Hakuna Uthibitisho wa Moja Kwa Moja kuhusu Ulaji wa Vyakula hivi kuwa unapelekea upotevu wa Nguvu za Kiume Endapo vitatengenezwa katika Utaratibu mzuri kuzingatia maadili ya Kiafya.
Maandalizi ya Chakula Hiki hasa Kwa jamii za Kitanzania ndio unapelekea Matatzo ya Nguvu za Kiume kutokea Mfano.
Jamii nyingi zinapika chips Kwa kutumia Mafuta Mengi na kama inavyojulikana Chips hunyonya Mafuta mengi sana, na mbaya zaidi Mafuta haya ni Yale yanayoganda Mfano Korie na mengineyo ambayo husababisha (cholesterol) au Mgando wa Mafuta Mwilini na Kusababisha Damu kuto tembea vizuri. Na tunajua Bila Damu Mashine haiwez kufanya kazi.
Sababu nyingine inayoweza kujitokeza ni kama Mtu tayari ana Ugonjwa wa Kisukari, Viazi kiasili vina virutubisho vingi vya Wanga (Carbohydrates) Kwa hiyo vinatakiwa kuliwa kwa Wastani, Kwa namna hiyo Basi inaweza kupekeka kusababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume.