huwa nawakubali sana watu wanaopenda kujua ukweli.. ipo hivi, mungu alifahamu kabisa ukoloni na mambo ya kitumwa, IN FACT, yeye ndiye muanzilishi wa utumwa na ukoloni..
AGANO AMBALO MUNGU ALIWEKEANA NA IBRAHIMU:
MWANZO 17:3-5
Ibrahimu angewezaje kuwa baba wa mataifa mengi bila kuvamia na kufanya makoloni katika hayo mataifa?
MWANZO 17:8
unaona kabisa Ibrahimu alikua sio mzaliwa wa kanaani, alikua ni mgeni pale, ila mungu akamuahidi atapindua utawala wa kanaani na kufanya kuwa milki ya milele ya Ibrahamu, na mungu wa Ibrahimu atakua mungu wa watu wa kanaani.. story hii inafanana kabisa na uvamizi wa wazungu katika nchi za afrika, na mungu wao amekuwa mungu wetu..
MWANZO 17:13
unaona kabisa hapa mungu anaongelea swala la kununua watu, yani biashara ya utumwa, mungu anamwelekeza Ibrahimu kuwa hata hao watu atakaowanunua kama watumwa lazima watahiriwe. SISI TUNAKAA HAPA TUNASEMA MZUNGU ATAKUJA KUHUKUMIWA SIKU YA MWISHO KWA KUTUFANYA WATUMWA, WAKATI MUNGU ALIWARUHUSU KABISA WAFANYE HIVYO..
KWA HIO MZUNGU MPAKA KUJA KUVAMIA BARA LA AFRIKA NI KAMA ALIPEWA MWONGOZO NA MUNGU WAO AFANYE HIVYO..
ukweli unauma ila vumilia tu.