Ni kweli kwamba Profesa Janabi hajawahi kusomea wala kuwa Daktari Bingwa wa Moyo?

Ni kweli kwamba Profesa Janabi hajawahi kusomea wala kuwa Daktari Bingwa wa Moyo?

Ila
Hiyo cardiology ni political science? Waalimu mna tabu sana
Mkuu, mtoa mada amejieleza vizuri tuu, ya kwamba, kwa mujibu wa Baraza la Madaktari la Tanganyika (MCT) na Duniani kwa ujumla, ili uwe Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, ni lazima usome kwanza Masters of Medicine (Mmed) in Internal Medicine kisha ndo usome mambo ya Moyo.

Kwenye CV ya Prof, hakuna mahali panaonyesha Prof amesoma Mmed in Internal Medicine. Masters pekee iliyopo ni Masters of Science (MSc) in Tropical Health. Na ndiyo maana anasema Prof siyo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo.

Itapendeza kwa uelewa wako, ukipinga Hoja ya Mleta mada kwa kuonyesha ni kwa namna gani Fellowship ya Moyo inamfanya Prof kuwa Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo.

Tupunguze mihemuko. Tujadili Hoja kwa Nguvu ya Hoja na siyo Hoja ya Nguvu.
 
Sijui chochote kuhusu NAPLEX wala miaka ya kusomea Doctor of Pharmacy huko USA.

Ninachokifahamu ni kuhusu sifa za mtu kuwa mfamasia hapa Tanzania. Na ziko mbili tu.
1. Kuwa na degree ya Pharmacy inayotambulika na TCU.
2. Kusajiriwa katika bodi ya famasi ya (katika hali ya kawaida mhusika anfanya na kufaulu mtihani wa bodi)
Hapa Mkuu, naomba kusahihisha kidogo. Naamini itakuwa Baraza la Famasi Tanzania (Pharmacy Council of Tanzania - PCT) na siyo Bodi ya Famasi.
 
Professor Janabi hana qualification yoyote ya kutibu moyo kibingwa, hana. Hakusomea popote na hakuwahi kutambuliwa na baraza la madaktari hapa Tanzania kama Daktari bingwa wa moyo. Na hata pale Muhimbili hajawahi kutibu moyo mtu kibingwa tangu awepo. Hana huo uwezo.
Kwani kuna siku yeye alisema anatibu watu moyo?
 
Dah Unaamini Kwamba Janabi sio Daktari Bingwa..
Kweli leyman Wakiweza Kuandika wanaandika Vitu vinakeera...

Kama Mnamchukia Samia Mchukieni Ola msichukie Fani ya Kidaktari na Kuanza kuleta Dharau soon Mnanitafutia Bann Naona kabisa
Syo daktari bingwa ubingwa wake tuambie alisoma wapi.
Alisomea nini.
 
Acha roho mbaya. Kwani ww una cv nzuri zaidi ya Dr Janabi?

Akipigiwa debe unapata hasara GANI?
Anachokusudiwa kushindania akiachwa yeye wewe ni Bora zaidi yake?
Black skin sijui nani katuloga?
Ukiona mwenzio ana dalili ya kufanikiwa wewe roho inakuuma.

Una faidika nini na hiyo roho mbaya ⁉️
 
Upo sahihi mkuu SIASA ya nchi yetu imemfikisha hapo alipo fika,,, ni mtu muhimu sanaaaa kwenye system na ana siri nzito kwenye nchi yetu,,,, ACHA TUENDELEE KUMSIKILIZIA KA ATATOBOA WHO,,, kila lakheri kwake na kwa TAIFA
Aisee, ni kweli kabisa nakubaliana na wewe 100%
 
Mtoa maada umekurupuka sanaa, binafsi muda ule ule SSH alivyosema niliingia online nikaangalia vyanzo kama vinne hivi jamaa ana CV nzuri tu. Moja ya detailed CV mdau ameweka hapo juu. We umeenda kuchukua chanzo kimoja ambacho hakina taarifa za kutosha.

Japo nilitamani jamaa awe na qualifications flani za sheria zinasaidia kwenye uelewa wa baadhi ya policies hasa za kimataifa, kitu ambacho ilikuwa added advantage kwa Ndungulile.
Nadhani hujaelewa mada.
Hapa hatujadili CV ya Janabi kufaa au kutokufaa kugombea huko WHO, tunajadili sifa na uwezo wa Professor Janabi kutibu kibingwa moyo. Nimepitia CV zake zilizoshiba na nikagundua bila shaka yoyote kuwa mwamba hakuwahi kusoma na kuwa bingwa wa kutibu moyo na wala hana sifa stahiki za kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo. Kuna namna mwamba alikuwa ametoshota akili kimtindo.
 
Mmmh hapana.
Umechanganya vitu.
Sio kila fellowship inaweza kuwa equivallent na degree.
Phd ni degree ya juu (kitaaluma) sio lazima iwe ni degree ya tatu.

Phd ni degree ya juu ya kitaaluma
Fellowship ni mafunzo mahususi ya kitaalam.
🤣🤣 ndo maana Nimekuuliza Unajua Ulichokuwa unakisema..
FEllowship zinaanzia Miaka 2 Mpaka 10 inategemea Na Aina Ya Fellowship..
Sasa hayo mafunzo maalumu yenye Miaka mimgi ndo tunaita Fellowship..🤣🤣🤣
 
Mkuu hawa watu kuwaelewesha ni kazi , mimi ni muumini wa meritocracy.

Ndio maana mimi huwezi kukuta mtu aliyepewa udaktari kama ice cream design ya mama nimuite Dr.

