Ni kweli Adam na Hawa waliishi miaka takribani 900?

Ni kweli Adam na Hawa waliishi miaka takribani 900?

Watu huwa tunasoma biblia juu juu...hatuielewii....ukitoka hapo na wewe unajikuta upo deep kwa kusoma kifungu kimoja...ukitaka kuielewa soma yotee.
 
Mtu kuishi miaka 100 tu ni mziki lakini Biblia inasema Adam na Hawa waliishi miaka 900.

Je, hao walioandika Adam na Hawa waliishi miaka 900 walitumia kipimo gani?
Sijaona uongo wa biblia labda wewe ndio muongo, Bibi yangu amefariki juzi juzi tu akiwa na miaka 90 lakini mimi nikijitazama naona kama life span imepungua maana sioni dalili za kufika miaka 90, lakini embu jiulize sasa hivi wewe una umri gani? je utaweza kufikisha umri mhe.Mugabe? jinsi siku zinavyokwenda mbele life span ya binadamu inazidi kupungua, muangalie Rooney mchezaji wa Manchester United anamiaka 31 na anaonekana ni mtu umri umeshakwenda tayari je akifikisha miaka 60 si atakuwa mzee sana, embu fananisha umri wa Rooney na Roger Mila wa cameroon wakati akiwa na miaka 30 ya Rooney alionekana bado kijana sana lakini leo hii Rooney anaonekana mzee kiasi kwamba watu wengine wanamshauri asicheze tena Timu ya Taifa ajikite kwenye kilabu chake tu, jinsi tunavyozidi kuishi umri unazidi kupungua.
 
UrbanGentleman ngoja nikupe ushauri wa bure....dini yeyote duniani huwa zina beyond human thinking powers. ...sio vitu vya mchezo. ..Kuna mtu aliamua kuichana BIBLIA hadharani, mikosi iliyo mjia sintoweza kukuadisia. ....wewe waache watu na imani zao nawe ufanye unalolitaka. ..I believe in KARMA, so watch out! Don't termpt anyone's faith. ..I wish you good morning
Katika hilo nakubishia,kwani kuna mtu namfahamu alikuwa anachana Biblia na kuvutia tumbaku,tulipomuuliza kulikoni anafanya vile ilihali kile ni kitabu kitakatifu cha wakristo?akasema afadhali yeye anavutia tumbaku kwani enzi zake alipokua baharia aliwahi kuwekwa jela huko ulaya na walipokua jela walikua wanachana biblia walizokua wakipewa wajisomee mle ndani na kuvutia unga na wengine bangi,huyo jamaa sasa yupo singida anafanya biashara ya kuku na yupo poa kabisa.
 
Uongo mwingine huu..

MWANZO 6:3

BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa MIAKA MIA NA ISHIRINI.

MWANZO 7:6

Naye Nuhu alikuwa mtu wa MIAKA MIA SITA hapo hiyo gharika ya maji ilipokuwa juu ya nchi.

* * * * * * * *

huyu mwandishi inaelekea alikua na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu.. alishaandika mungu amelimit umri wa binadamu uwe miaka ishirini tu.. baadae anakwambia Nuhu aliishi miaka mia sita..

Hatari sana.
Mzee kuna kikongwe kaishi miaka 138 au mungu ajamuona
 
sijakana uwepo wa mungu, ila uwepo wa mungu huyu wa kikristo, there's no way you can tell me wazee wangu na mababu wote wa kiafrika waliofariki kabla ya kuja kwa ukristo wapo motoni kisa hawakumjua yesu alieletwa na mkoloni.

Wala hao babu zako unaowasema hawako motoni maana siku ya hukumu haijafika bado.ila kwa kukusaidia uelewa kidogo no kwamba, kipindi hicho cha mababu walikuwa chini ya sheria hivyo watahukumiwa kulingana na matendo Yao maana utambuzi wa mema na mabaya ulikuwa ndani ya mioyo Yao.hata Kama hawakumjua Mungu lakin sasa hatuko chini ya sheria tena Bali chini ya Imani katika Kristo. Yesu ndio agano la mwisho kuelekea hukumu hakutakuwa na agano jingine tena Bali hukumu atakaporudi kwa Mara nyingine.
 
