Kabisa mzee, huwa nafeel guilty kabisaa.
Burudai ninayoipata nafsini mwangu baada ya kusaidia haielezeki kwa kweli nahisi inazidiwa kidogo na pale ninapompa mama yangu au kumpa zawadi mke wangu nae akaifurahia.
Nina majirani zangu hali tete, nikibahatisha kahela, nikinunua kitoweo cha kutosha basi hiyo nitaigawa na kwao, huyu mmoja mwanae ni mgonjwa gonjwa anateseka sana, plan yangu kwa sasa nikipata vichenji nimkatie bima tu(mungu anisaidie)
Kuna kipindi nilitamani nianzishe utaratibu wa kuwasaidia utaratibu wa kuwachangia bima ya afya watoto yatima, kuna mambo yakanikwamisha na kunirudisha nyuma(mwenye uwezo afanye hili jambo, niko tayari kumpa mipango yangu)