Ni kweli Wanawake wana akili kuliko wanaume wengi. Kwa sababu zifuatazo…

Mkuu umeandika maelezo mengi lakini msingi wa hoja yako una tatizo moja kubwa: unachanganya “aina ya uwezo” na “ubora wa akili”.

Kwa mtizamo wangu na hii ni kisayansi, hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa wanawake wana akili kuliko wanaume au kinyume chake. Tafiti nyingi zinaonyesha wastani wa IQ ni karibu sawa kabisa kati ya jinsia zote mbili.

Tofauti zilizopo ni kwenye maeneo maalum:
  • wanawake mara nyingi wanafanya vizuri kwenye lugha na kumbukumbu
  • wanaume wanafanya vizuri kwenye uwezo wa kuona vitu kwa nafasi (spatial) na baadhi ya problem solving

Hii haimaanishi mmoja ni bora kuliko mwingine, bali kila upande una strengths zake.

Pia hoja zako zinaonekana ku-generalize sana. Unachukua mifano ya kijamii au uzoefu binafsi kisha unatoa hitimisho la jumla kuhusu jinsia nzima — hiyo si njia sahihi ya kujenga hoja.

Ukweli ni kwamba akili ya mtu inategemea mambo mengi zaidi ya jinsia:
mazingira, elimu, malezi, na juhudi binafsi.

Kwa hiyo badala ya kusema wanawake wana akili kuliko wanaume, hoja sahihi zaidi ni:
binadamu wote wana uwezo wa akili unaokaribiana, ila wanatofautiana kwa namna wanavyoutumia.
 
Mfano ni vigumu sana kwa wanawake wanachukiana kufanya kazi pamoja hata kama muungano wao utaleta faida kubwa kwao, ila wanaume wanachukiana wanaweza fanya kazi vizuri tu kama kuna manufaa makubwa wanayapata kutoka kwenye muungano wao, kwenye hzo mifano ni nani anayetumia logic hapo.

Wanawake wanajua wapo vizuri kwenye kumsoma mtu na wanajua wanaume wana changamoto kwenye hyo area ila ana tegemea usome dalili na viashiria kwenye hisia zake ili kujua ana hisi nini au anataka nini na ukishindwa anakasirika na pengine kuvunja uhusiano sio kwamba hakupendi ila anaona humjali, kuna logic gani hapo
 
Huwezi shauri mtu arushe ndege kwa uangalifu kama si rubani.
Ndio maana yake..ishi nao kwa akili maana yake unakumbushwa wewe mwenye Akili ukae na mhusika kwa akili...otherwise wangetafuta jambo jingine kulieleza.
 

Umeongea vizuri Sana.
Lakini sio kweli wanawake hawawezi kufanya Kazi pamoja. Wanaweza
Tatizo la wanawake kutofanya kazi pamoja ni maslahi tuu.

Pili, wanawake hawapendi kushushiwa thamani na wanawake wenzao. Dharau.
Bora adharaulike na mwanaume lakini sio mwanamke mwenzake.

Wanaume hawaoni shida kudharauliwa na wanaume wenzao ilimradi wanapata chochote kitu.

Tatu, kutokana na akili walizonazo wanawake wao husoma patterns za dharau na kujua hatma ya maslahi Yao mapema kabla hata mwanaume hajafanya hivyo
 

Umejibu kitaalam Sana. Kisayansi.
Lakini kwa vile sayansi haijathibitisha haimaanishi Jambo Hilo halipo.

Ni kwamba bado wanasayansi hawajapata mbinu bora ya kuthibitisha dai husika.

So sayansi ni muhimu lakini tukumbuke pia sayansi inayoshindwa kuthibitisha Jambo fulani Leo haimaanishi Jambo Hilo haliwezi kuthibitishwa na sayansi ya miaka ijayo.

Msingi wa Sayansi ni Theories zilizopo kwenye falsafa
 
Wanawake hawaeleweki. Sema nimeshtuka wengi wao hawapendi kubembelezwa sana.
Ukiwabembeleza wanakwenda kinyume ukiwapeleka kijeshijeshi wao ndio wanakubembeleza wewe maisha yanakuwa mteremko.
Watu wasiojua hudhani mwanamke wakimbembeleza sana ndio itaongeza asilimia za kummiliki kumbe ni kinyume chake.
 
Ngoja kuna kitu nikuulize hapa.
Kuna mwanamke wangu aliwahi kunikimbia kwa kuona nimesimamishwa kazi lakini akaunti yangu ilikuwa imejaa maokoto ya kutosha ambayo nina uwezo wa kutumia mwaka mzima bila kufanya kazi ila sikumwambia ilikuwa siri yangu.
Unadhani hapo alikuwa na akili au alitumia akili kukimbia?
 
 

Attachments

  • 8df50d6716613eaba400282532d230c2.mp4
    15.5 MB
mtu akiwa tu mmbea au msengenyaji me namuona hana akili na tafiti zinaonyesha wao ndo wambea sana wakiwa 10 akiondoka mmoja tu tayari ashaanza kusemwa akiondoka mwingine tena anasemwa..japo na wanaume pia wambea ila wso wamezidi.so in my conclusion sifa ya kwanza ya mwanamke ambaye ana akili asiwe na marafiki wengi wa kike wa kufanya nao umbea
 
Hakuna watu wambea kuliko mwanaume na mwanamke wanaopendana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…