Binafsi nilipata kusoma biblia kwa undani kipindi nipo shule( seminary) siku moja nliuliza hilo swali pia, majibu niliyoyapata ni haya....biblia inaandika vile sio kweli mtu aliishi miaka mfano 900 ila hiyo miaka mia 9 inaonesha ukamilifu kwa jambo fulani, na ndio maana tunapoambiwa mfano: yesu akija wataokolewa watu 14440 hiyo ni hesabu ya waisrael ikiwa na maana sana, hivyo hivyo katika hiyo miaka ina onesha ukamilifu wa jambo fulani na sio kweli kwamba ni miaka 900 ya kuishi.....tuisome biblia na kuelewa maana ya namba zilizomo na maneno yako.
 
Katika hilo nakubishia,kwani kuna mtu namfahamu alikuwa anachana Biblia na kuvutia tumbaku,tulipomuuliza kulikoni anafanya vile ilihali kile ni kitabu kitakatifu cha wakristo?akasema afadhali yeye anavutia tumbaku kwani enzi zake alipokua baharia aliwahi kuwekwa jela huko ulaya na walipokua jela walikua wanachana biblia walizokua wakipewa wajisomee mle ndani na kuvutia unga na wengine bangi,huyo jamaa sasa yupo singida anafanya biashara ya kuku na yupo poa kabisa.
Hao watu wote uliyo nitajia wako katika hali gani? Na huyo MUUZA KUKU. .duh! Naona tuko anga ya tofauti. ..NAKUOMBA UNISAMEHE SANA KWA KUJARIBU KUKUELEWESHA....uwe na siku njema. .Bye-bye
 
Binafsi nilipata kusoma biblia kwa undani kipindi nipo shule( seminary) siku moja nliuliza hilo swali pia, majibu niliyoyapata ni haya....biblia inaandika vile sio kweli mtu aliishi miaka mfano 900 ila hiyo miaka mia 9 inaonesha ukamilifu kwa jambo fulani, na ndio maana tunapoambiwa mfano: yesu akija wataokolewa watu 14440 hiyo ni hesabu ya waisrael ikiwa na maana sana, hivyo hivyo katika hiyo miaka ina onesha ukamilifu wa jambo fulani na sio kweli kwamba ni miaka 900 ya kuishi.....tuisome biblia na kuelewa maana ya namba zilizomo na maneno yako.
14440 = 13 number ya kugeuza. Kuanza upya. ..
 
utambuzi wa mema na mabaya ulikuwa ndani ya mioyo Yao.
huko kwingine kote umeongea pumba kasoro hapo tu.. kumbe tumezaliwa na utambuzi wa mema na mabaya.. kwa maaana hio ukiishi katika misingi hio ya utambuzi huwezi kupotea, so yesu hana umuhimu hapo..

na kumbuka pale msalabani yesu alimwambia yule mwizi leo hii utakuwa nami peponi, sasa hio hukumu mbona haikusubiri mpaka yeye arudi? au alimfanyia feva kishkaji?

na hata hivyo yesu mwenyewe wanasema hakwenda peponi alienda kuzimu kwanza kumpora shetani funguo, sasa huyu mwizi alipelekwa na nani peponi angali yesu alienda kuzimu kwanza? au yesu alipaa nae hadi peponi akamdrop halafu akamwambia nakuja baada ya dakika sifuri??

na kama alimpora shetani funguo za mamlaka, mbona effects / matokeo ya shetani kuporwa funguo hayaonekani?? ni kama maovu yamezidi kile kipindi shetani alipokuwa nazo hizo funguo.

tafakari mkuu, hata wakati unaanza kufundishwa hesabu za kugawanya uliambiwa tatu gawa kwa mbili ni moja inabaki moja, na hauwezi kugawanya tena, na ukakubali.. ila kadri ulipozidi kuongeza darasa ukafundishwa uwezekano wa kugawanya tena na unapata desimali..

