Ni kweli kwamba Profesa Janabi hajawahi kusomea wala kuwa Daktari Bingwa wa Moyo?

Ngoja nikuulize tena hili swali.

Mtu aliyefanya Doctor of Pharmacy [PharmD] U.S , Tanzania anatambulika kama nani?
 
Lakini inatutia doa sana kuupeleka ujinga wetu kimataifa,yaani wenzetu wanapambana kupeleka vichwa sisi tunapeleka vituko?

Aibu sana bora kama waliona hamna mwengine zaidi yake wangeuchuna tu ingekuwa siyo kesi.
Kule wanaangalia cv na sio mhamashishaji
Jamaa kwa huku ndani ni daktari mzuri hilo halina ubishi ila ana-cv ya kawaida
 
So mkuu basi tukupendekeze wewe basi uende huko WHO lakini inaonekana wivu wa kijinga ndiyo unaokusumbua.
 
Dk kisenge ndo mpaka dakika za mwisho alikuwa daktari wa magufuli
 
Ngoja nikuulize tena hili swali.

Mtu aliyefanya Doctor of Pharmacy [PharmD] U.S , Tanzania anatambulika kama nani?
Akija hapa Tanzania TCU wata equivalent hicho alichosomea kama Degree of Pharmacy, na atatambulika kama mfamasia tena baada ya kuomba usajiri (ikiwemo kufanya mitihani ya bodi ya famasia).
 
Hoja ya Mleta mada siyo kwamba Prof hajasoma bali Prof hajasomea na hana Udaktari Bingwa wa Moyo kama ambavyo anatambulika kwa kuwa hajasoma Mmed (Masters of Medicine) in Internal Medicine kwanza kabla ya hiyo Fellowship ya Moyo kwa mujibu wa taratibu zilizopo.

Unajua zamani au mpaka sasa vijijini, hata waliosoma Clinical Officer au Assistant Medical Officer, wanaitwa nankujulikana Madaktari (kwa maana ya Medical Doctor) ilhali hawana/hawajasoma Degree of Medicine.

Ni vizuri tujaribu kumuelewa Mleta Hoja, na kujibu Hoja zake kwa ufasaha. Tuepueke mihemuko kisa anayeongelewa ni Prof.
 
Unaweza kuwa unamuelewesha mtu hivi kumbe kasoma zake HKL hata hakuelewi anakazania ubishi tu
 
Niko pamoja na wewe,watu wengi wanamsikiliza wakaiamini ni bingwa wa moyo
 
Natamani ungesema neno kuhusu sifa/taratibu za kuwa /kusomea Udaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, maana, ndiyo Hoja hasa ya Mleta mada kuhusu Prof.
 
Akija hapa Tanzania TCU wata equivalent hicho alichosomea kama Degree of Pharmacy, na atatambulika kama mfamasia tena baada ya kuomba usajiri (ikiwemo kufanya mitihani ya bodi ya famasia).
Mfamasia Tanzania anasoma miaka mingapi?

Doctor of Pharmacy ( PharmD)? inasomwa miaka mingapi U.S.

Criteria gani zitamruhusu mtu kufanya mtihani wa bodi ya PCTZ.

Na Criteria gani zitamruhusu mtu kufanya NAPLEX ?

Mtu akishafanya NAPLEX ataruhusiwa kufanya practice moja kwa moja bila kufanya mtihahi PCTZ ?

Na je mtu mwenye leseni ya PCTZ anaruhusiwa kufanya practice U.S bila kufanya NAPLEX?
 
Kuna wakati inabidi tukubaliana kwamba sio Kila kitu mtu unakuwa na uelewa nacho kama hujui kitu uliza ueleweshwe la sivyo utajitia aibu .
 
Dk kisenge ndo mpaka dakika za mwisho alikuwa daktari wa magufuli
Hapo umenena ukweli.
Huyo msela (Dr. Kisenge?) amesoma na ana tibu moyo mpaka sasa. Professional profile yake kule MCT inaonyesha ana Md, Mmed (internal medicine) na Msc (Cardiology) ambayo ndio cardiac superspecialist.
Naambiwa hata kesho ukitinga pale JKCI una shida ya moyo atakutibu yeye mwenyewe fresh na kwa uhakika.

Hicho kitu Prof Janabi hana na hawezi. Why? Hakusomea.
 
Kaileta nje ya context hasa bila kujua kwa kina exposure ni muhimu.

Nitamkosoa Janabi kwa vitu vingine sio elimu yake..

Unajua zamani au mpaka sasa vijijini, hata waliosoma Clinical Officer au Assistant Medical Officer, wanaitwa nankujulikana Madaktari (kwa maana ya Medical Doctor) ilhali hawana/hawajasoma Degree of Medicine.
Hii unaongelea miaka mingapi nyuma ?
Ni vizuri tujaribu kumuelewa Mleta Hoja, na kujibu Hoja zake kwa ufasaha. Tuepueke mihemuko kisa anayeongelewa ni Prof.
Yeye mwenyeww kaleta mada asiyoelewa ndio maana unaona anaruka viunzi.
 
Unajua sana Mwamba....Umetisha
 
Yeye alikuwa mpenyeza taarifa kwenda kwa Kikwete na wapambe wa JK kama wakina Zitto
 
Sijui chochote kuhusu NAPLEX wala miaka ya kusomea Doctor of Pharmacy huko USA.

Ninachokifahamu ni kuhusu sifa za mtu kuwa mfamasia hapa Tanzania. Na ziko mbili tu.
1. Kuwa na degree ya Pharmacy inayotambulika na TCU.
2. Kusajiriwa katika bodi ya famasi ya (katika hali ya kawaida mhusika anfanya na kufaulu mtihani wa bodi)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…