Bora wewe unajibiwa asante baba, wengine ni wanabisha hawajakosea na wako sahihi.. 🤣😂
Ukishinda hoja utaambiwa basi yaishe.
Nina mwanangu ana majanga, wakati mwingine unaona hata aibu kumtembelea nyumbani kwake.
Mkewe ana kaujeri kakimya kimya, ukimuona ni mpole lakini ni mjeuri kinoooma, mwanangu anapata tabu saana, kuna muda anafikiria kumuacha.
Mie wangu ni kutaka kujua kila kitu in details, ananiboa saana, chochote kile atataka in details, hata apige simu mtu akuongeleshe atakuuliza nani huyo, ndio yupi. 😂🤣 Unamuliza utamjuaje sasa, hata nikikutajia fulani huwezi kumjua 😂, sijui ni kupenda kuongea na simu au vipi
Hata umpelekee zawadi atataka kujua yoote, kama umekopa, umemnunulia na sh ngapi, unajiuliza we unataka kujua nini, yaani ni shughuli pevu 😂
Kingine anapenda mnoo kuongea na simu, bora muwe karibu hii inasaidia, akiwa mbali anapiga simu ataongea mpaka stori zaitaisha, mie mvivu kubonga na FONI naishia kuweka loudspeaker tu.
Sometimes hana stori, anakupihia anakwambia mwanao anakuita, sasa mtoto Mwenyewe ndio bado hajatimiza mwaka vizuri, kuongea haongei, unajua tu hapa nimemisiwa.
Mengine madogo madogo, yanachangiwa na maisha yangu ya awali.
Elewa neno AWALI. lizingatie vema.