Ni kweli wanaojenga Ikulu huwa wanauliwa wakishamaliza kujenga?

Ni kweli wanaojenga Ikulu huwa wanauliwa wakishamaliza kujenga?

yaani story ziko hivyo kwamba.

anayekimbiza mwenge lazima afe hakai siku nyingia

anayeweka msalaba pale juu ya mnara wa kanisa nayeye huwa anakufa tena kwa kuanguka vibaya,labda wawe wamerekebisha tayari.

na hawa wajenzi wa ikulu nao.
sema dunia ndogo sana hii sio ya kubisha kila kitu au kukataa kila kitu.
Sio kubishana, ila kwa vile umesema dunia ni ndogo basi tulipaswa kuwa tumethibitisha hizi stori kama sio porojo.

Hebu tumsikie mbobezi Stress Challenger.
 
Kuna mshikaji namfahamu amepiga rangi majengo ya Ikulu ya Chamwino na yupo anadunda mpaka leo.
 
Capture.PNG
 
yaani story ziko hivyo kwamba.

anayekimbiza mwenge lazima afe hakai siku nyingia

anayeweka msalaba pale juu ya mnara wa kanisa nayeye huwa anakufa tena kwa kuanguka vibaya,labda wawe wamerekebisha tayari.

na hawa wajenzi wa ikulu nao.
sema dunia ndogo sana hii sio ya kubisha kila kitu au kukataa kila kitu.
Jordan Lugimbana alikuwa kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2001 alilala Liparamba, miaka ya karibuni aliwahi kuwa mkuu wa wilaya moja Dar es salaam bado Yuko hai japo Kwasasa simsikii, Hizo stori za vijiweni tuu.
 
BM X6,
Hayo uliyoyasikia ,binafsi sijayasikia lakini ni kama njama zinazotokea katika tamthilia kwenye sinema.

Ningekushauri uwaulize wanahudhuri wa Jamii Intelligence.

...tupo kijiweni, tunasubiri kwa shauku majibu kede bin kede kuhusu njama hizo.

Walahi, hili jambo limefanya ijumaa yangu kuwa nzuri. Ahsante
 
Kuna story nishawahi kuzisikia kuhusu Ikulu, kama zina ukweli wowote naomba kujuzwa hapa

1. Ikulu Kuna njia ya chini kwa chini mpaka Makao makuu ya jeshi

2. Wote wanaohusika kwenye ujenzi wa ikulu wakimaliza wote wanauawa wanazikwa getini pale ikulu

We ushaisikia ipi? na je zina ukweli?View attachment 2256011
Sidhani tunayo teknoloji ya kutengeneza tunnel ndefu Kama hiyo.(Yaani toka Ikulu mpaka Ngome).
Wakijenga tunnel hawatakwambia,kwa sababu,hiyo itakuwa siri.
Hiyo hadithi uliyosikia ni hadithi ya Taj Mahal.
 
Kwamba kuna pango kutoka ikulu mpaka lugalo sio rahisi maana ni hatari kwa usalama...
Kwamba kuna handaki ikulu ni sahihi, nimesoma kitabu cha African Mutiny wameeleza hilo na kwamba hata Kambona aliwahi kulitumia kumuokoa mwalimu wakati fulani ila hilo handaki haliendi mbali ni baharini japo kunaweza kuwa na mabadiliko kulingana na marekebisho kadhaa (rejea dr Mwinyi bungeni akizungumzia ukarabati wa ikulu 2014)

Kuhusu wajenzi wa Ikulu kuuliwa nimesikia mara kwa mara. Ila kwa hakika kabisa naweza sema si Ikulu ya Mzizima magogoni hata mara moja. Ukitaka kufahamu hili jiulize ile ikulu ilijengwa lini? Utakosa jibu maana haijajengwa ile kama ikulu... akina mohamed said wanahadithia kuwa ile ni nyumba ya bwana tajiri kabla ya kufanywa kuwa boma la mjerumani... intact haijawah kujengwa kama ikulu zaid ya kushuhudia marekebisho tuu ya mara kwa mara hapo ndo waga najiuliza waliuawa lini.

Kuhusu watu kufukiwa ikulu, sio posta aisee hiyo inashadidiwa na majengo kama Belt el Ajabu pamoja na Ikulu ya Unguja anapo lala dr Mwinyi ambapo kila nguzo moja alisimikwa mtumwa mmoja.

Hivyo ndivyo ninavyo fahamu mimi
 
Back
Top Bottom