiga hela ndefu, hapa sasa ndiyo kuna shida.
 
Safi sana chukua Pepsi kwa mangi
 
Ni kweli kabisa na wengi wanakuwa vilaza kwasababu tunafundishwa na vilaza
 
Ni kwa sababu wao pia wanajidharaulisha mtaani.

Sasa unakuta mwalimu anadaiwa vitumbua vya elfu moja na mama ntilie miezi miwili bila kulipa
 
Ni kwa sababu wao pia wanajidharaulisha mtaani.

Sasa unakuta mwalimu anadaiwa vitumbua vya elfu moja na mama ntilie miezi miwili bila kulipa
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
 
Asichokijua kuna mpaka namba ya simu iliyotumika baina yake na mtu mwingine, Sasa anataka tufanye jambo tule ban ila mtakaobaki mtamjua huyo mlemavu wa akili. Bahat yake sheria haziruhusu ila leo angejutia hii mada yake.
Yaani dogo basi tu amezingua sana
 
Mimi ninavyojuwa
1.Muonekano- hili linatokana na mtu binafsi anavyojiweka lakini ninavyojuwa mimi hakuna mtu anayependa kuvaa na kuchomekea kama walimu

2.Madeni- hili linahusu maisha binafsi ya mtu na linasababishwa na kmtu kuwa na matumizi makubwa kuliko kipato chake

3.Kudharauliwa -hili linategemea na namna yeye mwenyewe anavyojiweka na anavyojichukulia yeye, kuna walimu wanaoheshimika na wanao dharaulika hata watu wenye kada tofauti wapo wanaodharaulika, utofauti ni pale mwalimu anapofanya kosa yeye huangaliwa tofauti sana na jamii inayo mzunguka kuliko mtu wa kada zingine.

4.Walimu ni watu waliofeli- hili siyo kweli kwani ukiangalia ufaulu wa walimu hususani kidato cha nne ni mkubwa kuliko D-4 zilizopo kada zingine ila sema watumishi wenzake wanamdharau mwalimu kulingana na mshahara wake kuwa mdogo


Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…