Ni kwanini walimu wanadharaulika sana mitaani?

Hakuna mtu aliyefeli anaweza kusomea ualimu.

Ualimu na afya ni kozi zinazozingatia sana ufaulu. Mtu mwenye sifa za kusoma ualimu basi ana sifa za kusoma taaluma yoyote.
 
nina brother wangu Moshi ni mwalimu...ana gari na nyumba nzuri sana na biashara zake ndogondogo
ukikutana nae jumamosi sabato unaweza dhani yeye ni mkuu wa wilaya maana ananyuka sana kaunda kali...
all in all uwe unafanya kazi yoyote ile jiongeze kwa mambo mengine utaishi vzuri .....usisikilize maneno ya watu kwamba kazi fulani ni za kimaskini hazina hela
 
Sababu wanahudumia watoto na Hawana mianya ya rushwa
 
Hawajatambua nguvu waliyo nayo ambayo ingeweza kuipaisha jamii na wao wenyewe wakapaa pia.

Ni kweli hawajitambui.
 
waalimu wanadharauliwa kwasababu wanapewa kipato kidogo cha mshahara. serikali kama za scandinavian hata marekani waalimu wana pesa nzuri sana na hii inawapa hamasa kufundisha mtoto kwa moyo. hawa wanachapa sana watoto na hawafundishi kwa moyo kwasababu ya kipato kidogo wanapewa, wanafundisha wakiwa na mawazo ya madeni, mwalimu anakopa mshahara wote kwa mangi kabla hata mwezi haujaisha na ukiisha tu nikuchukua mshahara na kulipa madeni. nikisema toka moyoni, hawa watu ni wa kuwaongezea mshahara uwe mkubwa sana. wanaofuata ni madaktari. period.
 
Hili kundi la walimu lina changamoto kubwa sana, nyingi zinafedhehesha. Walimu wengi wanakufa kwa Kisukari na pressure baada tu ya kustaafu sazingine anatembea njiani na kuongea peke ake

Nadhani kwasababu ya maisha duni waliyonayo na hofu ya kuwa jobless kwamba Sasa pesa atapata wapi kwasababu hawana maarifa ya kufanya biashara

Wengi wao ikiingia pension tu hata mwez haufiki ishateketezwa yoote, anagawia watoto million Tano Tano wanaenda mjini kuzitafuna zote mwisho watoto na baba wanakuwa vichaa wa kuomba omba

Mbaya zaidi nyumba wanajenga kwa pesa ya kustaafu, huwa ujenzi hauishi wanaungaunga za tope imeisha hiyoo
 
Walichowahi kukufanyia walimu kitakuathiri miaka yako yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…