Ni kweli Mungu hana Upendo? Au sisi tu ndio hatumuelewi!?

Ni kweli Mungu hana Upendo? Au sisi tu ndio hatumuelewi!?

Faiza wewe najua ni mtu mzima sasa nakushangaa sana unapokuwa kama mtoto

Uliniuliza swali halafu kabla ya kukujibi nilitaka muongozo wa namna ambavyo nitakujibu,hujanijibu maswali yangu ambayo majibu yako yangenipa muongozo ili nikujibu na matokeo yake unaniuliza tena mimi swali,huu ni utaratibu gani wa majadiliano?

Jibu maswali niliyokuuliza ili tuendelee au kama hutaki kujibu nitakuwa nimeishia hapa kwenye mjadala huu mimi na wewe!

Wewe achana na utoto wangu, hiyo ni sifa kubwa sana unanipa.

Jibu hoja, kama hauna majibu kaa kimya. Wacha kuhororoja na kubwabwaja bila mpango.

Wapi Yesu anasema "Mimi Mungu"?
 
Eiyer we mungu wako alishindwa kuwasamehe madhambi mpaka akaamua kujitoa roho yake mwenyewe..
Hakushindwa bali kwasababu Mungu wangu hajipingi wala habadiliki badiliki kimaamuzi aliamua kuziheshimu sheria zake alizoziweka kwani alisema kwamba hakuna dhambi ambayo haitaadhibiwa kwasababu kuadhibu ni kutoa stahiki na kutoadhibu ni kuvunja sheria yake mwenyewe

Pamoja na hilo,Mungu wangu alisema yeye ni hakimu wa haki na ni Mungu mwenye huruma,isingewezekana kufanya kimojawapo bila kutumia njia aliyoitumia

Kwasababu Mungu ni wa huruma na ni hakimu wa haki lakini pia aliahidi kila dhambi ataiadhibu na kwasababu ni hakimu wa haki na kwasababu alitupenda zaidi wanadamu aliamua aadhibiwe yeye kwa makosa yetu ili tuwe huru

Kama unataka maelezo mazuri kuhusu hili soma mada ...
Soma sifa za Mungu wangu anapotaka kusamehe madhambi. .

Quraan As-shuaraa.

وَهُوَ الَّذِي يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَعْفُو عَنِ السَّيِّئَاتِ وَيَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ

Naye ndiye anaye pokea toba kwa waja wake, na anasamehe makosa, na anayajua mnayo yatenda. Eiyer Mungu wa Kweli Hana haja ya Kufa ili wewe usamehewe, yeye anatoa amri tu mambo yakawa.

Mungu wako ni hakimu wa haki na ni mungu mwenye huruma?
 
Wewe achana na utoto wangu, hiyo ni sifa kubwa sana unanipa.

Jibu hoja, kama hauna majibu kaa kimya. Wacha kuhororoja na kubwabwaja bila mpango.

Wapi Yesu anasema "Mimi Mungu"?

Nataka sana kukujibu lakini siwezi kujibu swali kama mlevi ...

Niambie,unataka nikujibu kwa kutumia ushahidi gani?
Huo ushahidi ambao unataka nikujibu unauamini kwamba haudanganyi?
 
sifa za mungu wenu
1. wa upendo
2. mwenye nguvu
3. mjuzi wa yote
4. muweza wa yote
4. mponyaji
6. mwokoaji

lakini kwanini dunia yetu haionyeshi kuna nguvu inaconotrol hayo yote watoto wadogo wanafanyiwa ukatili wa ajabu, majanga ya kutisha, vita kila siku global warming at alerming rate bado ajali zinaua hata wachungaji.

Hii nchi ina binadamu wa ajabu sana ....

Huyu anauliza kitu ambacho kimejibiwa kwenye mada,haya matatizo yakutokusoma sijui yatakwisha lini kwenye hii nchi ....!!
 
Hakushindwa bali kwasababu Mungu wangu hajipingi wala habadiliki badiliki kimaamuzi aliamua kuziheshimu sheria zake alizoziweka kwani alisema kwamba hakuna dhambi ambayo haitaadhibiwa kwasababu kuadhibu ni kutoa stahiki na kutoadhibu ni kuvunja sheria yake mwenyewe

Pamoja na hilo,Mungu wangu alisema yeye ni hakimu wa haki na ni Mungu mwenye huruma,isingewezekana kufanya kimojawapo bila kutumia njia aliyoitumia

Kwasababu Mungu ni wa huruma na ni hakimu wa haki lakini pia aliahidi kila dhambi ataiadhibu na kwasababu ni hakimu wa haki na kwasababu alitupenda zaidi wanadamu aliamua aadhibiwe yeye kwa makosa yetu ili tuwe huru

Kama unataka maelezo mazuri kuhusu hili soma mada ...

