Ni kweli kwamba Profesa Janabi hajawahi kusomea wala kuwa Daktari Bingwa wa Moyo?

Ni kweli kwamba Profesa Janabi hajawahi kusomea wala kuwa Daktari Bingwa wa Moyo?

Hii Elimu yake inatusaidia nini kwa Kipindi hiki?

Jambo la Msingi aungwe Mkono.

Huu Upuuzi wa Elimu umebakia sana hapa kwetu Africa Mashariki.

Huko kwa Mabeberu kinachoangaliwa ni Uwezo wako Ku deliver.

Tuachaneni na Hizo mambo za Kuangalia Elimu , hazilijengi Taifa.
Elimu yake ikusaidie wewe kivipi?

Kusoma asome yeye kwa shida halafu eti unakaa hapa na kupanua pua eti "elimu yake inatusaidia nini"

Wewe nani kakwambia anakusaidia kwa lolote?

Elimu ni yake inamsaidia yeye binafsi na familia yake na sio jamii

Jamii inalipia kupa his services wewe included,hakuna cha msaada wowote

Hii tabia ya jamii kukaa na kujipa mamlaka ya kumiliki elimu au mali za watu eti zipo kwa ajili wao kusaidiwa ni one of the biggest stupidity ever
 
hizi elimu za ku google tabu sana, sasa mumegoogle elimubyake ili iweje, muda mwingine google inakuletea majibu kutegemea unatembeleaga site zipi mara kwa mara google
Hakuna mtu kagoogle, sifa za madaktari wote waliosajiriwa kutibu zipo baraza za madaktari (MCT), na wao taarifa zote wameziweka wazi kwa umma ili kila mtu azione na ajiridhishe kila anapotaka kutibiwa.

Hata wewe unaweza kuingia sasa kwenye ukurasa wa baraza la madaktari ni kuangalia official medical professional profile&status ya Daktari yoyote yule wa hapa Tanzania. Nenda (MCT Doctor search), ingiza jina utaona.
 
Fellowship[emoji16][emoji16][emoji6][emoji6]
Huo ndo ubobezi kwenye kutibu moyo?

Anyway hata hivyo hakuwahi kutibu bali alikuwa mtawala ktk hospitali ya JKSI na alikua anashiriki na madaktari bingwa kama msaidizi(kama walivyo manesi) wakati wa operation.
Hawezi kuwa second oncall kwenye ishu ya moyo[emoji3][emoji2][emoji3][emoji2][emoji3][emoji2]
Dah Unaamini Kwamba Janabi sio Daktari Bingwa..
Kweli leyman Wakiweza Kuandika wanaandika Vitu vinakeera...

Kama Mnamchukia Samia Mchukieni Ola msichukie Fani ya Kidaktari na Kuanza kuleta Dharau soon Mnanitafutia Bann Naona kabisa
 
Acha uongo ndugu yangu.
Standard ya elimu ya utabibu kipindi cha USSR mpaka leo hii haijawahi kuwa bora kupita yetu katika kipindi chochote kile. Mhitimu wa Muhimbili amekuwa better dhidi ya hao wa USSR.
Me mwenyewe nimehitimu MUHAS ila kulinganisha elimu ya sekta ya afya ya urusi na Tanzania ni kukosa heshima
 
Pengine wewe ndio huelewi ulichokiandika.

Mosi Unaelewa kwanza fellowship ni nini?[ yaani inahusu kitu gani].

Pili unaelewa fellowship kwaUS kwenye cardiology inachukua miaka mingapi?

Na tatu unaelewa mtu akimaliza fellowship anaenda kuwa nani?

Mimi naishi hapa nikwambie tu mfumo wa N.America particularly U.S na CA huwezi kusoma degree let's say ya Medicine kama hujafanya first degree ya science.

Ukimaliza hapo ndio unaweza fanya M.D , the same to law huwezi fanya L.L.B kama hujafanya shahada ya kwanza katika kitu kingine ndio uende LLM au JD[ hii sijui kwa Tanzania equivalent yake ni nini]

Huyo Janabi alifanya hiyo akiwa na shahada tayari hivyo alikuwa qualified kuingia kwenye ubobezi.
Unachokiandika hakina hata mantiki, hufamu kitu, nenda katafiti upya.

Mtu unawezaje kufanya Fellowship ya ubingwa wa moyo (super specialist) kama hujawahi kuwa Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani (internal medicine specialist)? Yaani mtoto ameanza kutembea na kuongea kabla ya kuzaliwa. Hakuna kitu kama hicho duniani.
 
Fellowship Ni sawa na Degree ya Tatu kwa degree za kawaida..
Ila kwa Madaktaru Huitwa Hivyo..
Yaani Ni sawa na PhD
Mmmh hapana.
Umechanganya vitu.
Sio kila fellowship inaweza kuwa equivallent na degree.
Phd ni degree ya juu (kitaaluma) sio lazima iwe ni degree ya tatu.

