Ni kweli Mungu hana Upendo? Au sisi tu ndio hatumuelewi!?

Ni kweli Mungu hana Upendo? Au sisi tu ndio hatumuelewi!?

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,891
Kuna madai ambayo yameshakuwa yakitolewa hapa na watu mbali mbali na pia nje ya hapa kuna madai ya aina hiyo ambayo yamekuwa yakitolewa na watu mbali mbali wakimkosoa Mungu kwamba hana Upendo, japokuwa wanaodai hivyo wamekuwa hawasemi ni wapi wanaupata upendo na ni kwa namna gani wanaweza hata kuupima upendo, lakini wamekuwa wakijenga hoja yao kwenye huo huo upendo kumpimia Mungu, yaani msingi wa hoja yao ni upendo.

Nimekuwa nikiulizwa mara nyingi sana kuhusu jambo hili na baadhi ya jamaa zangu hapa na nje ya hapa ni kwa namna gani nimekuwa nikiona mtazamo wa hawa ndugu kuhusu hoja yao ya uwepo wa uovu na mabaya kwa ujumla wake hapa duniani, nimekuwa nikijibu hili mara nyingi sana na bahati mbaya wengi wamekuwa hawayaoni majibu hayo, nimeona leo nitengeneza makala hii ili niweze kujibu swali hili kwa kirefu zaidi.

Kwanza tunapaswa kujua kwamba Mungu ni mkuu sana na kamwe hatuwezi kumsaidia kwenye chochote kwa sababu anajitosheleza kabisa kwa sababu ni Mungu, tunachokwenda kufanya hapa ni kuwasaidia hawa wenzetu hawa wanaodai Mungu anajipinga kwa kanuni yake mwenyewe ya Upendo ili waweze kuona mantiki kwenye upendo wa Mungu ili waweze kubadilika na kumkubali Mungu, lakini pia pia tunakwenda kuwasaidia wale wanaohangaika kifkra kuhusu hoja za hawa watu waweze kupata majibu na kuondoka kwenye mahangaiko hayo.

Ndugu zetu hawa wamekuwa wakihoji kama Mungu kweli ana upendo iweje dunia iwe kama ilivyo leo kwa maana ya kuumba dunia ambayo mabaya kama vile magonjwa, vita na mengineyo yanawezekana kutokea, wanadai kwamba upendo wa Mungu usingemuelekeza kuumba dunia ambayo yote hayo yanawezekana, kwa kifupi wanadai kwamba kama Mungu angekuwa na upendo unaodaiwa kuwa anao basi angeumba dunia tofauti sana na hii
Jambo hili limekuwa haliingii kabisa akilini au kwa lugha nyingine wamekuwa hawaelewii kabisa Mungu anaedaiwa kuwa ana upendo halafu aumbe dunia ambayo ubaya unawezekana, wao wanaona kwamba haiwezekani Mungu mwenye upendo aumbe dunia kama hii

Tunakwenda kujibu swali hili tukitumia maana rahisi sana ya Upendo ambayo itakwenda kumsaidia kila mmoja kupata ushahidi wa Upendo mkuu wa Mungu bila kutumia falsafa au maneno magumu ambayo yatasababisha watu wengine wa kawaida kutoelewa,lengo la makala hii ni kuwasaidia watu wengi kuelewa kirahisi suala hili na sio kinyume chake,tutatumia pia mifano michache sana ambayo nayo pia ni rahisi sana kueleweka kwa wasomaji wetu

Tukianza kujibu swali hili ni lazima kwanza tuweke wazi maana au fasiri ya Upendo ambayo tutajengea hoja yetu kwenye makala hii ambayo pia tutalijibu swali hilo la hawa ndugu zetu, maana ambayo tutajengea hoja ambayo itakwenda kujibu swali hili linalohusu au lililojengwa kwenye Upendo ni ile hali ya kumpatia mtu kile ambacho anakihitaji au kukitaka ikiwa na maana pia ya kumpatia mtu stahiki yake bila kumlazimisha, nitatoa mifano michache ambayo ni ya kawaida sana ili sote tuelewe hili.

Mfano wa kwanza

Hebu chukulia kwamba unaishi na mtu pale nyumbani halafu akawa anapenda sana kula wali na maharage kila siku na wewe mwenyeji wake una uwezo huo wa kumpatia chakula hicho ambacho anakipenda sana halafu ukamnyima chakula hicho na kumpa chakula kingine, kwa kitendo hicho cha kumyima chakula anachokipenda utakuwa haujampenda bali kinyume chake,kumnyima mtu kile ambacho anakihitaji au kukitaka ni ishara ya kutomjali na kama humjali basi humpendi

Mfano wa pili

Chukulia kwamba mtu anataka kulala bila kula chakula cha usiku kwasababu tu hataki kula na huko kulala bila kula ndicho kitu ambacho anakitaka,na wewe ukamruhusu kufanya hivyo,kwa kumruhusu kufanya kile ambacho anakipenda au kukihitaji, hapa maana yake ni kwamba unampenda kwa sababu umempa kile ambacho anakitaka bila kujali madhara ya anachokitaka kwa sababu ni mtu mzima na anajua madhara ya kutokula.