Mungu wako ni hakimu wa haki na ni mungu mwenye huruma?

Wewe unamjuwa Mungu? wewe unalijuwa sanamu la mzungu lililovishwa nepi unaloliabudu.

Hapo sasa.
 
Unapomjadili Mungu wangu tafadhali usiniandikie jina lake ukaanza na "m".

Ndio Mungu wangu ni Hakimu wa Haki Na Ni mwenye Rehema Na Huruma. Na hapo hapo ni Mkali kwa wenye Viburi na wafanya HARAMU.

Sasa leta maswali yako ya mtego.
 
Wewe unamjuwa Mungu? wewe unalijuwa sanamu la mzungu lililovishwa nepi unaloliabudu.

Hapo sasa.

Hakuna kitu cha ajabu sana duniani kama mtu anapoamua kuwa mjinga kwa hiyari yake mwenyewe

Kwanini unaniwekea maneno mdomoni?
Niulize mimi namjua Mungu ama simjui na huyo Mungu ninaemjua ni yupi na sio kujilisha ujinga tu!
 
Unapomjadili Mungu wangu tafadhali usiniandikie jina lake ukaanza na "m".

Ndio Mungu wangu ni Hakimu wa Haki Na Ni mwenye Rehema Na Huruma.

Sasa leta maswali yako ya mtego.
Haki maana yake nini kwa mtazamo wako?
Huruma ni nini kwa mtazamo wako?

Nataka nikuulize swali kutokana na maoni yako wewe kuhusu yote hayo mawili ndio maana nimekuuliza hayo maswali,hivyo basi nijibu ili nikuulize swali!
 
Hakuna kitu cha ajabu sana duniani kama mtu anapoamua kuwa mjinga kwa hiyari yake mwenyewe

Kwanini unaniwekea maneno mdomoni?
Niulize mimi namjua Mungu ama simjui na huyo Mungu ninaemjua ni yupi na sio kujilisha ujinga tu!

Huyu mzungu mnaemuabudu mlio mvisha nepi vipi?

1a566-jesusoncross.jpg
 
natamani nicomment hii mada ila mmh sijaisoma maana ni ndefu sana, atayeweza kufupisha anisaidie maana huu uwezo wa kusoma mada ndefu nahifadhi kwa kusoma bible tu
 
Wewe achana na utoto wangu, hiyo ni sifa kubwa sana unanipa.

Jibu hoja, kama hauna majibu kaa kimya. Wacha kuhororoja na kubwabwaja bila mpango.

Wapi Yesu anasema "Mimi Mungu"?

Revelation 21:7
 
Eiyer ubarikiwe sana mkuu,binafsi nimekusoma na kupata mambo mazuri mengi hapo,na hasa hapo mwisho jinsi Mungu alivyosolve equation ya kumuokoa binadamu bila kutangua adhabu bali kuitimiliza kwa kumtumia Yesu,na ndio maana siku ya kiama wale wasiokubali dhabihu ya mwana wa Adamu (kwa makusudi) wataibeba adhabu wenyewe.Nimekupata uzuri sana,pamenigusa hapo mno.Nina jambo moja la kuuliza humu wana jf tujadili.Hivi wana jf,tunaelewa nini tunaposikia maneno haya matatu:wema,uovu na haki?
 
Last edited by a moderator:
Tazama usivyokuwa na haya, unaibadili biblia kwa mkono wako, kuna "Jesus" kwenye hiyo aya ya 6? hata Wakristo wenzako wakiisoma watakushangaa jinsi unavyojaribu kuichakachuwa Biblia kijinga kabisa.

