Ni kweli filamu ya Ottoman inaoneshwa Azam tv ili kuudhalilisha ukristo?

Ni kweli filamu ya Ottoman inaoneshwa Azam tv ili kuudhalilisha ukristo?

Kwani kuna namna wanakuwa affected na hiyo filamu? Mimi sio muislamu na napenda kufatilia muvi za aina hiyo na sio kwa lengo la kuona naonewa au vipi! Nahisi negativity imetutawala sana!
Nimeipenda hii
 
Sasa wanadhalilishaje ukristu? Ile ni history ya kweli ambayo ilishatokea huko
Yani kuna watu wanajua kujidhalilisha🤣 tunaoneka vituko huko kwa wenzetu unajua eeh😅
 
Sio mfuatiliaji wa hiyo tamthilia, lakini kama ujumbe unaooneshwa kwenye hiyo tamthilia basi sio mzuri kisaikolojia.

Hao Azam Tv naamini kabisa wansupenda huo ujumbe ndio maana wanaacha uendelee kuoneshwa kwenye television yao.

Vipi kama hiyo tamthilia ingekuwa na ujumbe wa tofauti, unaoonesha wakristu wakiwapiga waislamu, hao Azam Tv wangeonesha hiyo tamthilia?

Naamini wasingeonesha, kwasababu wanajua hawataki kuifanya dini yao ionekane nyonge dhidi ya dini nyingine.

Sasa kama hawataki kuishusha dini yao, kwanini wanaishusha ya wengine? Vipi ikitokea television station nyingine ikaonesha maudhui ya waislamu wakipigwa na wakristu? Najua watakavyo pagawa.

Azam Tv wanafanya huo ujinga kwasababu wanajua yupo mama yao atawalinda, wanajiona wako salama sana mpaka kuingilia hisia za wengine, na kutojali maumivu wanayowasababishia kisaikolojia.

TCRA wako wapi? Hawauoni huo ujinga wa Azam Tv, au nao ndio wanaogopa kuwashughulikia kwasababu nao wanamuogopa "mama yao" Azam Tv?

Kama wahusika wameamua kulifumbia macho hilo suala, bado uamuzi wa mwisho upo kwa watumiaji wa Azam, waachane na kununua vin'gamuzi vya Azam, watafute wengine wanaojali hisia za watumiaji wa vin'gamuzi vyao.
Ebu jaribu kuficha huu ujinga wako hata kidogo,unaweza kuibadilisha historia? Kwahiyo wasionyeshe kisa wewe mgalatia utachukia?

Labda kama wengi wenu ni wadogo humu,miaka ya wakati huo ipo ITV tu,walikuwa wanaonyesha filamu za kinigeria huko ni kanisa na kukemea kwa jina la Yesu,mbona watu hatuku mind?

Acheni ujinga,kama hutaki kuangalia,acha na angalia mambo mengine,huwezi ukafurahishwa na kila kitu hapa duniani
 
Mleta mada umeona kitu kizuri...

Uturuki bado ina ndoto ya Dola ya Ottoman.

Nchini Uturuki kuna makundi ya Kisiasa ya Aina mbili Akina Edorgan wanaotaka kuona Uturuki inakuwa na influence kama Ottoman na kuna kundi lingine ni secular hawataki tabia ya Edorgan na kundi lake...
Sasa hizi tamthilia ya Uturuki unazoziona zinatumika kupush agenda ya Ottoman.

Uturuki imefanikiwa kuukamata utawala wa Syria, Somalia sasa wanataka kwenda nchi zingine
 
Mwambie huyo jamaa aende google akasearch kitu kimoja kinaitwa "Motivated Reasoning".
Atapata majibu ya hilo swali.
 
Kuna mengi sana ya kufanya katika haya maisha, ila ukishaanza kuona akili yako inawaza sijui dini flan ina mpango flan jua kuna shida sehem..........
 
Mdau ametufata inbox na kutoa dukuduku lake kama ifuatavyo:-
"Tamthilia ya Kituruki Ottoman, ambayo inaoneshwa kupitia Az@m Media, imekuwa gumzo kubwa miongoni mwa watazamaji wengi nchini Tanzania.
Licha ya kuvutia kwa hadithi yake ya kihistoria, baadhi ya watu wameanza kuhoji maudhui yake na ujumbe unaopitishwa.

