Ni mapungufu gani ya mkeo/mumeo umeamua kuishi nayo?

Na lile la kale kajamaa kumnyandua mbona hujasema au hilo hauishi nalo
 
Tunaishi nayo na miaka inasogea.

Hata ukenda leo kumuuliza baba yako yanayozungumzwa humu mama yako baadhi alikuwa anamfanyia na hakumuacha,kuwa mwanandoa ni kuwa na akili timamu huwezi kuwa kichwa panzi ukasema utaishi kwenye ndoa,never!!!
Sio kweli mkuu ,kuna vichwa panzi wengi kwenye ndoa kuliko unavyofikiri.
 
Wangu jamani uwii! Ukikosea analisema jambo kama lilivyo bila hata chembe ya kupepesa macho.

Which is good, but kuna mambo huwa anakosea nashindwa kumface kumchana nampotezea tu nikiamini anajua anachofanya, ila ikija upande wangu nachanwa chanwa bila kuremba kitu. Sasa naona why mimi nambebea madhaifu yake yeye hanibebei? Is it fair?

Ukisafiri ukiwa unarudi lazima alazimishe kuja kukupokea, yaani hii ni lazima sio ombi, tatizo ni kwamba hata umwambie nusu saa kabla hujafika, au lisaa kabisa lazima achelewe, yaani lazima achelewe. Kwahiyo mimi kukaa airport/Au stendi dakika 10/15/20 ni kitu cha kawaida tu. Nilishamshauri hili suala la kunipokea aliache, ntapanda tax, bajaji etc ila hakubali ng'oo ni bora umuue! Nishanuna sana, nishazira sana ila haisaidii. Mwaka wa 9 huu.

Anyways.... Naishi humo!
 
Hayo sio mapungufu brother, ni tabia ya mtu.

Alaf anakupenda huyo.
 
Najiona mimi kabisa. Hiyo ndio weakness yangu kubwa kukubali nimekosea ni mtihani. Naweza hamisha story lakini baba naye mtata hata ukihamisha story ataileta tu mpaka useme sorry
 
Kuachaniza vitu ndani,kila mkitaka kitu fulani lazima ianze operation tafuta,iwe kadi ya benki ,kadi ya mtoto ya hospitali,funguo na chochote kile mtatafuta tu.
Hii nimecheka sana aisee😅😅😅

Huyu ni mama yangu kabisa, huwaga sio mpangaji wa vitu, baba ndo alikuwa anatutunzia vitu tulipokuwa wadogo, huwaga yuko very systematic kutunza vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya shule, kadi za hospitali, ukimuuliza baba anakuletea ndani ya dakika moja, ukimpa mama kitu chako utakikuta uvunguni.
 
Kataaa ndoa wakikukuta utaomba pooh
 
Jamani mwanaume anakupenda hivo hadi anataka akupokee waubavu wake kipendacho roho ila unaona kero?

Wewe ndo kama mpenzi wangu, kila nikimwambia nataka nije kukupokea anakataa, huwaga inaniuma sema simwambiagi, kwann mnafanya hivo lakini?
 
Kumbe hayo ni madhaifu ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…