Ni kweli kwamba private wa jeshi la Marekani ni bora kuliko Generali wa jeshi la Tanzania?

Tatizo JWTZ halizalishi ndio maana wanayafanya hayo,wabadilike wawe wanafanya pia na uzalishaji,maana kazi wanazofanya sio za jeshi kabisa,ma"KURUTI" ndio wanateseka sana kutwa kufyeka mapori tu.
Pole mkuu,labda hujui tu hakuna jeshi lenye ubunifu east na central Africa especially kwenye mambo ya uzalishaji na uwekezaji kama jwtz Ina miradi mikubwa tu inafanya na tena kwa kupitia kamandi yao ya jkt ,ujenzi Wa ukuta ,reli sgr ,miradi ya nyumba yote tenda wanazipata kupitia SUMA jkt
 
Kwenye uzalishaji Mimi naona Magereza wanafanya vizuri. JWTZ ni porojo tu.
JKT ni kamandi ya JWTZ?
 
hivi Tanzania kuna jeshi au kichekesho?
maluten wao kazi yao ni kushinda chini miembe wanapiga story za madem na pombe tu.bora hata police wa Tanzania kazi yao inaonekana
Asee.. Kwa hiyo pale monduli huwa wanaenda kuharibu tax zetu tu?
 
Jenereli wa Tz ni bora zaidi ya private wa US. inabidi kwanza ufaham jeshini private ni mwanajeshi wa aina gani na jenereli ni mwanajeshi wa aina gani.
pengine kimajukum jenereli ni sawa na kocha wa mpira wa miguu na private ni sawa na mchezaji.

Kwa hiyo hapo jenereli wa tz ni kama kocha Hemed Morroco au Mkwasa na private wa US army ni kama Cristiano Ronaldo , Mbape au Pogba. Hapo Mkwasa anaweza kumfundisha Rondaldo lakini hawez kucheza kama Ronaldo na Ronaldo pia hawezi kumfundisha mpira Mkwasa.

Tofaut ipo kubwa lakini kimajukum jeshini Jenerali wa bongo ni zaidi maradufu ya private wa US
 
Ukweli unabaki palepale huwezi ukamlinganisha mwanajeshi wa tz na mwanajeshi wa usa, usa watabaki kuwa juu! Askari wetu bado sana kwanza kuwalinganisha ni sawa namatusi,mwanafunzi hawezi kulinganishwa na mwalimu wake.
 
Lakini mkuu sisi tunavunja matofali kila mwaka[emoji16][emoji16] tunalalia misumari,tunavuta gari kwa shingo aseee General imara[emoji16][emoji16][emoji16]
We jamaa siku hizi hayo maguvu yamepitwa na wakati zilikuwa enzi za akina Samsoni sikuhizi ni science na technologies.
 
Jeshi letu linaandaliwa zaidi ktk utimamu wa mwili ila kiakili na tech ni zero kabixa,,,ndo maana unakuta wanatembea na kadi za ccm mfukoni,,hawajui maana halisi ya kuitwa jeshi la wananchi yaani wapo wapo tu,,wananchi hata wakandamizwe kiasi gani huwezi sikia linawatetea bali linakaa nyuma ya watawala kujadili jinsi ya kuwakabili wananchi,,,,,huwezi amini askari watu wana uelewa mdogo kuhusu elimu ya uraia na katiba ya nchi,,,uchumi wa marekani unajengwa na jeshi kupitia ugunguzi wa tech,operations mbali mbali nk lkn bongo jeshi ni parasite linanyonya tu. Wakati mwingine huwa nashangaa raisi kuwapa sifa zile labda kwa sababu hataki wamchukie lkn hawana tija linapokuja swala la kukuza uchumi wa nchi.
 
Wee ni askari mpumbavu kwahiyo unapingana na katiba inayotoa haki ya kuandamana?? Kwahiyo tuna jeshi ambalo linawasubari watu wanye kambini ili liwaadhibu,???? Nina uhakika 100% we ni askari jwtz maana wapo wengi vilaza huko wasiojua kwanini wapo huko!!! Ebu rudia comment yako uone ulivo zero kichwani,askari wa hivi ni janga kuu uelewa mdogo mno.Eti andamana uone!!!! Askari mwelevu hawezi kukandamiza haki za kiraia hata cku moja bali atamlinda aandamane kwa Amani na ujumbe ufike kwa walengwa.
 
I accept my Ignorance,
 
Hakuna jeshi lisilofanya mazoezi ya Utimamu ya mwili Duniani, Hivi hajaona askari wa marekani wakibeba mabegi makubwa mgongoni, bila mwili kuwa timamu watamudu.

Hata ukipigiana na kwa kutumia ndege, mwili wa mwanajeshi unahitaji kushinda maumivu,
Mwanajeshi akiugulia kila maaumivu ni shida.

Nadhani unakumbuka Kilichowakuta wamerekani waliojaribu, kushukuka kwenye ndege zao, Wakapigane na Wasomali.

Msomali hana buti lakini mwiba ukimchoma ni kama umechoma mguu wa Tembo, Wamerekani wakipigwa na joto la jua kali hoi.

Mazoezi ya mwili ni muhimu hayapitwi na wakati kinachobadilika ni vya kufanyia mazoezi tusidanganyane.
Dunia imeshahama huko kwenye maguvu ya enzi za kale!
 
Hebu Editi kwanza ili ueleweke duh, mbona kama umeandika una jazba,.
 
Alichoandika ni Uongo, haitatokea mpo mahala popote, watu mko wa wawili wa tatu.
Mpaka muongelee mambo ya mademu, siyo wanawake nieleweke mademu, basi lazima muwe mambo yenu ya mademu muwe mnafahamiana.

Hivyo hawezi tokea asiye husika, akajumuika ama anapita karibu yenu, alafu msimuliaji aendelee kusimulia.
Mkuu ulitaka wafanye nini je kilasiku unakuta wanapiga hizo stor au majukumu yao unayajua ?
 
Unadhani Wamerekani waendao Vitani, mwisho wa siku wanarudi kwao wakiwa wazima
Labda wenafanya zoezi tu.
Inawezekana ikawa kweli...

Na kwa nini tuwa deploye kwenye war zone kama siku zote ni amani tuu...

Wale wanaopelekwaga Somalia au comorro zinarudigi combat tuu...


Cc: mahondaw
 
Bora hata jeshi la Rwanda linaenda battle Congo kutafuta Madini n. k...... Linazalisha
 
Jeshini kuna;

1. Maserule.

2.Mananga,

3.Wadojaji wa fatiki za jeshi,

4.Maroporopo, mazobe

5.E.D za matron

huyo wa kijiweni kwenu muangalie kati ya hizo yuko fungu gani. then lete mrejesho.
 
sisi TPDF tulikwenda Anzuwani, Msumbji, zimbabwe,namibia,Lebanono, Sudani, somalia, Israel, RSA, Syria, Vietnam, hata ww ii. babu yangu alienda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…