Katika tamthilia hiyo, inaonekana wazi kuwa kuna mapambano kati ya Waislamu wakiongozwa na Othman na Wakristo wanaowakilishwa kama Waroma. Mapigano haya yanaoneshwa kuwa ni kwa ajili ya kusimika dini ya Uislamu, na katika kila pambano, upande wa Waislamu huonekana kushinda.

Wakati wa ushindi, mara nyingi husikika kauli kama “Allahu Akbar,” huku upande unaoshindwa ukiwasilishwa kwa alama za Kikristo kama misalaba na mavazi yenye maandishi ya Roma. Hali hii imeibua tafsiri kwa baadhi ya watazamaji kuwa kuna ujumbe unaolenga kuonyesha ubora wa dini moja dhidi ya nyingine.

Mbali na hilo, kumekuwa na maswali kuhusu tafsiri ya tamthilia mbalimbali zinazooneshwa. Watazamaji wengine wanasema kuwa hata filamu ambazo si za Kiislamu, tafsiri zake huingiza maneno kama “Assalamu Aleikum” au “Allah,” jambo ambalo linaongeza hisia za mwelekeo wa kidini kwenye maudhui yasiyokuwa ya asili hiyo.

Kutokana na hali hii, baadhi ya watu wangu tunajiuliza:

Je, huu ni mkakati wa makusudi wa kuingiza propaganda ya kidini kupitia burudani?

Aidha, hoja nyingine inayojitokeza ni kuhusu uwiano katika nafasi za kazi ndani ya vyombo vya habari, ambapo tunahisi kuna upendeleo wa kidini unaoweza kuonekana au kuhisiwa"
MDAU AKAMALIZA HIVYO

(MAONI YETU SISI KAMA @JAMIIDIARY)

Ni muhimu kutambua kuwa tamthilia kama Ottoman ni kazi ya kihistoria inayotokana na utamaduni na historia ya Uturuki, ambapo Uislamu ulikuwa sehemu kubwa ya dola hiyo. Hivyo, baadhi ya maudhui yanaweza kuwa yanaakisi historia badala ya kudhani ni kampeni ya moja kwa moja ya kidini.

Kuhusu swala la uwiano wa kazi/ajira kwa kigezo cha dini sio swala la kujadili kwa kuwa tunaamini medias wanaajiri watu kutokana na CV au weledi.

USHAURI: Ni jukumu la vyombo vya habari kuhakikisha maudhui yanatolewa kwa uwiano, lakini pia watazamaji wanapaswa kuwa makini katika kutafsiri kile wanachokiona.
Sidhani kama watu wanadhani hivyo maana kwenye historia ya dunia ilishatikeq hiyo vita sioni kama kuna jipya labda kama huelewi
 
Kwani kuna namna wanakuwa affected na hiyo filamu? Mimi sio muislamu na napenda kufatilia muvi za aina hiyo na sio kwa lengo la kuona naonewa au vipi! Nahisi negativity imetutawala sana!
Usijiwazie wewe, wawazie watoto Wadogo katika Uislamu, na namna vile wanavyopandikiziwa mentality ya Doing for ALLAH, whatever is Fine.
Kuna jambo haliko sawa hakika.
 
Hilo nililiina sikunyingi nikapiga marufuku watoto wabgu kuangalia hizo tamthilia..
Sina lengo kuu za kuupa nguvu uislamu
 
Hilo nililiina sikunyingi nikapiga marufuku watoto wabgu kuangalia hizo tamthilia..
Sina lengo kuu za kuupa nguvu uislamu

Na movies za kina kanumba na za kinigeria za kuhamasisha ulokole vipi? Movies zinazowa portray Waislam kama magaidi tena kwa uzushi na stereotypes mbaya kabisa vipi?
 
Baba yako amewahi kumiliki hata Tv ukiachilia mbali amewahi kumiliki akili?
Hili jibu lina ondoa maana nzima ya mada uliyoleta.Fkr a moment nilidhani ume andika ili ku balance taarifa lakini kumbe una upande tayari.Malalamiko kuhusu azam yamekuwepo almost miaka 4 au 5 hivi na wanajua,kwa mara ya kwanza mwaka jana msimu wa krismasi waliweka matangazo ya krismasi hata hili la ottoman lina julikana ni bahati mbaya wateja wa azam wengi ni vichwa maji hawaelewi lakini kwa anae jua la ottoman kuwa na mlengo wa kudhalilisha au kupinga ukristo liko wazi.
 