Usikubali kubaki kwenye ufahamu wa TATU GAWA KWA MBILI NI MOJA INABAKI MOJA.. Kuna desimali mkuu.
 
Uongo mwingine huu..

MWANZO 6:3

BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa MIAKA MIA NA ISHIRINI.

MWANZO 7:6

Naye Nuhu alikuwa mtu wa MIAKA MIA SITA hapo hiyo gharika ya maji ilipokuwa juu ya nchi.

* * * * * * * *

huyu mwandishi inaelekea alikua na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu.. alishaandika mungu amelimit umri wa binadamu uwe miaka ishirini tu.. baadae anakwambia Nuhu aliishi miaka mia sita..

Hatari sana.
Kwa ninavo elew japo nikidog
Haya maandik yameandikwa baada ya hayo matukio kutokea....
Iyo miaka 120 aliyo pewa mwanadam ni baada ya mwanadam ku muhuz Mungu ,hii inamaanisha walio ishi hawal walihish kwa muda mrefu zaid ...
Kumbuka!!
Maandiko yameandikwa baada ya matukio kutokea c wakati matukio yanatokea
 
wakristo bwana, when it comes to proving the truth about some biblical scriptures, science is very applicable, IN SCIENCE WE TRUST. ila kwenye mambo mengine science is demonic, because they dont believe in the existence of God!!!??

WHY WOULD YOU USE AND TRUST THE KNOWLEDGE OF SOMEONE WHO DOESNT BELIEVE IN GOD TO PROVE THE EXISTENCE OF SOMETHING CONCERNING YOUR BELIEF?

kweli baniani mbaya kiatu chake dawa.
Hapo ni sawa na waislamu wakati wanakuja na mabandiko yao kuikashifu Biblia.. baada ya muda utawaona wakiitumia hiyo hiyo biblia kusema imemtabiri mwamadi wao na al lah wao.
 
Mtu kuishi miaka 100 tu ni mziki lakini Biblia inasema Adam na Hawa waliishi miaka 900.

Je, hao walioandika Adam na Hawa waliishi miaka 900 walitumia kipimo gani?
uwezo wako wa kufikiri umegota hapo. pole sana
 
Kwa ninavo elew japo nikidog
Haya maandik yameandikwa baada ya hayo matukio kutokea....
Iyo miaka 120 aliyo pewa mwanadam ni baada ya mwanadam ku muhuz Mungu ,hii inamaanisha walio ishi hawal walihish kwa muda mrefu zaid ...
Kumbuka!!
Maandiko yameandikwa baada ya matukio kutokea c wakati matukio yanatokea
uongo WA Hali y'all juu
 
UrbanGentleman ngoja nikupe ushauri wa bure....dini yeyote duniani huwa zina beyond human thinking powers. ...sio vitu vya mchezo. ..Kuna mtu aliamua kuichana BIBLIA hadharani, mikosi iliyo mjia sintoweza kukuadisia. ....wewe waache watu na imani zao nawe ufanye unalolitaka. ..I believe in KARMA, so watch out! Don't termpt anyone's faith. ..I wish you good morning
Wewe acha story Zach chai mbna vitu vidogo na nini vyepesi haviitaji nguvu sana kuvielewa kua ni uzandiki wa wazungu
 
Kwa ninavo elew japo nikidog
Haya maandik yameandikwa baada ya hayo matukio kutokea....
Iyo miaka 120 aliyo pewa mwanadam ni baada ya mwanadam ku muhuz Mungu ,hii inamaanisha walio ishi hawal walihish kwa muda mrefu zaid ...
Kumbuka!!
Maandiko yameandikwa baada ya matukio kutokea c wakati matukio yanatokea

naona umestick kwa noah tu, ambayo ni hadithi, na ushahidi huna.. ila kwenye reality nimetaja watu wawili ambao wameishi miaka zaidi ya 120, na kuna memba ameongeza watatu anaemfahamu ameishi miaka 138.. unasemaje kuhusu hilo?
 
Back
Top Bottom