Ngoja nikupe somo la bure hapa
Umedai kwamba hayo maneno uliyowekewa na mtumishi
ISHAMel sio maneno ya Yesu au kwa lugha nyingine hapo hakuzungumzwa Yesu,ngoja tuone maandiko yanasema nini kuhusu Yesu na kuhusu kuwa Alfa na Omega
Ufunuo 1:7
7 Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.
Kwenye huo mstari tunaona Yohana anasema kwamba kuna atakaekuja na kila jicho litamuona na wote waliomchoma na kabila zote za dunia zitaomboleza kwaajili yake
Kwa lugha rahisi kabisa inaeleweka ni nani atakaekuja kwenye mawingi na inaeleweka ni nani aliechomwa,huyu sio mwingine bali ni Yesu Kristo [Danieli 9:26 kwa ushahidi na hii hapa chini kwa uthibitisho zaidi
Mathayo 24:30
30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
Huo ushahidi unaonesha kabisa huyo anaesemwa kwenye Ufunuo hapo juu ni Yesu Kristo,sasa fungua moyo wako kupata ushahidi utakaoitikisa ngome ya imani yako na kuisambaratisha kwa kishindo cha ukuu wa Mungu mkuu
Ufunuo 1:8
8 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.
Maneno hayo yanaonesha huyo anaezungumza anasema kuna wakati atakuja,sote tunajua kabisa kwamba atakaekuja sio Miwingine ila ni Yesu Kristo,hili ni wazi kwasababu maandoko yameyuthibitishia kwamba Yesu ndie atakaekuja kama hayo maandiko hapo juu yanavyotuonesha,kwa mujibu wa maandiko ni kwamba atakaekuja ni Yesu Kristo siku hiyo ya mwisho pamoja na Jeshi kuu la mbinguni na sio Mungu baba
Ufunuo 19:11-13
11 Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.
12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
Maandiko hayo hapo juu yanatuyonesha kwamba huyo ambae atakuja ni neno la Mungu,ngoja tuitazame Biblia inasema neno la Mungu ni nani
Yohana 1:8
14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Sote tunajua kwamba aliefanyika mwili ambae ni neno ni Yesu Kristo hivyo hili linaendelea kuthibitisha kwamba ni yule ambae alisemwa kwenye Ufunuo 1 kwamba ni Alfa na Omega
Ufunuo 1:17-18
17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
Sasa hapo tunaona maneno kutoka kwenye kinywa cha mhusika mwenyewe ambae anasema ni wa kwanza na wa mwisho sawasawa na Alfa na Omega,lakini anaendelea kusema kwamba alikuwa amekufa na sasa yu hai,hakuna yoyote ambae alikuwa amekufa na akawa hai tofauti na Yesu Kristo
Dada yangu Faiza,huna namna ya kukataa haya na yapo wazi kabisa kwa mba Yesu ni Alfa na Omega na ni Mungu mwenyewe [Ufunuo 1:7]
Glory to God Faiza ......
Karibu kwenye furaha ya kweli kwa Yesu Kristo Mungu mkuu aliekuumba wewe,Kahtaan na mimi na wote pia!