Kumbukeni kwamba mifano yote hiyo hapo juu inawahusu watu wenye utimamu wa akili na ni watu wazima kiumri
Kwa maana hiyo ya Upendo ni wazi kwamba kwa nionavyo mimi imeweza kabisa kuenea kwenye kanuni nzima ya upendo ambayo sio kulazimisha chochote
Sasa tuanze na hoja ya uwepo wa mabaya au uwezekano wa uwepo wa mabaya kama kunakinzana na Upendo au haukinzani

Kwanza tuangalie chanzo cha huu ubaya chanzo chake ni kipi,
Ubaya ulikuwepo kwasababu kwanza Mungu aliumba dunia ambayo ubaya unawezekana,swali litakalofuata hapa ni "kwanini kama alikuwa ana upendo aumbe dunia ambayo ubaya unawezekana"? Jibu la swali hili tutaweza kulijibu kwa kutazama maana ya upendo kama tulivyoiona hapo juu,kwanza kabla ya kujibu swali hilo tunapaswa tujue ni nini kinamfanya Mungu awe Mungu maana anakuwa Mungu kwasababu ya sifa zake

Moja kati ya sifa zinazomfanya Mungu awe Mungu ni uwezo wake wa kujua yote,kama anauwezo huo ni wazi kwamba wakati anaumba viumbe vyote alijua kuna viumbe ambavyo vitataka hayo mabaya,kitendo cha kutaka Mungu aumbe dunia ambayo mabaya hayawezekani ni kutaka kumfanya huyu Mungu afanye mambo kinyume na upendo kwasababu tumeshaona kwamba upendo maana yake ni kumpatia kile ambacho mtu au yoyote anachokitaka bila kujali matokeo yake kwasababu ukimnyima kwasababu tu unajua matokeo yake ni kwenda kinyume cha kanuni ya upendo ambayo ni kutokulazimishana

Kwa maana hii ni kwamba uwepo wa ubaya huu ambao tunauona leo hapa duniani ni matokeo ya upendo wa huyu Mungu ambae alijua yote tangu mwanzo

Watu fulani wanaweza kudhani kwamba nakufuru kwa kumjengea Mungu uwezekano wa kuonekana nae anapenda mabaya kwasababu yapo kwa ruhusa yake,hili sio kweli kwasababu tunapaswa tujue kwamba Mungu hakutaka mabaya lakini kwasababu viumbe vyake au baadhi ya viumbe vyake viliutaka hakuwa na namna tofauti na kuvipa kile ambacho vilitaka japokuwa ubaya hauna shirika na Mungu kwasababu Mungu ni mtakatifu kwa asilimia zaidi ya 100
Kuna jambo ambalo tunapenda kuliweka wazi hapa,jambo lenyewe ni kwamba,Mungu hakuumba chochote kwaajili yake bali kwaajili ya viumbe vitakavyokuwepo hapa duniani,ukiangalia kwa mfano Oxygen,hewa hii ipo kwasababu kuna viumbe vitaihitaji ili viishi au viwe na uhai,Mungu yupo kabla ya hewa hiyo kuwepo na yupo kabla ya uwepo wa chochote hivyo tunapaswa kuvitenda vitu hivi na Mungu kwenye suala la uwepo na dhumuni lake,kwa maana hiyo hata ubaya upo sio kwasababu ya Mungu bali kwasababu ya wale wanaouhitaji sawasawa na hewa ya oksijeni ambayo nayo madhumuni yake yanafanana na ya ubaya

Kwa maana hiyo ni kwamba Mungu hakuumba ulimwengu huu na vyote vilivyomo kwaajili yake yeye bali kwaajili ya viumbe vyake ikiwemo na logic,hivyo ni vyema tukajua hilo na kulitenga
Baada ya kujua hili ni wazi kama tunaweza kuwa tumeshajibu swali lote kwa ujumla wake kwasababu tatizo kuu la uwepo wa ubaya tumeona ni zao la upendo mkuu wa Mungu wa kumpatia kila mmoja kile ambacho anahitaji,lakini tofauti na hili ni kwamba sifa nyingine ya Mungu ni kuweza kila kitu,tunatarajia kwamba Mungu huyu aumbe dunia ambayo kwa kiwango fulani dunia hiyo iakisi uwezo huo wa huyu Mungu

Tukiangalia dunia hii ni kwamba inaakisi uwezo wa huyu Mungu kwa kiwango fulani ambapo tunaona kwamba kuna uwezekano wa kutokea mabaya na mema na mengine ambayo ni mengi na yanaakisi uwezo wa Mungu wa kuweza yote,kuhoji hili lisitokee kwenye ulimwengi ambao umeumbwa na anaeweza yote ni kutaka kumuwekea limit kitu ambacho sio halali

Pamoja na kujibu swali hili bado huwa kuna swali lingine ambalo watu huuliza na ambalo huwasumbua baadhi ya waamini uwepo wa Mungu na swali hili ni la kumhusu Shetani,Watu wamekuwa wakihoji sababu ya huyu Mungu kumuacha Shetani au kumuumba wakati alijua kabisa kwamba ataasi kwasababu Mungu anajua yote
Swali hili nalo linaangukia kwenye kundi la swali la kwanza kwasababu kuacha kumuumba shetani kwasababu tu Mungu alijua atakuja kuasi ni kutompenda Shetani kwasababu hiyo ni kumnyima kile ambacho alipaswa akipate kwa uhuru wake mwenyewe,kwa maana hiyo basi ni wazi kwamba Mungu kuacha Shetani aendelee kuwepo ni kumpa kile ambacho anakitaka ambacho kwa maana yetu ni kwamba Mungu alimpenda Shetani
Pamoja na hayo watu wanaweza kujiuliza kwamba kama uwepo wa yote hayo ni matokeo ya upendo,je mbona sasa Shetani na wanadamu ambao walipenda mabaya wanakuja kuadhibiwa baadae?

Swali hili nalo linajibika kirahisi sana kwa kutumia maana ya upendo tuliyonayo hapo

Ili kupata jibu la swali hili ni kwamba tunapaswa kujua kwamba mtu anapokosea na ukamuacha bila kumuadhibu unakuwa umemdhulumu,kwa mujibu wa kanuni ya sheria ambayo hata ulimwengu huu unaongozwa nayo ni kwamba ni lazima unapokosea ni haki yako kuadhibiwa,kuachwa na kwenda hivi hivi tu ni kutokutendewa haki na ni kwenda kinyume na upendo pia,yoyote ambae anakosea ni haki yake kupata adhabu hivyo hawa ambao wanatenda mabaya leo ni haki yao kuadhibiwa na huko ndio kwenda sambamba na upendo kwasababu upendo maana yake ni kumpa kila mmoja stahiki yake na sio kudhulumiana,kutokuadhibiwa ni kudhulumiwa

Jibu la swali hili linaweza kusababisha swali kwamba "Mbona huyu Mungu anasema kwamba ukimuomba msamaha anakusamehe"? "Je Mungu huyu si alisema kwamba yeye ni hakimu wa haki na kila kosa ni lazima liadhibiwe,sasa iweje awaache wengine wakati wamekosa hata kama wamemuomba msamaha"? Lakini pia huyu Mungu anawezaje kuwa wa huruma na hapo hapo awe ni hakimu wa haki"?

Hapo kunaweza kuwa na maswali zaidi ya hayo lakini maswali yote yana jibu moja kuu ambalo ni upendo,nitafafanua,kufikia hapa ngoja tu niseme kweli kwamba,ni lazima niingie kwenye msimamo wa Kikristo kwenye kujibu swali hili kwasababu ndio ninauouna una majibu stahiki kwenye mrundikano wa hayo maswali katika msingi wa Upendo

Ni kweli Mungu aliahidi kuiadhibu kila dhambi bila kujali umeomba msamaha au laa na alijua tu kwamba kumsamehe au kusamehe makosa bila kumuadhibu mkosaji na kosa lenyewe kwa ujumla au dhambi ni kwenda kinyume na kanuni ya sheria ambayo inaagiza kila kosa linapaswa kuadhibiwa na Mungu anasema yeye ni hakimu wa haki,je Mungu anaweza kuwa hakimu wa haki halafu akawa na huruma? Jibu la swali hili ni ndio lakini ni Mungu wa kwenye Biblia tu ndio ambae anaweza kuwa hakimu wa haki na hapo hapo kuwa Mungu wa huruma na hili linamthibitisha kuwa ni Mungu kwasababu hakuna kinachomshinda na anaenea kabisa kwenye sifa yake ya kuweza yote

Kimsingi kila binadamu ana makosa kwasababu ya udhaifu wetu wa kibinadamu hivyo kwa maana hii kila mwanadamu ana hatia mbele za Mungu na ni lazima sote tuhukumiwe kwasababu sote tumekosea,lakini je tutapataje kuwa salama? Je ni kwa namna gani? Jibu ni kwa upendo wa Mungu,Je ni kwa namna gani? Jibu lake ni kwa kupitia Yesu Kristo,usijali nitafafanua hili na hapa nitajibu maswali ya wengi sana waliokuwa wanajiuliza kuhusu hili

Kwanza tunapaswa kujua kwamba sheria tunayoizungumza hapa ambayo hatukupaswa kuivunja na ambayo hata Mungu mwenyewe hajaivunja na hata ivunja na muwekaji wa sheria hiyo ni Mungu mwenyewe,sheria hiyo ni ile ya kutokwenda kinyume na upendo na uhalisia,uhalisia ni pamoja na kutokuvuruga mazingira,maana ya upendo na kanuni yake tumeshajifunza huko juu,kwa maana hiyo basi kukosea kwetu kunatupeleka kwenye kuadhibiwa,makosa yote yataadhibiwa kama sheria inavyosema kwamba kila kosa linastahili adhabu

Kwasababu Mungu alimpenda sana Mwanadamu na aliamua kumuumba kwa mfano wake aliamua kutengeneza mpango wa kumfanya mwanadamu huyu aepuke adhabu ambayo hiyo ambayo kwanza aliichagua yeye mwenyewe na pili ni haki yake kuipata kwasababu ambazo tayari tumeshazisema huko juu,kwasababu Mungu anampenda sana mwanadamu alitaka amuepushe mwanadamu huyu na adhabu hiyo

Kwanza Mungu hakutaka kumuumba kiumbe mwingine kwasababu hakutaka kwenda kinyume na mipango yake,hivyo aliamua kumtengenezea mwanadamu huyu mpango wa kumuepusha na adhabu ambayo aliitaka mwenyewe,lakini kwasababu Mungu ni wa upendo hakutaka kumlazimisha mwanadamu huyu kufuata mpando wake [Mungu] kwasababu kufanya hivyo ni kwenda kinyume na upendo,hivyo kukubaliana na mpango wa Mungu ni hiyari na sio lazima kwasababu Mungu anaupendo wa hali ya juu sana

Kwa kupitia maisha yale yale ambayo binadamu aliyachagua Mungu aliamua kutengeneza mpango kwenye maisha hayo hayo kumuokoa mwanadamu na adhabu ya kuikaidi sheria ambayo ni haki yake,lakini je kama akiiepuka adhabu hii Mungu si atakuwa amevunja sheria yake ya kutokumpa haki yake mwanadamu huyu ambayo ni adhabu kwasababu alikosea? Jibu ni hapana na nitaeleza hili

Baada ya kuona kumsamehe mwanadamu bila mwanadamu huyo kulipa au kugharamia makosa yake ni kuvunja kanuni ya sheria,Mungu aliamua kulipa gharama ile yeye mwenyewe kwa kuamua kuadhibiwa kwasababu ya makosa ya mwanadamu huyo.Mungu aliamua kuja duniani na kuadhibiwa bila kosa lolote na hadi kufa na kumfanya mwanadamu huyu kuwa huru

Je kwa Mungu kuadhibiwa,huyu mwanadamu anapaswa afanye nini ili apate msamaha wa adhabu yake? Au inakuwa hivyo tu automatic? Jibu lake ni hapana bali kuna ambacho Mungu anahitaji mwanadamu huyu akifanye kwasababu kumsamehe hivi hivi bila huyu mwanadamu huyo kujua au kuulizwa kama anahitaji msamaha huo basi Mungu anakuwa hajamtendea haki huyu mwanadamu na atakuwa amevunja kanuni ya upendo,kwa maana hiyo Mungu huyu ameweka mpango kwamba kila mwanadamu ambae atataka asiingie kwenye malipo ya makosa yake yote anapaswa kukubali malipo ya dhambi au makosa yake kwa Mungu mwenyewe kuadhibiwa na kufa kwa niaba yake,hii ina maana kwamba wewe na mimi,kama hatutaki kuja kuwajibika sisi kama sisi kwa makosa yetu wenyewe na tuliyoyachagua kwasababu ya uhuru wa kuchagua basi tukubali leo hii kwamba Mungu alitulipia makosa yetu hayo

Tunachopaswa ni kukiri au kukubali bila shuruti kwamba Mungu alitulipia gharama za malipo ya dhambi zetu kwa kupigwa na sisi tutakuwa huru na adhabu inayotungoja kwasababu ya makosa yetu,kama hutaki huna haja ya kukubali bali wewe endelea tu na maisha yako na utakuja kulipa mwenyewe adhabu yako

Kwa maana hii ni kwamba Mungu ameweza kumuondoa mwanadamu kwenye adhabu ya makosa yake mwenyewe kwa kutoadhibiwa lakini kwa kutumia upendo wake mkuu kwa kuamua kuyabeba yote haya yeye mwenyewe,lakini pia amefanya haya bila kuvunja sheria yake mwenyewe kwa kuadhibu kila kosa kama alivyoahidi na sio kuacha tu.Kwahiyo Mungu ameweza kuwa hakimu wa haki na hapo hapo kuwa Mungu mwenye huruma ya ajabu

Unaweza kujiuliza kwamba huyu Mungu alikujaje duniani na kulipa makosa yetu,jibu lake ni kwamba alikuja na kufahamika kama Yesu Kristo,hivyo unapaswa kukubali kuwa Yesu Kristo ni mwokozi wa maisha yako kwa maana ya kufia dhambi zako wewe

Siku ya mwisho wote tutahukumiwa kama wakosaji na kutakiwa kupelekwa kwenye adhabu yetu lakini yule ambae alitufia atatushika mkono na kutuambia njooni kwangu ninyi mliokubali kafara yangu kwa makosa yenu mfurahi pamoja nami milele na tutapona kwenye adhabu hiyo ya milele
Kwahiyo ndugu yangu Mungu wa kwenye Biblia ndie Mungu kwasababu ni Mungu wa Upendo wa kutisha na ni hakiku wa kweli,karibu kwake

Kupitia yote hayo tumeweza kuona ni kwa namna gani Mungu anakuwa ni Mungu wa upendo wote bila kujikinza na Mungu wetu ni Mungu anaeishi kila siku na hata sasa

Karibuni Mkuu wa chuo , Wickama , Ishmael , Ntuzu , christine ibrahim , Kaunga na wengine wote kwenye mjadala huu ili tukosoane na kujifunza pamoja

Nawakutakia tafakuri njema na mbarikiwa nyote ......!!
 
Makala ndeeeeefu ndani ni blah blah mingi tu!

Mungu gani hana consistance? Babu mzaa babu yangu he know nothing about this God or Jesus ambaye alikuja zaidi ya miaka milioni3 iliopita!

Upendo ni dhana tu mkuu, sababu ukiulizwa upendo ni nini utaleta tafsiri kwa upeo na vile unadhani. Niliwahi kumsoma Padri mfukuwa Karugendo alikua anazungumzia dhana ya upenda na akauliza hivi;

Wakati wa mauaji ya halaiki Rwanda kuna familia mbili zilikimbia kujificha zikiwa mama na watoto wake 6 mmoja wao ni kachanga. Wakiwa wamejificha mara wauaji wakawa wanapita karibu na familia ya kwanza, kachanga kakawa kanalia kwa sauti, mama akajaribu kila namna kanyamaze lakini wapi, akakaziba mdomo akaona kama kanataka kufa akakaachia na wauji wakasikia wakaja kuua familia nzima..

Familia ya pili ikawa kama ya mwanzo lakini mama akamziba mtoto mdomo na akaona anakufa lakini akaona bora afe mtoto wengine watano wabaki, na kweli mtoto alikufa na wauaji hawakuwaona na familia ikapona.

Je ni mama yupi alikua na upendo kwa familia yake?

Karugendo aliuliza hivyo lakini mimi ningeuliza, Je hapa upendo wa Mungu ni upi katika hili?
 
Umesoma nilichoandika?

Nimekusoma na ndio maana nikakuuliza babu mzaa babu yangu hajawahi kusikia wala kujua kama kuna Mungu zaidi ya kuamini alivyoamini, miti, mapango nk.

Je hawa watu wote walioishi hadi kufa bila kujua Mungu toka yesu aje hadi baada ya miaka elfu 3 upendo wa Mungu unawahusu nini?

Upendo ni dhana tu, na ndio maana wengine waliamini nvua isiponyesha basi chukua binti watano mabikira na wachnjwe kafara nvua itanyesha
Au huyo Mungu unaye muamini aliamua kumtoa kafara mwanae ili wewe uokoke....... ni dhana tu!

Ina maana siku ya mwisho Mimi niliyesikia Injili ntahukumiwa tofauti na aliyekufa bila Injili kumfikia, na hukumu ya kizazi cha kabla ya Musa kitahukumiwa tofuti na kizazi cha baada ya Musa na pia kizazi cha kaini kitahukumiwa kwa sheria tofauti..........

Mi nadhani ungejikita na kueleza wajibu wa Mungu ni nini? Kama kweli yupo!

Je upendo wa Mungu unaanzia pale tu Vasco Dagama alipotua let say Bagamoyo na kuwaambia kuna Mungu?
 
Paul S.S

Hujasoma kabisa nilichoandika na kama imesoma hujaelewa kabisa nimeandika makala inayohusu nini..

Madai yako.yako nje ya nilichojibu na kwasababu hiyo ni kwamba hujaelewa japokuwa nimeandika kwa lugha rahisi kabisa na hii ni hatari sana kwa afya ya ubongo wako!

Rudia kusoma hata mara elfu moja huenda ukaelewa!
 
Paul S.S

The Holy Bible makes it conspicuous and crystal clear that while there are might be people in the world who may not have heard of Christ Jesus, simultaneously, none of them can plead ignorance of God their Creator.

"The heavens declare the glory of God; and the firmament sheweth his handiwork" (Psalm 19:1, KJV).

"Ever since the creation of the world his invisible nature, namely, his eternal power and deity, has been clearly perceived in the things that have been made" (Romans 1:20)

Wherefore, the order, regularity and natural laws of the universe are the permanent veracity and impeccable airtight testimony of the Invisible God, the Creator of all things, of which all people are instinctively aware. As a consequence, we find among the most ignorant peoples on the earth a desire to worship God, even though it may be in a perverted form.
 
Last edited by a moderator:
Kiongozi Eiyer, asante sana kwa somo hili tamu ambalo litafungua macho watu wengi sana hapa. Hili in fact ni moja ya masomo niliyo fundisha wakati fulani. Let us teach the Word of God Boldly.
 
Last edited by a moderator:
Upendo ni dhana tu, na ndio maana wengine waliamini nvua isiponyesha basi chukua binti watano mabikira na wachnjwe kafara nvua itanyesha
Au huyo Mungu unaye muamini aliamua kumtoa kafara mwanae ili wewe uokoke....... ni dhana tu
Upendo na kunyesha kwa kumvua kuna uhusiano gani hapa? Jifunze kufikiria kijana. Zaidi ya hapo, wewe unalinganisha "Upendo" na "kuamini".

IN BLUE:
1. Kwanini Mungu alimtuma Mwanae?
2. Kwanini Mwanae ilibidi afe?
3. Kwanini Mwanae na sio Malaika?
4. Kuokoka kutokea nini na au wapi?
5. Kwanini watu wokoke?
 
Kiongozi Eiyer, asante sana kwa somo hili tamu ambalo litafungua macho watu wengi sana hapa. Hili in fact ni moja ya masomo niliyo fundisha wakati fulani. Let us teach the Word of God Boldly.
Kiongozi Mungu anakwenda kujifunua mwenyewe kwa watu wake hivyo watajifunza wenyewe kwa wenyewe kama maandiko yanavyosema kiongozi

Mungu ni wa ajabu sana na upendo wake ni mkuu sana!
 
Last edited by a moderator:
Upendo na kunyesha kwa kumvua kuna uhusiano gani hapa? Jifunze kufikiria kijana. Zaidi ya hapo, wewe unalinganisha "Upendo" na "kuamini".

IN BLUE:
1. Kwanini Mungu alimtuma Mwanae?
2. Kwanini Mwanae ilibidi afe?
3. Kwanini Mwanae na sio Malaika?
4. Kuokoka kutokea nini na au wapi?
5. Kwanini watu wokoke?
Mkuu unauliza maswali magumu sana mkuu

Huyo jamaa sijui kama atakuelewa!
 
Mkuu Eiyer, kwa sasa nina maswali mengi sana na kutokuamini kwingi kuhusu upendo wa Mungu. Ngoja niangalie tu huu mjadala, maana nawaza kuna mambo ambayo tunamtwisha Mungu huku uhalisia ukiwa tofauti.
 
Last edited by a moderator:
Moja kati ya sifa zinazomfanya Mungu awe Mungu ni uwezo wake wa kujua yote,kama anauwezo huo ni wazi kwamba wakati anaumba viumbe vyote alijua kuna viumbe ambavyo vitataka hayo mabaya,kitendo cha kutaka Mungu aumbe dunia ambayo mabaya hayawezekani ni kutaka kumfanya huyu Mungu afanye mambo kinyume na upendo kwasababu tumeshaona kwamba upendo maana yake ni kumpatia kile ambacho mtu au yoyote anachokitaka bila kujali matokeo yake kwasababu ukimnyima kwasababu tu unajua matokeo yake ni kwenda kinyume cha kanuni ya upendo ambayo ni kutokulazimishana

Mkuu hii maana yako ya upendo ya kutokulazimishana ina utata kama nilivyoonesha pale juu. Ukisema kuwa Mungu karuhusu ubaya kutokana na upendo (kutokulazimishana) basi huo utakuwa si upendo. Nasema hivyo kwa sababu upendo na ubaya havikai pamoja (palipo na upendo hakuna ubaya na palipo na ubaya hakuna upendo), hivyo basi maana yako ya upendo inashindwa kukidhi viwango vya upendo.

Kwa maana hii ni kwamba uwepo wa ubaya huu ambao tunauona leo hapa duniani ni matokeo ya upendo wa huyu Mungu ambae alijua yote tangu mwanzo

Hapa naweza kukuuliza, kama Mungu alijua yote tangu mwanzo (kuwa viumbe vyake vitataka ubaya) Je, alishindwa kuumba viumbe visivyotaka ubaya kama kweli ana upendo? (kumbuka yeye ni muweza wa yote)

Watu fulani wanaweza kudhani kwamba nakufuru kwa kumjengea Mungu uwezekano wa kuonekana nae anapenda mabaya kwasababu yapo kwa ruhusa yake,hili sio kweli kwasababu tunapaswa tujue kwamba Mungu hakutaka mabaya lakini kwasababu viumbe vyake au baadhi ya viumbe vyake viliutaka hakuwa na namna tofauti na kuvipa kile ambacho vilitaka japokuwa ubaya hauna shirika na Mungu kwasababu Mungu ni mtakatifu kwa asilimia zaidi ya 100

Kama ubaya hauna shirika na Mungu kwa sababu hapendi ubaya kwa nini aruhusu ubaya? labda unaweza sema ni upendo (kama maana yako ya upendo inavyosema) lakini bado tunaona kuwa upendo na ubaya havikai pamoja.

Hivi unawezaje kutumia ubaya kuonesha upendo? nahitaji ufafanuzi zaidi hapa mkuu

Kwa maana hiyo ni kwamba Mungu hakuumba ulimwengu huu na vyote vilivyomo kwaajili yake
yeye bali kwaajili ya viumbe vyake ikiwemo na logic,hivyo ni vyema tukajua hilo na kulitenga.

Baada ya kujua hili ni wazi kama tunaweza kuwa tumeshajibu swali lote kwa ujumla wake kwasababu tatizo kuu la uwepo wa ubaya tumeona ni zao la upendo mkuu wa Mungu wa kumpatia kila mmoja kile ambacho anahitaji,lakini tofauti na hili ni kwamba sifa nyingine ya Mungu ni kuweza kila kitu,tunatarajia kwamba Mungu huyu aumbe dunia ambayo kwa kiwango fulani dunia hiyo iakisi uwezo huo wa huyu Mungu

Naomba nirudie tena kama anaweza kila kitu, basi pia angeweza kuumba viumbe visivyotaka ubaya ili kuonesha upendo wake. Nashindwa kukuelewa unaposema Mungu ana upendo ndio maana ameruhusu ubaya (wakati ubaya na upendo havikai pamoja ni vitu viwili tofauti kabisa kama moto na maji)

Tukiangalia dunia hii ni kwamba inaakisi uwezo wa huyu Mungu kwa kiwango fulani ambapo tunaona kwamba kuna uwezekano wa kutokea mabaya na mema na mengine ambayo ni mengi na yanaakisi uwezo wa Mungu wa kuweza yote,kuhoji hili lisitokee kwenye ulimwengi ambao umeumbwa na anaeweza yote ni kutaka kumuwekea limit kitu ambacho sio halali

Hapa ni halali kuhoji kwa sababu moja ya sifa za huyu Mungu ni upendo wote, kwa hiyo palipo na upendo wote hatutegemei kuona mabaya, ukiona mabaya lazima uhoji kwa nini kuna mabaya ilhali mtengenezaji (Mungu) ana upendo wote na hana chembe ya ubaya.

Swali hili nalo linaangukia kwenye kundi la swali la kwanza kwasababu kuacha kumuumba shetani kwasababu tu Mungu alijua atakuja kuasi ni kutompenda Shetani kwasababu hiyo ni kumnyima kile ambacho alipaswa akipate kwa uhuru wake mwenyewe

Na vipi kuhusu hao wanadamu ambao shetani anakuja kuwapotosha, Je Mungu hakuwapenda? kama aliwapenda na wanadamu kwa nini amruhusu shetani aje kuwapotosha?

Ili kupata jibu la swali hili ni kwamba tunapaswa kujua kwamba mtu anapokosea na ukamuacha bila kumuadhibu unakuwa umemdhulumu,kwa mujibu wa kanuni ya sheria ambayo hata ulimwengu huu unaongozwa nayo ni kwamba ni lazima unapokosea ni haki yako kuadhibiwa, kuachwa na kwenda hivi hivi tu ni kutokutendewa haki na ni kwenda kinyume na upendo pia, yoyote ambae anakosea ni haki yake kupata adhabu hivyo hawa ambao wanatenda mabaya leo ni haki yao kuadhibiwa na huko ndio kwenda sambamba na upendo kwasababu upendo maana yake ni kumpa kila mmoja stahiki yake na sio kudhulumiana, kutokuadhibiwa ni kudhulumiwa

Sasa mkuu kukosea kunatoka wapi wakati mwanzoni umesema upendo ni kutokumlazimisha mtu, nanukuu maelezo yako

"Tukianza kujibu swali hili ni lazima kwanza tuweke wazi maana au fasiri ya Upendo ambayo tutajengea hoja yetu kwenye makala hii ambayo pia tutalijibu swali hilo la hawa ndugu zetu, maana ambayo tutajengea hoja ambayo itakwenda kujibu swali hili linalohusu au lililojengwa kwenye Upendo ni ile hali ya kumpatia mtu kile ambacho anakihitaji au kukitaka ikiwa na maana pia ya kumpatia mtu stahiki yake bila kumlazimisha"

Unapomuadhibu mtu maana yake ulimlazimisha mtu afanye kitu fulani hakufanya kile kitu ndo maana kuna adhabu, kama kweli hakuna kulazimishana basi adhabu haikutakiwa kuwepo.

Pia, unaposema humlazimishi mtu kufanya au kutofanya kitu fulani halafu ukaweka adhabu,mimi naona hapo hakuna upendo (kama maana yako ya upendo inavyosema) hapa chini.

"Kwa maana hiyo ya Upendo ni wazi kwamba kwa nionavyo mimi imeweza kabisa kuenea kwenye kanuni nzima ya upendo ambayo sio kulazimisha chochote"

Ni hayo tu.
 
Mkuu Eiyer, kwa sasa nina maswali mengi sana na kutokuamini kwingi kuhusu upendo wa Mungu. Ngoja niangalie tu huu mjadala, maana nawaza kuna mambo ambayo tunamtwisha Mungu huku uhalisia ukiwa tofauti.
Mkuu tupo hapa kwaajili ya kujifunza,kama una mahali umeona unaweza kusahihisha unakaribishwa sana mkuu na hili ndilo lengo kuu

Karibu tuelimishane mkuu!
 
Last edited by a moderator:

Mkuu hii maana yako ya upendo ya kutokulazimishana ina utata kama nilivyoonesha pale juu. Ukisema kuwa Mungu karuhusu ubaya kutokana na upendo (kutokulazimishana) basi huo utakuwa si upendo. Nasema hivyo kwa sababu upendo na ubaya havikai pamoja (palipo na upendo hakuna ubaya na palipo na ubaya hakuna upendo), hivyo basi maana yako ya upendo inashindwa kukidhi viwango vya upendo.

Mkuu nilichomaanisha sicho hiki ulichoandika hapa

Unapomnunulia rafiki yako chakula ambacho wewe hukopendi utakuea unskipenda chakula kile kwasababu tu umekinunua?

Hapa naweza kukuuliza, kama Mungu alijua yote tangu mwanzo (kuwa viumbe vyake vitataka ubaya) Je, alishindwa kuumba viumbe visivyotaka ubaya kama kweli ana upendo? (kumbuka yeye ni muweza wa yote)

Hivi umesoma haya unayoyanukuu au umenukuu bila kusoma?

Hiki unachouliza mbona nimeshakijibu kwenye mada?

Kama ubaya hauna shirika na Mungu kwa sababu hapendi ubaya kwa nini aruhusu ubaya? labda unaweza sema ni upendo (kama maana yako ya upendo inavyosema) lakini bado tunaona kuwa upendo na ubaya havikai pamoja.

Hivi unawezaje kutumia ubaya kuonesha upendo? nahitaji ufafanuzi zaidi hapa mkuu

Naomba nirudie tena kama anaweza kila kitu, basi pia angeweza kuumba viumbe visivyotaka ubaya ili kuonesha upendo wake. Nashindwa kukuelewa unaposema Mungu ana upendo ndio maana ameruhusu ubaya (wakati ubaya na upendo havikai pamoja ni vitu viwili tofauti kabisa kama moto na maji)

Najua uwezo wako wa kufikiri kwa sehemu kwasababu tulishajadiliana na wewe kwenye baadhi ya thread lakini sitaki kuamini kwamba bado uko vile vile tu

Nimekuuliza kwamba,wewe unapoamua kufanya jambo kwa niaba ya mwingine na jamvo lile wewe hupendi kulifanya,kitendo cha wewe kulifanya kinakufanya uwe unalipenda jambo lile?

Mungu ni upendo tu na hana ubaya lakini haimaanishi kwamba hawezi jambo lolote,sasa kwanini huelewi kwamba alifanya hayo kwa niaba ya viumbe vyake?

Hapa ni halali kuhoji kwa sababu moja ya sifa za huyu Mungu ni upendo wote, kwa hiyo palipo na upendo wote hatutegemei kuona mabaya, ukiona mabaya lazima uhoji kwa nini kuna mabaya ilhali mtengenezaji (Mungu) ana upendo wote na hana chembe ya ubaya.

Nimeshakueleza kwamba Mungu anaweza yote kwanini hilo lishindikane?

Halafu hili nimeshalitolea maelezo kwenye mada kwamba unapotaka Mungu aumbe dunia ambayo kuna mambo hayawezekaniki hii inamaana ya kumtaka Mungu asiwe wa upendo na nimeeleza hilo kwa kirefu,mkuu mbona huelewi wakati nimelitolea maelezo?

Na vipi kuhusu hao wanadamu ambao shetani anakuja kuwapotosha, Je Mungu hakuwapenda? kama aliwapenda na wanadamu kwa nini amruhusu shetani aje kuwapotosha?

Wewe hujasoma kabisa nilichiandika na kujadiliana na watu kama wewe ni kupoteza muda tu

Soma kwanza halafu uje uulize

Sasa mkuu kukosea kunatoka wapi wakati mwanzoni umesema upendo ni kutokumlazimisha mtu, nanukuu maelezo yako

"
Tukianza kujibu swali hili ni lazima kwanza tuweke wazi maana au fasiri ya Upendo ambayo
tutajengea hoja yetu kwenye makala hii ambayo pia tutalijibu swali hilo la hawa ndugu
zetu, maana ambayo tutajengea hoja ambayo itakwenda kujibu swali hili linalohusu au
lililojengwa kwenye Upendo ni ile hali ya kumpatia mtu kile ambacho anakihitaji au kukitaka
ikiwa na maana pia ya kumpatia mtu stahiki yake bila kumlazimisha"

Unapomuadhibu mtu maana yake ulimlazimisha mtu afanye kitu fulani hakufanya kile kitu ndo maana kuna adhabu, kama kweli hakuna kulazimishana basi adhabu haikutakiwa kuwepo.

Pia, unaposema humlazimishi mtu kufanya au kutofanya kitu fulani halafu ukaweka adhabu,mimi naona hapo hakuna upendo (kama maana yako ya upendo inavyosema) hapa chini.

"Kwa maana hiyo ya Upendo ni wazi kwamba kwa nionavyo mimi imeweza kabisa kuenea
kwenye kanuni nzima ya upendo ambayo sio kulazimisha chochote
"

Ni hayo tu.
Kuna mtu anaadhibiwa bila kuwa na uhuru wa kuchagua mwanzoni?

Sasa hivi nani anakilazimisha usiibe?
Lakini ukiiba hutapelekwa lupango?

Nyie watu mnachosha sana!
 
Mkuu nilichomaanisha sicho hiki ulichoandika hapa

Unapomnunulia rafiki yako chakula ambacho wewe hukopendi utakuea unskipenda chakula kile kwasababu tu umekinunua?

