warumi
R I P
- May 6, 2013
- 16,218
- 18,440
Kwangu mimi binafsi (In my Humble Opinion) ingawa simpangii mtu nitashukuru na nitaona ni matumizi mazuri ya Kodi zetu kama Kiongozi Mkuu atatumia huo muda kutatua na kuunganisha wote na kuwaongoza kutatua Kero kuliko kutumia muda mwingi kujifanya anasikiliza (wakati popote pale anaweza kuzisikia na anazisikia) kwa kujifanya ndio mtendaji mkuu wakati akiondoka hapo hakuna kinachofanyika...
Yaani kufanya afanye kazi hata behind the scenes sio kuonekana anafanya kazi (kupiga siasa) wakati hakuna kinachofanyika zaidi ya propaganda.... (Atumie muda mwingi na hao wasaidizi wake kwa kuwafuatilia na kuwahoji na kwa kufanya mikutano lukuki ya tumepanga nini / tumefanya nini / tumekosea wapi / turekebishe wapi / tuanze kutenda tena...., (Continuous Improvement)
Usiseme kujifanya, marehemu ki ukweli tuliona alikua ana nia thabiti ya kusikiliza kero za wananchi wake popote walipo, he did it na moyo wake wote, he was passionate in serving his people , alikua na uchungu na nchi yake Ndio maana alikua hapendi ujinga, alikemea maovu na uzembe . Ni kweli marehemu alikua na mapungufu yake, ila mazuri yake anayo, tena mengi tu.
Msiba wake ni uthibitisho tosha kuwa marehemu alikua ni kipenzi cha watu , wananchi wake aliowatumikia walimzika kwa heshima mno, watu walilia kwa uchungu kwa sababu wanajua hawawezi kupata raisi kama magufuli na Ndio ukweli
Kwa sasa hivi hawawezi kutudanganya tena, tunajua tofauti ya kiongozi bora na bora kiongozi.
Mama asipojifunza mazuri kutoka kwa mtangulizi wake, atapata shida sana, moja wapo ikiwa ni hiyo y kusikiliza kero za wananchi