Phd ni degree ya juu ya kitaaluma
Fellowship ni mafunzo mahususi ya kitaalam.
 
Upo sahihi mkuu SIASA ya nchi yetu imemfikisha hapo alipo fika,,, ni mtu muhimu sanaaaa kwenye system na ana siri nzito kwenye nchi yetu,,,, ACHA TUENDELEE KUMSIKILIZIA KA ATATOBOA WHO,,, kila lakheri kwake na kwa TAIFA
 
Sio nakupiga kamba, nenda popote katika hii nchi kaulize madaktari watakwambia hichi kitu.
Mhitimu (fresh from university) wa udaktari wa binadamu (Md) aliyehitimu USSR ya zamani, Russia ya sasa, Ukraine, China au India hana uwezo kamili wa kutibu mgonjwa kumkaribia mhitimu wa hapa Tanzania hususani kutoka Muhimbili. Na siri ni moja tu, daktari mwanafunzi, tena mgeni kutoka afrika, halafu mwenye ngozi nyeusi hawezi kupewa nafasi kamili ya kujifunza kwa kutibu (clinical practice) kwenye mwili wa mzungu (mrusi), mchina au mhindi.
Ungesema sio watu wote waliosoma nje wamesoma vyuo vyenye hadhi kama Muhimbili hapo ungeeleweka, ila kuclaim yoyote aliesoma USSR, India ama China kapitwa na Muhimbili hii kamba mkuu, Unahisi mtu asome Chuo Prestigious kama St Petersburg Chuo kinachotoa watu walio badili dunia Umfananishe na Muhimbili?

Ukiangalia Hivyo vyuo Alivyosoma Janabi ndio kumegunduliwa vitu kama Vitamin B6, wametoa watu kibao walioshinda Noble prize etc ufananishe na Muhimbili kweli?
 
Amefanya fellowship U.S huyo tumkosoe kwa vingine kuhusu elimu kanyooka huyo jamaa hakuna ukanjanja hapo.

Hao MCT wafanye maboresho ya kanzidata yao.
Nenda pale Muhimbili utakutana na wauguzi kibao wamefanya fellowship na sio madaktari bingwa wabobezi. Na pia kuna madaktari kibao wapo muhimbili wamefanya fellowship mbali mbali na bado sio madaktari bingwa wabobezi (super specialist).

Kufanya fellowship hakukufanyi kuwa daktari bingwa, na sio kila fellowship itakufanya kuwa superspecialist.

Professor Janabi haijarishi aliwahi kufanya fellowship gani, kama hakuwahi kufanya Mmed ya internal medicine hana chembe ya sifa yoyote ya kuwa Daktari bingwa wa moyo. Hiyo ndio kanuni ya kudumu ya baraza la madaktari.
 
Dah Unaamini Kwamba Janabi sio Daktari Bingwa..
Kweli leyman Wakiweza Kuandika wanaandika Vitu vinakeera...

Kama Mnamchukia Samia Mchukieni Ola msichukie Fani ya Kidaktari na Kuanza kuleta Dharau soon Mnanitafutia Bann Naona kabisa
Mkuu hawa watu kuwaelewesha ni kazi , mimi ni muumini wa meritocracy.

Ndio maana mimi huwezi kukuta mtu aliyepewa udaktari kama ice cream design ya mama nimuite Dr.

Janabi shule amefanya tumkosoe kwa vingine [kama ambavyo kuna mtu kasema tangu aingie gharama za matibabu zimepanda MHN] , japo tunaaminishwa humu na machawa mama amefanikisha sijui mama anaupiga mwingi na ujinga mwingine.
 
Nenda pale Muhimbili utakutana na wauguzi kibao wamefanya fellowship na sio madaktari bingwa wabobezi. Na pia kuna madaktari kibao wapo muhimbili wamefanya fellowship mbali mbali na bado sio madaktari bingwa wabobezi (super specialist).

Kufanya fellowship hakukufanyi kuwa daktari bingwa, na sio kila fellowship itakufanya kuwa superspecialist.

Professor Janabi haijarishi aliwahi kufanya fellowship gani, kama hakuwahi kufanya Mmed ya internal medicine hana chembe ya sifa yoyote ya kuwa Daktari bingwa wa moyo. Hiyo ndio kanuni ya kudumu ya baraza la madaktari.
Ukileta criteria ya Mmed ya Internal medicine wewe unakuwa umetumia standard za wapi Tanzania au U.S hebu nijibu hapo.

Na kwa uelewa wako Janabi sasa kama unavyodai anapractice kama mbobezi wa kitu gani huko?
 
Back
Top Bottom