Ni maadili gani aliyobomoa Zuchu katika shoo yake mpaka wamfungie kufanya mziki Zanzibar pamoja na kulipa faini?

Ni maadili gani aliyobomoa Zuchu katika shoo yake mpaka wamfungie kufanya mziki Zanzibar pamoja na kulipa faini?

Wakuu,

Watu tuache unafiki na ushabiki kwenye jambo hili. Zuchu kaharibu maadili gani kwenye shoo yake ya Zanzibar, ametukana tusi gani?

Kipande alichoimba alisema hata ".... hata mumpe mku..." akaendelea zake kupiga shoo. Hiyo "Mku" ndio tusi? Tusi gani? Kuna anayeweza kuthibitisha kuwamba "Mku" ni tusi? Akisema alimaanisha mkungu wa ndizi? Mkutano mkuu, Mkuu wa mkoa?

Zuchu akiamua kupiga hili mapema sana anashinda, hakuna grounds za kumfungia kwamba kavunja maadili kwa tafsiri ambayo inakamilishwa na watazamaji, yaani chombo chenyewe ndio knakisia kwamba hapa itakuwa alikwa alimaanisha hivi. Hata wewe unayesoma hapa, nikikuuliza Zuchu katukana nini kaenda vipi kinyume na maadili kutokana na alichotamka hutakuwa na jibu, utabaki kuzunguka zunguka lakini hautakuwa na jibu!

Baraza la Sanaa Zanzibar hapa limekurupuka na hata wakienda Mahakamani Zuchu mapema sana anawalaza na watatakiwa kumlipa faini, BASATA na yenyewe ikijichanganya itakuwa mule mule tu, sema wasanii wa bongo ndio hivyo, hawajui haki zao, mwisho wa siku wanapelekeshwa tu ovyo ovyo ka ng'ombe.

Uje kubishana kwa hoja, mihemko iache nyumbani kwako.

Sasa mbona aliomba msamaha kabla ya kufungiwa, ina maana anajua mwenyewe alichokusudia. Lakini ww shabiki andazi unacomplain utasema ndio meneja wake.
 
Mkiendelea kuwaachia na ujinga wao kuna siku wataenda kuwekana mbele ya jukwaa na huyo mwehu mwenzie.

Mtu una wazazi wako hai kabisa unatamkaje hivyo mbele za watu? Mi sielewi mtu unawezaje kukosa adabu kiasi hicho hata kama ndio usanii.
Zuchu kamuiga mamake matusi
 
Basata wataogopa japo SMZ wapo sahihi kumpiga pin.......hivi vitoto vinaimba matusi tupu ila vinasurvive kwasababu wanasiasa wakubwa wanavitumia
Screenshot_20240305-232546.png
 
Kisu kimepenya kwenye mfupa 😂😂
Kijana wa sinza ndio mambo yenu mnavaa hereni na vibukta bila kusahau kupaka lips shine halafu ni mwendo kinyume na maumbile hivyo lazima utetee…….
Wanakushikisha ukuta ndio maana umejaa chuki na wivu
 
Kuna lugha ya ishara.Aliposema mku akaonyesha kwa ishara anamaanisha nini.
Angeimba mku halafu akaonyesha ishara ya mkufu watu wangetafsiri alichomaanisha.
Alionyesha wazi alichomaanisha na ndio sababu ameomba radhi.
Ila kuomba radhi siyo justification ya kuwa umekubali kosa mkuu. Mkuu kuna ile unaona bora yaishe basi unaomba radhi badala ya kuendelea kugombana wakati wajua umeshika wapi na adui kashika wapi
 
Back
Top Bottom