Siku moja watu mtakuja kushukuru kazi kubwa anayofanya Netanyahu.

Netanyahu hatoshinda. Hatoweza kuushinda Uislam. Licha ya genocide anayo commit kule Palestine na Lebanon, hatofanikiwa kamwe kuushinda Uislam.

Halafu ulikuwa mstari wa mbele kujifanya "haki haki" kwenye jukwaa la siasa, kumbe chuki za kidini tu zinakusumbua.
 
Mdau ametufata inbox na kutoa dukuduku lake kama ifuatavyo:-
"Tamthilia ya Kituruki Ottoman, ambayo inaoneshwa kupitia Az@m Media, imekuwa gumzo kubwa miongoni mwa watazamaji wengi nchini Tanzania.
Licha ya kuvutia kwa hadithi yake ya kihistoria, baadhi ya watu wameanza kuhoji maudhui yake na ujumbe unaopitishwa.

Katika tamthilia hiyo, inaonekana wazi kuwa kuna mapambano kati ya Waislamu wakiongozwa na Othman na Wakristo wanaowakilishwa kama Waroma. Mapigano haya yanaoneshwa kuwa ni kwa ajili ya kusimika dini ya Uislamu, na katika kila pambano, upande wa Waislamu huonekana kushinda.

Wakati wa ushindi, mara nyingi husikika kauli kama “Allahu Akbar,” huku upande unaoshindwa ukiwasilishwa kwa alama za Kikristo kama misalaba na mavazi yenye maandishi ya Roma. Hali hii imeibua tafsiri kwa baadhi ya watazamaji kuwa kuna ujumbe unaolenga kuonyesha ubora wa dini moja dhidi ya nyingine.

Mbali na hilo, kumekuwa na maswali kuhusu tafsiri ya tamthilia mbalimbali zinazooneshwa. Watazamaji wengine wanasema kuwa hata filamu ambazo si za Kiislamu, tafsiri zake huingiza maneno kama “Assalamu Aleikum” au “Allah,” jambo ambalo linaongeza hisia za mwelekeo wa kidini kwenye maudhui yasiyokuwa ya asili hiyo.

Kutokana na hali hii, baadhi ya watu wangu tunajiuliza:

Je, huu ni mkakati wa makusudi wa kuingiza propaganda ya kidini kupitia burudani?

Aidha, hoja nyingine inayojitokeza ni kuhusu uwiano katika nafasi za kazi ndani ya vyombo vya habari, ambapo tunahisi kuna upendeleo wa kidini unaoweza kuonekana au kuhisiwa"
MDAU AKAMALIZA HIVYO

(MAONI YETU SISI KAMA @JAMIIDIARY)

Ni muhimu kutambua kuwa tamthilia kama Ottoman ni kazi ya kihistoria inayotokana na utamaduni na historia ya Uturuki, ambapo Uislamu ulikuwa sehemu kubwa ya dola hiyo. Hivyo, baadhi ya maudhui yanaweza kuwa yanaakisi historia badala ya kudhani ni kampeni ya moja kwa moja ya kidini.

Kuhusu swala la uwiano wa kazi/ajira kwa kigezo cha dini sio swala la kujadili kwa kuwa tunaamini medias wanaajiri watu kutokana na CV au weledi.

USHAURI: Ni jukumu la vyombo vya habari kuhakikisha maudhui yanatolewa kwa uwiano, lakini pia watazamaji wanapaswa kuwa makini katika kutafsiri kile wanachokiona.
Achana na udini,kaa kwenye mstari unaokufaa.
Turkey ni baina ya takataka zimeingizwa euro ila NATO wakamate magaidi wooite
 
Netanyahu hatoshinda. Hatoweza kuushinda Uislam. Licha ya genocide anayo commit kule Palestine na Lebanon, hatofanikiwa kamwe kuushinda Uislam.

Halafu ulikuwa mstari wa mbele kujifanya "haki haki" kwenye jukwaa la siasa, kumbe chuki za kidini tu zinakusumbua.
Bila Wayahudi kusingekuwa na Uislamu
 
Back
Top Bottom