Hoya quote context ujione ulivyo juha:

Revelations 21: 1-8
1 And I saw a new heaven and a new earth: for the first heaven and the first earth were passed away; and there was no more sea. 2 And I John saw the holy city, new Jerusalem, coming down from God out of heaven, prepared as a bride adorned for her husband. 3 And I heard a great voice out of heaven saying, Behold, the tabernacle of God is with men, and he will dwell with them, and they shall be his people, and God himself shall be with them, and be their God. 4 And God shall wipe away all tears from their eyes; and there shall be no more death, neither sorrow, nor crying, neither shall there be any more pain: for the former things are passed away. 5 And he that sat upon the throne said, Behold, I make all things new. And he said unto me, Write: for these words are true and faithful. 6 And he said unto me, It is done. I am Alpha and Omega, the beginning and the end. I will give unto him that is athirst of the fountain of the water of life freely. 7 He that overcometh shall inherit all things; and I will be his God, and he shall be my son. 8 But the fearful, and unbelieving, and the abominable, and murderers, and whoremongers, and sorcerers, and idolaters, and all liars, shall have their part in the lake which burneth with fire and brimstone: which is the second death.

This is not Jesus speaking but rather the Father. As it says I will be his God and he will be my son. Or does Jesus have a son now?

Ndiyo maana ulikuwa unaweka manamba badala ya aya? ulijuwa hapa huchomoki.

Na kama hiyo ya Kiingereza haikutoshi hii hapa ya Kiswahili:

1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.
6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.

7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.

8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar

Hapo kwa kuchakachuwa kwako maneno ya biblia kama uko mahakama ya Kanisa hukumu yako ni nini?

Unasikitisha sana. Hivi ndivyo mnavyodanganyana na ndivyo unavyodangaya wenzako humu?

Ngija Mkristo mwenzako aje kukusaidia na awe mkweli, kama yu amfata Kristo.

Eiyer njoo msaidie Ishmael tumembamba anachakachuwa biblia. Ndiyo sababu alikuwa anaweka manamba hataki kuweka aya, kuiweka kuiona haikidhi matakwa yake akatia maneno yake kwenye biblia. Aibu kubwa sana.
Ishmael fanya toba ya ukweli la sivyo hutouona "uzima wa milele", njoo kwenye haki, amini tu kuwa Yasu ni mtume wa Mwenyeezi Mungu kama walivyo mitume wengine, huna haja ya kuchakachuwa biblia kupoteza wenzako na kujipoteza mwenyewe kwa ajili ya kutafuta ushindi wa kubishana. Elimika, fanya toba, Shahadia kuwa hapana Mungu apasae kuabudiwa ila mmoja tu na Muhammad ni mtume wake, kama ilivyo kwa Yesu, Ibrahim, Mussa, Daud, Ishaqa na wengine wengi. Kubali usamehewe, bila hivyo huna ujanja.

Ngoja nikupe somo la bure hapa

Umedai kwamba hayo maneno uliyowekewa na mtumishi ISHAMel sio maneno ya Yesu au kwa lugha nyingine hapo hakuzungumzwa Yesu,ngoja tuone maandiko yanasema nini kuhusu Yesu na kuhusu kuwa Alfa na Omega

Ufunuo 1:7
7 Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.

Kwenye huo mstari tunaona Yohana anasema kwamba kuna atakaekuja na kila jicho litamuona na wote waliomchoma na kabila zote za dunia zitaomboleza kwaajili yake

Kwa lugha rahisi kabisa inaeleweka ni nani atakaekuja kwenye mawingi na inaeleweka ni nani aliechomwa,huyu sio mwingine bali ni Yesu Kristo [Danieli 9:26 kwa ushahidi na hii hapa chini kwa uthibitisho zaidi

Mathayo 24:30
30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.

Huo ushahidi unaonesha kabisa huyo anaesemwa kwenye Ufunuo hapo juu ni Yesu Kristo,sasa fungua moyo wako kupata ushahidi utakaoitikisa ngome ya imani yako na kuisambaratisha kwa kishindo cha ukuu wa Mungu mkuu

Ufunuo 1:8
8 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.

Maneno hayo yanaonesha huyo anaezungumza anasema kuna wakati atakuja,sote tunajua kabisa kwamba atakaekuja sio Miwingine ila ni Yesu Kristo,hili ni wazi kwasababu maandoko yameyuthibitishia kwamba Yesu ndie atakaekuja kama hayo maandiko hapo juu yanavyotuonesha,kwa mujibu wa maandiko ni kwamba atakaekuja ni Yesu Kristo siku hiyo ya mwisho pamoja na Jeshi kuu la mbinguni na sio Mungu baba

Ufunuo 19:11-13
11 Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.
12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

Maandiko hayo hapo juu yanatuyonesha kwamba huyo ambae atakuja ni neno la Mungu,ngoja tuitazame Biblia inasema neno la Mungu ni nani

Yohana 1:8
14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

Sote tunajua kwamba aliefanyika mwili ambae ni neno ni Yesu Kristo hivyo hili linaendelea kuthibitisha kwamba ni yule ambae alisemwa kwenye Ufunuo 1 kwamba ni Alfa na Omega

Ufunuo 1:17-18
17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.

