Ni kweli kwamba Profesa Janabi hajawahi kusomea wala kuwa Daktari Bingwa wa Moyo?

Kuna mtu hapo nimemuuliza swali jepesi anajua fellowship ya cardiology inachukua miaka mingapi na inahusu nini hajajibu .

Hapo ndio nilipocheka na kufunga mjadala maana naona nitajadiliana na mtu ambaye mada imemzidi kimo.
There are several cardiology fellowship programs in the United States, including:

  • General Cardiovascular Medicine Fellowship
    A three-year program that provides training in clinical cardiology and cardiovascular research. The first two years are focused on core clinical training, and the third year is individualized.

  • Cardiovascular Diseases Fellowship
    A three-year program at the Mayo Clinic in Rochester, Minnesota that prepares fellows for academic medicine. The first two years satisfy the American College of Cardiology's Core Cardiovascular Training Statement (COCATS) requirements.

  • Advanced Interventional Cardiology Fellowship
    A one-year program that provides training in cardiac interventional procedures. Fellows work with a faculty mentor on a research project and can participate in a second year of training if they have an interest in peripheral or structural heart disease interventions.

  • Interventional Cardiology Fellowship
    A one-year program at UCSF that teaches fellows a range of diagnostic and interventional peripheral angiographic procedures.

  • Prevention Fellowship
    A one-year program at UCSF that trains general, non-invasive cardiologists to obtain expertise in prevention.
 
Nimekupa Mfano Sarungi, Hebu weka jina lake Tupe Matokeo
 
Unazungumzia habari za kina Dr. Sarungi ambao zama hizo walikuwa ni wao pekee kwa uchache walikuwa wamesomea ubingwa, tena nje kwa kuwa Tanzania hakukuwa na vyuo vya kufundisha mabingwa wa kutosha wa fani kama mifupa. Kwa sasa mambo yamebadilika mnoo.

Nenda sasa pale Muhimbili (MOI) ukakutane na vijana wadogo na wamoto sana wakijifunza vilivyo kuchoronga na kurekebisha mfupa kisasa kabisa.

Mwisho labda nikuambie ukweli, karibu madaktari bingwa wote wazuri wa pale Muhimbili ukija Aga Khan, Regency, Selfee, Hindu Mandal utakutana nao tena. Ni madaktari wale wale.
 
Mtoa maada umekurupuka sanaa, binafsi muda ule ule SSH alivyosema niliingia online nikaangalia vyanzo kama vinne hivi jamaa ana CV nzuri tu. Moja ya detailed CV mdau ameweka hapo juu. We umeenda kuchukua chanzo kimoja ambacho hakina taarifa za kutosha.

Japo nilitamani jamaa awe na qualifications flani za sheria zinasaidia kwenye uelewa wa baadhi ya policies hasa za kimataifa, kitu ambacho ilikuwa added advantage kwa Ndungulile.
 
Wewe hoja yako ya mwanzo umesema madaktari wote hadi wa 80s toka hizo Nchi hawana kitu, usianze kukataa ulichoandika,

Na si kweli kuna Madaktari kibao hizo Hospitali sio zao la Muhimbili, in short kuna kozi hata Tanzania hazipatikani kibao.

There is a reason kwanini hao madaktari wakubwa wakubwa Tanzania wamesoma Nje.
 
Mkuu, Hoja ya Mleta Uzi ni kwamba, Prof hana Ubingwa wa Magonjwa ya Moyo, akimaanisha kwamba, hajasoma Mmed (Masters of Medicine) in Internal Medicine na kisha kuspecialize kwenye Magonjwa ya Moyo. Kwenye CV, tunaona Prof ana MSc (Masters of Science) in Tropical Health, siyo Mmed.

Swali kwako, hizo specialization ulizozitaja, unaweza kusoma bila kuwa na Mmed?
 
Watanzania tuwe Wazalendo tunaweza kumuharibia hadi Dr Tulia PhD

Lucas Mwashambwa 😂
 
Dah!
Nakusikitia sana, umeandika usichokijua. Sikuja hapa JF kabla ya kuuliza, kudadisi na kuchunguza mwenyewe.

Kwa kukusaidia tu, neno fellowship lisikupe shida, ni neno la kawaida katika kujifunza professional yoyote. Narudia kuandika hapa, Professor Janabi hakuwahi kufanya Mmed ya internal medicine (udaktari bingwa wa magonjwa ya ndani) ambayo ndio sifa ya msingi ya kuweza kusomea superspecialist ya moyo. Professor hakuwahi kufanya. Kama aliwahi kusoma ni lazima Professional profile yake kule MCT ingesoma tu.
 
Madaktari wengi wa hapa ni hovyo sana.
Mlimpiga vita Dr Ferdinad Masau aliyekuwa wa kwanza kuanzisha heart institute na figisu na fitna nyingi hadi mzee wa watu akafilisiwa na kufa.
Akaja mzungu mmoja kuwa director Muhimbili mambo yalibadilika sana,naye mkampiga zengwe ili mchukue nafasi ninyi mafisadi wakubwa.
Mungu ni mwema akatuletea Prof Janabi mtu kweli kweli ,muadilifu na mimi ndiye namuona daktari wa pekee wa kisasa Tanzania.
Naye mnataka kutuaminisha hajasoma- upuuzi mtupu.
Ukisikiliza madaktari wengi wanatoa elimu,wanalisha watu matango pori sana.Mimi namheshimu Prof ni daktari wa kisasa,tofauti na wengi mmesoma kwa kukariri na huwa ham reason
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…