That's more than a super monster!!
Sayansi:
Sayansi ya leo imethibitisha kuwa Mtu wa kwanza (Adam) alikuwa na kimo cha dhiraa 60. Soma nukuu zifuatazo katika Sehemu moja ya Toleo la Septemba 2001 la Jarida Mashuhuri la Sayansi la Israil, Ha-Mada Ha-Yisraeli B’ Angleet V’lvreet.” Kisha soma maoni chini yake.
Tel Aviv, Israil
Katika Kongamano la hivi karibuni nchini Israil lililozungumzia sayansi na dini, Dkt. Shlomi Lesser wa Chuo Kikuu cha Hebrew, na Mwenyekiti wa Taasisi ya Hofesh V’ Mada, akiwakilisha wanasayansi wenye shaka na dini, aliongoza mdahalo mkali baina ya wanabaiolojia na Wanazuoni wa ki-Orthodox wa Kiyahudi juu ya mada “Mwanzo wa Maisha”.
Wengi walioshuhudia mdahalo huo wakiwemo wale wenye msimamo mkali wa kidini, wakaibuka na hisia kuwa wanazuoni wa Kiyahudi hawakufanya vizuri dhidi ya wapinzani wao wa mrengo wa “Epicurean”.
Mwangaza wa mchana ulichomoza pale Dkt Lesser aliposhiriki katika kuulizana maswali; moja baada ya jingine na Rabbi Dovid Brown wa Chuo Kikuu cha Yeshiva.
Katika nukta moja, Dkt. Brown alimuuliza Rabbi Brown, je, mtu wa kwanza alikuwa na kimo gani? Mwanazuoni wa Kiyahudi akajibu, “aghalabu alikuwa na kimo cha mwanadamu wa wastani kwa mujibu wa Wahenga wa Kiyahudi (chazal)
Dkt. Lesser, akirejea utafiti ulioshirikisha taasisi yake na taasisi nyingine, akasema, “njia pekee ya mwanadamu kuweza kuja kutokana na jozi moja ya wazazi (wazazi wawili-Adam na Hawa) ni iwapo tu kama wazazi hao wa mwanzo walikuwa ni majitu makubwa katika zama za kabla ya elimu ya lishe.”
Hesabu zake zilionesha kuwa ili jamii ya mwanadamu kuweza kufikia hali ya maumbile waliyokuwa nayo katika karne ya 17, Kisa cha Adam na Hawa kingelikuwa na maana iwapo tu mtu wa kwanza angelikuwa na kimo cha futi 90.
Hakuna njia nyingine ambayo mwanadamu angeliweza kuvuka kikwazo cha kijenetikia.” Aidha, Dkt. Lesser anasema, kama Adam angelikuwa na kimo cha mtu mwingine yoyote yule kama wanavyosema wanazuoni wa dini ya Kiyahudi, basi hii ingekifanya kisa cha Adam na Hawa kuwa upuuzi ulio dhahiri.”
Ni jambo la kuvutia kwamba wakati wanabaiolojia hao wakidhani kuwa wanaipondaponda dini ya Kiyahudi kumbe wanauthibitisha Uislamu! Wanasayansi waliibuka na utafiti wa kijenetikia ambao uliwapelekea kufanya hesabu za kimo ambacho mtu wa kwanza angekuwa nacho kama Kisa (cha Adam na Hawa) kilikuwa cha kweli.
Wakaibuka na futi 90. Zingatia kuwa miaka 1400 iliyopita kabla ya wasomi hawa hawajafikia hitimisho hilo, Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, alishazungumzia kitu hicho. Kimahesabu, dhiraa sitini ni sawa na Futi 90.