Janabi shule amefanya tumkosoe kwa vingine [kama ambavyo kuna mtu kasema tangu aingie gharama za matibabu zimepanda MHN] , japo tunaaminishwa humu na machawa mama amefanikisha sijui mama anaupiga mwingi na ujinga mwingine.
Nimesoma mpaka mwisho bado sijaelewa mimi kilaza wa mambo ya afya.

Hoja ya mleta mada ingejibiwa kama mgemuhakikishia kuwa kuna uwezekano wa mtu kuwa daktari bingwa mbobezi wa moyo bila kuwa na hiyo Mmed anayolalamikia mleta mada kwamba Prof. Janabi hana.

Anadai kwamba kuna hatua ya MD, kisha hatua ya Mmed kisha ubingwa na ubobezi unafuatia. Je kuna njia ya kuruka Mmed ila ukawa cardiologist?
Kama inawezekana kule Marekani, Japan au hapa nchini mumsaidie mleta mada. Mmojawapo kagusia fellowship, je hii inaweza simama kama mbadala wa Mmed?

cc DR Mambo Jambo
 
Pale taasisi ya moyo ya Jakaya kikwete kuna tapeli mmoja anaitwa Prof Ny........ yule jamaa jamaa ni tapeli ana clinic zake za kitapeli morogoro.Kuna jambo alilifanya nitakuja kuliweka humu hadharani siku moja
 
Hapa Mkuu, naomba kusahihisha kidogo. Naamini itakuwa Baraza la Famasi Tanzania (Pharmacy Council of Tanzania - PCT) na siyo Bodi ya Famasi.
Nashukuru sana kwa kunisahihisha.
Kwangu mimi mabaraza ya kitaaluma na bodi za usajiri wa kitaalamu huwa ninaziweka kapu moja, kwa maana ya mantiki ya wanachokifanya.
Sisi wa fani zingine kama Uhandisi na uhasibu tumezoea maneno bodi, bodi, bodi tukidhani hata huko kwenye afya ni bodi kumbe mabaraza!
 
Mmmh hapana.
Umechanganya vitu.
Sio kila fellowship inaweza kuwa equivallent na degree.
Phd ni degree ya juu (kitaaluma) sio lazima iwe ni degree ya tatu.

Phd ni degree ya juu ya kitaaluma
Fellowship ni mafunzo mahususi ya kitaalam.
Sijui kama Ulichokiandika Umekisoma vizuri 🤣🤣🤣
Tuchukulie Mfano..
Mfano Mimi Ni Neonatologists
Nilifanya Neonatal fellowship Kwa Miaka Mitatu..
Baada ya Kupata MMED(Paed) degree ya Pili Au master Ya Miaka 3..

Kwahyo Fellow Huku Medicine tunairegard kama Degree ya tatu SO its equivalent na Phd Kama utakuwa Kwenye Track ya Proffesional ila Ulitoka kwenye proffesional Ndo unaweza ouchukua Degree ya Utawala ila ukibaki huku ndo unakuwa Super so Ma Super wote ni.Phd Holder..

Au Wanaitwa Wabobezi...
 
Mueleze vema. Alichosema ni sahihi hajasomea hilo eneo kwenye post graduate… kilichomfanya kuwa hapo ni hizo unazoziita fellowship au kwa jina lingîne ni professional certificates

Tunao cardiologist pure…. Janabi is not bali ana professional certificates
Tanzania Tuna Cardiologist Yaani wabobezi nahisi wenye fellowship 11 Kama sijakosea Zaidi ukiacha Wale wenye bachelor za Cardio
 
Alifanya Fellowship ya Moyo mkuu Usizushe kitu usichokijua..
Soma Hii Link
Mkuu, kwa kuwa unajitambulisha kwa Jina la Dr Mambo Jambo, naomba kuuliza swali kutokana na ulichoandika. Je, Fellowship ya Moyo peke yake, inatosha kumfanya Daktari yoyote kuwa DaktrBingwa wa Magonjwa ya Moyo?

Zaidi, unaweza kutueleza sifa za Kitaaluma za Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo?

Itapendeza kunipatia majibu ya maswali haya na kufanya huu mjadala kuwa na tija zaidi.
 
Nimesoma mpaka mwisho bado sijaelewa mimi kilaza wa mambo ya afya.

Hoja ya mleta mada ingejibiwa kama mgemuhakikishia kuwa kuna uwezekano wa mtu kuwa daktari bingwa mbobezi wa moyo bila kuwa na hiyo Mmed anayolalamikia mleta mada kwamba Prof. Janabi hana.

Anadai kwamba kuna hatua ya MD, kisha hatua ya Mmed kisha ubingwa na ubobezi unafuatia. Je kuna njia ya kuruka Mmed ila ukawa cardiologist?
Kama inawezekana kule Marekani, Japan au hapa nchini mumsaidie mleta mada. Mmojawapo kagusia fellowship, je hii inaweza simama kama mbadala wa Mmed?

cc DR Mambo Jambo
Walau wewe umeuliza vyema ninaweza kukujibu hasa huo mstari wa mwisho.

Mtu kufanya fellowship kuna miaka 2 ya kufanya clinical practice chini ya usimamizi wa wataalam na mwaka mmoja wa mwisho mtu hawi limited sana chini ya usimamizi na kama mtu anatambulika na taasisi kubwa za cardiology U.S mtu ataibukaje kusema sio mbobezi?

Ndio maana nimemuuliza katika uwiano wa ufamasia japo hakuelewa concept yangu standard za Tanzania hazifanani na US na ukija katika ubora mtu aliyefanya ubobezi US atachukuliwa kabla ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom