KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 32,529
- 76,691
Kila nikifatilia historia juu ya majengo makubwa na yenye stori lukuki pale Egypt, yani pyramids napata mashaka ya nini kinachoendelea.
Hususani kumekuwa na stori tofauti tofauti lakini bado hazijategua kitendawili!, vilevile uwepo wake hapa Africa na nikiambiwa kuwa waafrika ndio waasisi wa majengo yale ndo kabisa naona tafrani.
Hii ni kutokana na umaridadi wa majengo yale inaonyesha kabisa alieyatengeneza alikuwa ni fundi haswa!, sasa kama ni sisi waafrika mbona hatuna majibu na utaalamu huo uliishia wapi..??
Kwa uchache nitagusia nadharia mbalimbali ambazo zinadai kuwa watu ama jamii fulani ndio waliratibu majengo yale!..
Annunaki.
Baadhi ya watu huamini kuwa majengo yale yalitengenezwa na viumbe waitwao annunaki ambapo kwa wakati huo walikuwa na utaalamu wa aina yake!, haiishii hapo tu wapo pia wanaosema hao annunaki ndio waliotuumba sisi binadamu!, lakini nadharia hii bado haina majibu ya uhakika/uthibitisho!. so bado ni fumbo...!
Wayahudi/Israel
Hii inatoka kwenye biblia ya kwamba waisrael walichukuliwa kwenda uhamishoni hapo misri wakati wa utawala wa mafarao na walifanyika kuwa watumwa, na walitumika kujenga hayo ma pyramid wakati huo wa utumwa wao!, utata unakuja haifahamiki walitumia utaalamu upi maana kwa kipindi hicho ni ngumu kwa mwanadamu Kutengeneza majengo kama yale kutokana na teknolojia ya wakati huo ni ngumu!, kupandikiza yale majabali mengi kiasi kile na yenye uzito mkubwa huo ufanisi binadamu wa wakati huo uliutolea wapi..?
Isitoshe wataalum walipima nakugundua pyramid za pale misri zapata kuwepo miaka 4500 iliyopita!.. vilevile hao wa misri wao walikuwa wanadai waliyatengeneza kwaajili yakuzikia wafalme na malkia zao!, ama waweza sema royal family.
Lakini kwa mujibu wa watafiti hawajawahi kupata mwili wowote kwenye pyramids!, miili imekuwa ikipatikana maeneo ya mbali na yalipo hayo ma pyramid!.
Hata hivyo haingii akilini mtu kujenga mijengo kama ile ati kwaajili tu ya kuzika mafalao na malkia zao!, mh! bado inatia shaka!.
Viumbe toka anga za mbali ama Aliens.
Wengine huamini kuwa majengo yale yaliratibiwa na viumbe wenye uwezo mkubwa wa kiteknolojia maarufu kama aliens, na lengo la wao kujenga hayo madude ilikuwa ni kwaajili ya Kutengeneza umeme ama nguvu ambayo wenyewe ndo wanajua ilikuwa kwaajili ya nini!!.
Nadharia hii ya yale madude kuwa sehemu ya power implant inachagizwa zaidi na nguli wa maswala ya umeme nikola tesla!, ambae alisema kuwa haswa hiyo ndo ilikuwa kazi ya yale madude, pia wapo wataalum wengine pia wamejaribu kugusia hilo na kutokana na ramani za yale madude kule ndani wanaafiki kuwa nikola yupo sahihi!, kizungumkuti ni haifahamiki ilikuwa kwa lengo gani na haijathibitika!.
Jamii ama kizazi ambacho kimeshapotea!.
madai ya baadhi ya watu husema pyramids zilijengwa na jamii ambayo ilikuwa na uwezo huo na hapa katikati kukatokea janga hiyo jamii ikapotea!, hivyo ndio maana tunakosa majibu!..😅
Nadharia juu ya nani ni mjenzi wa zile pyramid zipo nyingi nimegusia chache ambazo nazo hazijatoa majibu!, sasa hoja yangu ni tutakuwa kwenye giza la kukosa majibu ya hakika mpaka lini..?
Naona kama hatupo serious! madude makubwa kiasi kile na hatujui yameratibiwa na nani!, hapohapo ma injinia wanakili hata teknolojia ya sasa haiwezi kujenga yale madude!!!! WTF!.
Wanakiri pia yale mawe yaliyotengenezewa pyramid yaonyesha yalikuwa yanakatwa kwa ustadi mkubwa halafu ndo yanajengewa pyramid!, wakati huohuo mawe yale yalikuwa yanapatikana umbali mrefu toka zilipo pyramid!, hivyo maswali ni mengi maana kwa wakati huo walisafirisha na nini kwenye kuyabeba!.
Pia utata mwengine ni ile perfection ya kuyabebanisha yale mawe!, unaambiwa nafasi kati ya jiwe moja na lengine ni ndogo sana kiasi kwamba hata kucha ya binadamu haipiti!..😅
Maoni yangu.
Inaweza ikawa kweli tukawa hatujui, ila pia wapo wanaojua na wameamua watunze siri kwa minajili ya kwao wenyewe!, ijapo bado tafiti zinaendelea kufanyika mpaka leo.
Ndugu msomaji nini maoni yako juu ya hili, unafikiri tutaendelea kukaa kwenye hichi kitendawili mpaka lini?