Ni kweli chipsi mayai inaua nguvu za kiume?

Ni kweli chipsi mayai inaua nguvu za kiume?

Poker

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Posts
5,445
Reaction score
14,828
Habari wanajamii na kheri ya Eid El fitr! Naona kumekuwa na propaganda ati kwamba kwa wanaume kula kiepe kunaua nguvu za kiume ila wataalamu yaani madaktari wanakataa!

Vp wadau wa kiepe mumewahi experience erectile dysfunction kwa kula zege!

N.B walianza kutuambia Chinese mboga inaua nguvu za kiume, wakaja na energy drinks, wakaja na kuku za kisasa na mayai ya kisasa sasa wameingia kwenye kiepe. Na bado tunaambiwa tukitumia Viagra tutakufa kibudu! Tuamini kipi, tushike kipi na tuache kipi?

Screenshot_20220503-183554.jpg
 
Tatizo ni mayai ya kisasa na maguta wanayo tumia kukaangia yana kuwa yasha haribika sana
 
Ngoja nikakaange sasa hivi.

ILa ya mtaani ndo huwa tamu zaidi kuliko homemade
 
Mzee kama wewe ni mwanaume kiepe kula kwa hamu tu lakini isiwe katika list ya vyakula vyako.
 
Hakuna Uthibitisho wa Moja Kwa Moja kuhusu Ulaji wa Vyakula hivi kuwa unapelekea upotevu wa Nguvu za Kiume Endapo vitatengenezwa katika Utaratibu mzuri kuzingatia maadili ya Kiafya.

Maandalizi ya Chakula Hiki hasa Kwa jamii za Kitanzania ndio unapelekea Matatzo ya Nguvu za Kiume kutokea Mfano.

Jamii nyingi zinapika chips Kwa kutumia Mafuta Mengi na kama inavyojulikana Chips hunyonya Mafuta mengi sana, na mbaya zaidi Mafuta haya ni Yale yanayoganda Mfano Korie na mengineyo ambayo husababisha (cholesterol) au Mgando wa Mafuta Mwilini na Kusababisha Damu kuto tembea vizuri. Na tunajua Bila Damu Mashine haiwez kufanya kazi.

Sababu nyingine inayoweza kujitokeza ni kama Mtu tayari ana Ugonjwa wa Kisukari, Viazi kiasili vina virutubisho vingi vya Wanga (Carbohydrates) Kwa hiyo vinatakiwa kuliwa kwa Wastani, Kwa namna hiyo Basi inaweza kupekeka kusababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume.
 
Kula hata usiongope..ila ogopa sana processed food and drinks.

#MaendeleoHayanaChama
 
Habari wanajamii na kheri ya Eid El fitr! Naona kumekuwa na propaganda ati kwamba kwa wanaume kula kiepe kunaua nguvu za kiume ila wataalamu yaani madaktari wanakataa! Vp wadau wa kiepe mumewahi experience erectile dysfunction kwa kula zege!View attachment 2210118View attachment 2210121

View attachment 2210119

View attachment 2210120
Ni kweli kinaua nguvu za kiume kabisa, 💯 . Accumulation ya mafuta kwenye mishipa inasababisha msukumo wa damu kuwa kidogo, hivyo nguvu za kusimamisha zinakuwa ndogo sana. Wengi unenepeana kwa Sababu ya mafuta , pressure, kisukari etc. Angalia yale matoto ya kule masaki, upanga, mikocheni mingi ni mine mine sababu wazazi wao uwalisha kiepe kwa wingi, wengi utakuta Wana pressure na kisukari, tipwatipwa halinq nguvu.
 
Back
Top Bottom