Sasa hapo tunaona maneno kutoka kwenye kinywa cha mhusika mwenyewe ambae anasema ni wa kwanza na wa mwisho sawasawa na Alfa na Omega,lakini anaendelea kusema kwamba alikuwa amekufa na sasa yu hai,hakuna yoyote ambae alikuwa amekufa na akawa hai tofauti na Yesu Kristo

Dada yangu Faiza,huna namna ya kukataa haya na yapo wazi kabisa kwa mba Yesu ni Alfa na Omega na ni Mungu mwenyewe [Ufunuo 1:7]

Glory to God Faiza ......

Karibu kwenye furaha ya kweli kwa Yesu Kristo Mungu mkuu aliekuumba wewe,Kahtaan na mimi na wote pia!
 
Last edited by a moderator:
Haki maana yake nini kwa mtazamo wako?
Huruma ni nini kwa mtazamo wako?

Nataka nikuulize swali kutokana na maoni yako wewe kuhusu yote hayo mawili ndio maana nimekuuliza hayo maswali,hivyo basi nijibu ili nikuulize swali!

Sasa we unauliza vitu ambavyo hata maana yake Hujui?
Au unataka kurefusha uzi kwa maswali ya kitoto?
We mtu mzima unauliza nini maana ya haki?
 
Sasa we unauliza vitu ambavyo hata maana yake Hujui?
Au unataka kurefusha uzi kwa maswali ya kitoto?
We mtu mzima unauliza nini maana ya haki?

Mkuu maneno mengi ya nini?

Nimekuambia kwamba nataka nikuulize maswali kutoka kwenye maoni au mtazamo wako kuhusu maana ya hayo maneno,sasa kipi huelewi hapo?

Mbona kama una hofu na jibu lako mkuu?
 
Eiyer ubarikiwe sana mkuu,binafsi nimekusoma na kupata mambo mazuri mengi hapo,na hasa hapo mwisho jinsi Mungu alivyosolve equation ya kumuokoa binadamu bila kutangua adhabu bali kuitimiliza kwa kumtumia Yesu,na ndio maana siku ya kiama wale wasiokubali dhabihu ya mwana wa Adamu (kwa makusudi) wataibeba adhabu wenyewe.Nimekupata uzuri sana,pamenigusa hapo mno.Nina jambo moja la kuuliza humu wana jf tujadili.Hivi wana jf,tunaelewa nini tunaposikia maneno haya matatu:wema,uovu na haki?

Mkuu roho mtakatifu ni mkuu sana anapotufungulia vifungo ambavyo vimetesa wengi sana miaka na miaka ...

Hili ni jambo ambalo limewasumbua wengi na wengi hawalielewi vizuri na ndio maana kuna mikanganyiko sana

Tumpe sifa Yesu Kristo alietupa roho wake kuja kutufumbulia maneno makuu ya Mungu

Kuhusu hayo maneno matatu mkuu yanahitaji tafakuri ndefu ili kuweza kuyaelewa vizuri na sio kukurupuka tu,tunahitaji tutafakari na kumshirikisha Roho Mtakatifu ili tuweze kuyaelewa vyema zaidi ya sasa mkuu

Mkuu nakuomba umwage elimu yako hapa kuhusu hayo namna unavyoyaelewa ili tujifunze pamoja

Tubarikiwe sote kiongozi!
 
Dini ya kweli ni Islamic tu nyingine ni biashara.

Umeingia choo cha kike kijana ....

Hapa hatuhubiri kuhusu dini tunajadili mambo makubwa ya Mungu mkuu aliyoyafanya kwa wanadamu pamoja na kujibu madai ya watu ambao wanadai Mungu anajikinza ....

Kama una cha kuongeza au kuuliza unaweza kuuliza,lakini zingatia kiwe ndani ya mada tafadhali ....

Karibu ....!!
 
Back
Top Bottom