Ni lini Rais Samia ataanza ziara kusikiliza kero za Wananchi?

Yaan ni wa ovyoo kabisa mkuu
 
Ikiwa Mh. Rais anafanya kazi za kusikiliza kero za wananchi kwa kufanya ziara basi hakina maana ya kuwa na serikali za mitaa na tawala za mikoa!! Ukiona Rais anafanya mambo ya aina hiyo kuna maana mbili
1. Hawaamini au wasaidizi wake hawaaminiki.
2. Hakuna uwajibikaji kwa waliopewa majukumu ya kuhudumia wananchi au viatu vinawapwaya....
 
Ni nini kazi ya DC, DAS, mwenyekiti wa mtaa mwenyekiti wa kijiji?

Badala ya kutaka kufanya kila kitu mwache mama ajenge mifumo.

Enzi za one man show zimepita, mifumo ijengwe.
 
Kazi ya DC na mwenyekiti wa kijiji ni nini kama mnataka mama atatue kila kitu yeye?
 
Msilazimishe mama awe JPM.There is only one JPM, Mnataka mama azurure na magali ya serikali na misafara kuwasikiliza wanchi? Ataweza nchi hii ni kubwa. Tusimpangie mama cha kufanya.
 
Swadakta, 100%.
 

Akisema warumi ataonekana ana mdomo... hata msiba haujaisha vizur huyo kashaanza kukimbilia nchi za watu Sijui anatafuta nini

Magu alikua ana mapungufu yake ila ulikua unaona kabisa he was dedicated in serving the people of Tanzania, alikua na uchungu na nchi yake, ila huyu mama yupo kimaslahi, yani tutalia na kusaga meno had miaka minne iishe
 
Mwinyi hakuwasubiri tu Ikulu, aliwafuata pia ktk ziara zake. Hatuhitaji ushabiki usio na manufaa au kujikomba. Mama si malaika, dhamana kapewa na watanzania, tuna haki ya kumkosoa anapokosea, hata yeye karuhusu kukoselewa. Hizi siasa za upambe Tanzania ndo zimeharibu nchi hii.
Swala si awamu ya 6 hata ingekuwa ya kumi. Tunataka kuona kinachotendeka kinaifanya nchi yetu ipige hatua. Si porojo na maneno yenye sukari, wakati nchi inabaki pale pale. Tunataka kuona kazi inafanyika. Kero mbalimbali zinaisha. Miradi inasonga mbele.
Swala la kusema najuaje labda atawakaribisha Ikulu, yeye mwenyewe alitamka hataki kusikia kero za wananchi zinamfikia. Hukumu itakuja 2025 na msishangae upinzani ukachukua nchi kama kweli watapata mtu sahihi, kwa wakati sahihi.
Wapiga kula wengi wa nchi hii ni watu wa hali ya chini. Ili ufanikiwe teka mioyo yao.
 
Zama za giza,kiki na propaganda zimepita.

Rais ana deal na mambo makubwa ya Nchi.
Huko kwenu kuna kero gani inayomhitai Rais ambayo Watendaji wameshindwa kuitatua?

Yaani Rais aende kuzurura mitaani kuzungumzia stand na vyoo? Mko serious nyie?
 
Kwani hayo mahindi yameruhusiwa, utaratibu bado ule ule wa vikwazo, ukitaka kuingiza mahindi Kenya lazima yapimwe pimwe kwanza, tuna Rais dhaifu na naive kupita wakati wote...
Kupima ni sahihi, Ss tuna TBS, Huwa tunapima bidhaa zao. Ni taratibu tu za kuingiza na kutoa bidhaa kwenye mipaka ya nchi. Usipopima ni hatari, adui anaweza ingiza sumu majirani mkaanza gombana yeye anawaangalia tu.
 
Zama za giza,kiki na propaganda zimepita.

Rais ana deal na mambo makubwa ya Nchi.
Huko kwenu kuna kero gani inayomhitai Rais ambayo Watendaji wameshindwa kuitatua?

Yaani Rais aende kuzurura mitaani kuzungumzia stand na vyoo? Mko serious nyie?
Eti!!
 
Nini kimekwama huko kwako kwa yeye kusafiri?
 
Huko uliko mkuu hamna mkuu wa wilaya? Mkuu wa mkoa? Mbunge? N.k tutamchosha mama!
 
Zama za giza,kiki na propaganda zimepita.

Rais ana deal na mambo makubwa ya Nchi.
Huko kwenu kuna kero gani inayomhitai Rais ambayo Watendaji wameshindwa kuitatua?

Yaani Rais aende kuzurura mitaani kuzungumzia stand na vyoo? Mko serious nyie?
Mambo gani makubwa unayodhani zaid ya kuwatumikia wananchi. Kuingia mikataba ya Gesi au? Rais ni Rais wa watu si Rais wakusafiri bila kuona tija ya safari zake. So unataka azurure mitaa ya Karen, Mombasa, Kasarani na si mitaa ya nchi yake! Ha ha ha!
 
Ule ulikuwa ni upumbavu wa Mwendazake tu na kutaka masifa matatizo ya wananchi hayatatuliwi namna ile. Hata akina Nabii Musa walioishi miaka 4,000 kabla ya Kristu walishauriwa wasitatue matatizo kwa namna ile.

Soma Kutoka 18: 19-22
Musa. Alipokuwa kiongozi wa Israeli, ghafla alikuwa mtu mwenye shughuli nyingi. Watu wa Mungu walihesabiwa mamilioni na maisha ya Musa yalikuwa magumu kwani alihukumu na kuwahudumia watu tangu asubuhi hadi usiku.

Kuangalia yote haya, mkwewe wa Musa Jethro aliingilia kati na kumuonya Musa kwamba atajifunga mwenyewe ikiwa haitafanya mabadiliko. "Wewe ni mchungaji, Musa, na unahitaji kujifunga na Mungu. Wape wengine kazi za ugomvi na ushauri nasaha. Kisha uwe peke yako na Mungu, utafute uwepo wake, pata akili yake, na upokee neno lake. Hii inapaswa kuwa kipaumbele j”

Hiyo ndiyo maana ya delegation, organisation structure, division of labour, hierarchy and people management
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…