Haimaniishi na wewe unakipena nakubali, Labda nikuulize, tuchukulie hicho chakula sikipendi kwa sababu kina sumu, sasa kama ninampenda rafiki yangu siwezi kumnunulia hicho chakula. Ni sawa na suala zima la ubaya Mungu anajua madhara ya ubaya kama ana upendo kama usemavyo asingerurhusu ubaya mkuu.

Siwezi kumpa rafiki yangu chakula chenye sumu wakati najua kitamdhuru, huo si upendo kaka.

Hivi umesoma haya unayoyanukuu au umenukuu bila kusoma?

Hiki unachouliza mbona nimeshakijibu kwenye mada?

Nimesoma na ndio maana nilikuwa naquote halafu ndio nauliza, haya ndio yalikuwa maelezo yako

"Kwa maana hii ni kwamba uwepo wa ubaya huu ambao tunauona leo hapa duniani ni matokeo ya upendo wa huyu Mungu ambae alijua yote tangu mwanzo"

Narudia tena swali langu,

Hapa naweza kukuuliza, kama Mungu alijua yote tangu mwanzo (kuwa viumbe vyake vitataka ubaya) Je, alishindwa kuumba viumbe visivyotaka ubaya kama kweli ana upendo? (kumbuka yeye ni muweza wa yote)

Hujajibu hili swali, kama umejibu naomba unukuu maelezo uweke hapa labda sikuyaona.

Najua uwezo wako wa kufikiri kwa sehemu kwasababu tulishajadiliana na wewe kwenye baadhi ya thread lakini sitaki kuamini kwamba bado uko vile vile tu

Nimekuuliza kwamba,wewe unapoamua kufanya jambo kwa niaba ya mwingine na jamvo lile wewe hupendi kulifanya,kitendo cha wewe kulifanya kinakufanya uwe unalipenda jambo lile?

Labda hukunielewa, sikusema kwamba kitendo cha Mungu kuruhusu ubaya anapenda ubaya. Ila ninachosema ni kwamba huwezi kusema Mungu anaonesha upendo kwa kuruhusu ubaya. Hata kama anafanya kwa ajili ya mwanadamu, rejea mf wangu wa chakula chenye sumu. Kumruhusu/kumpa mtu chakula chenye sumu wakati uanajua kina sumu huo si upendo.

Mungu ni upendo tu na hana ubaya lakini haimaanishi kwamba hawezi jambo lolote,sasa kwanini huelewi kwamba alifanya hayo kwa niaba ya viumbe vyake?

Kwa hiyo kwa sababu tu alifanya kwa ajili ya viumbe vyake hata kama jambo ni baya na lina madhara maana yake ni upendo?

Unapoamaua kumpa rafiki yako chakula chenye sumu kwa sababu ametaka huo ni upendo?

Nimeshakueleza kwamba Mungu anaweza yote kwanini hilo lishindikane? Halafu hili nimeshalitolea maelezo kwenye mada kwamba unapotaka Mungu aumbe dunia ambayo kuna mambo hayawezekaniki hii inamaana ya kumtaka Mungu asiwe wa upendo na nimeeleza hilo kwa kirefu,mkuu mbona huelewi wakati nimelitolea maelezo?

Hapo unakuwa unajipinga mwenyewe mkuu, kutokana na sifa yake ya upendo wote basi hatutegemei kuona mabaya, mabaya yanapowezekana basi tayari sifa ya upendo inapungua.

Pia katika sifa yake ya kuweza yote bado angeweza umba ulimwengu usio na mabaya

Wewe hujasoma kabisa nilichiandika na kujadiliana na watu kama wewe ni kupoteza muda tu

Soma kwanza halafu uje uulize

Nilijua utasema hivi, na ndio maana nimequote na kuuliza labda hujaelewa maswali yangu kutokana na mindset yako. niliqoute haya maelezo

Swali hili nalo linaangukia kwenye kundi la swali la kwanza kwasababu kuacha kumuumba shetani kwasababu tu Mungu alijua atakuja kuasi ni kutompenda Shetani kwasababu hiyo ni kumnyima kile ambacho alipaswa akipate kwa uhuru wake mwenyewe

kisha nikauliza hivi

Na vipi kuhusu hao wanadamu ambao shetani anakuja kuwapotosha, Je Mungu hakuwapenda? kama aliwapenda na wanadamu kwa nini amruhusu shetani aje kuwapotosha?

Kuna mtu anaadhibiwa bila kuwa na uhuru wa kuchagua mwanzoni?

Sasa hivi nani anakilazimisha usiibe?
Lakini ukiiba hutapelekwa lupango?

Unapotoa adhabu kwa kitendo cha wizi, maana yake unawataka watu wasiibe, ni sawa na kuwalazimisha wasiibe ungekuewa hulazimishi usingetoa adhabu. Unapoweka adhabu maana yake usifanye kitu fulani ukifanya unaadhibiwa hapo hakuna uhuru.

Natoa mf, watu wafanyao mapenzi ya jinsia moja wanadai haki zao sehemu nyingi duniani, unajua kwa nini? Ni kwa sababu baadhi ya sehemu ukifanya hivyo vitendo vichafu unafungwa (adhabu), sasa unaweza kuniambia kuwa hawa watu wana uhuru? kama wana uhuru hicho wanachodai ni nini?

Sisupport mapenzi ya jinsia moja nimetoa mfano tu.

Nyie watu mnachosha sana!

Mkuu, unapoamua kuleta mada sehemu kama hii ni lazima ukubali mawazo na mitizamo tuofauti kwa sababu kuna watu tofauti. Unapoanza kusema maneno kama hayo na mada umeleta mwenyewe sijui unategemea nini. Kama unaona michango ya wengine inakuchosha basi uwe specific kwa watu uanaotaka wachangie mada yako.
 
Back
Top Bottom