Ni kweli mtu akitumia dawa ya UKIMWI hawezi kumuambukiza mwenzake hata bila kutumia kinga?

Ni kweli mtu akitumia dawa ya UKIMWI hawezi kumuambukiza mwenzake hata bila kutumia kinga?

Ndiyo maana unaweza kuoa au kuolewa na muathirika ambaye anajijali na akiwa anazingatia dozi ,vyakula na maelezo ya daktari kwa usahihi hauwezi pata hadi mnazeeka.
Mimi hii kauli ya " Kama atazingatia dozi vizuri......." ndiyo inayonitisha... Binadamu bwana hatupo perfect.. Ina maana siku moja akiteleza au akawa mrejevu kwenye kuzingatia dozi kwa wakati tayari unao.
Sasa yote haya ya nini? Hapo si kama umeyaweka rehani masiha yako kwake? Yani kiufupi yeye ndyo ameishikilia roho yako na ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho ya kukuambukiza ama kutokuambukiza HIV.
 
🤣🤣🤣 bahati yako nilishaenda kufunua kitabu cha matusi mfyuuu!!

Sasa bebe ana miwaya mi wa nini.?? Pesa ikahatarishe afya yangu??!! Hivi unajua km mtaji wa kwanza hapa duniani ni afya yako??
Jirani ilinde afya yako kwa gharama yoyote ile ikiondoka imeondoka nakwambia oooh!!
Jirani ndio upo hivi au ni kwa kipindi hiki cha mfungo tu ?😂

Afya njema ni mtaji
 
Kanuni ya ukimwi ni hii hapa kitabibu

Undetectable = Untrunsmitted

vidonge vya kupunguza makali ya ukimwi huwa yanafanya virusi visiongezeke kwa kasi hivyo kuvizuia vibaki vichache ndani ya seli hai yaani "copies per cell" na idadi ya virusi vinavyohitajika ndani seli ili mtu asiweze kuambukiza ni chini ya 200 kwa kila seli.

Kiwango hicho ndicho wataalamu huita undetectable na kama ni undetectable hii inamaanisha haviwezi kuambukiza.

Ndiyo maana unaweza kuoa au kuolewa na muathirika ambaye anajijali na akiwa anazingatia dozi ,vyakula na maelezo ya daktari kwa usahihi hauwezi pata hadi mnazeeka.
Ookay
 
Mimi hii kauli ya " Kama atazingatia dozi vizuri......." ndiyo inayonitisha... Binadamu bwana hatupo perfect.. Ina maana siku moja akiteleza au akawa mrejevu kwenye kuzingatia dozi kwa wakati tayari unao.
Sasa yote haya ya nini? Hapo si kama umeyaweka rehani masiha yako kwake? Yani kiufupi yeye ndyo ameishikilia roho yako na ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho ya kukuambukiza ama kutokuambukiza HIV.
😅😅 sina comment mkuu
 
100% Ni kweli..
Na watu wengi sana wanaishi ni Serodiscordant..
Sisemi Kwa ushabiki bali nimeshuhudia sana..
Watu wengi ambao mara Nyingi tunaruhusu mahusiano hayo ni wale waliopima HVL na mara nyingi Huwa Zinasoma TND..("Target Not Detected")

Huyu ana Percent chini ya 0.01 ya kumuambika mwingine na hata wakinamama wakifika Hapa huwa wanaruhusiwa kuwa na watoto yaani kuchukua mimba na kuzaa..
Watu hawajiulizi kwanini Serostatus (Maambukizi) ya Watu hayaongezeki na yanazidi kupungua?

Kwanini siku hizi Idadi ya watoto Wadogo wenye maambukizi imepungua Sana tofauti na Zamani..

Jibu Ni moja Tu kuwa inawezekana na mifano ninayo na nimeiona si chini ya couple 100 zikiishi hivyo na kwa furaha

Kama kuna mtu mwenye swali namkaribisha maana hii ni moja ya Sehemu zangu za kujidai
Hongera Dr...umeiweka vizuri,tatizo Wana JF woteee humu wanajifanya wako negative, sasa sijui watakuelewa?😅
 
Back
Top Bottom