Ni mashine gani ambayo ukiipata itafungua njia zako za kibiashara?

Hili liliwahi kutukuta kwenye mashine ya kutengeneza ice cream au mabonge ya barafu,aisee ilikuwa inakamua umeme hatari,kwa siku inaweza kula umeme wa 10,000
 
Huu uzi bila kumpata kicheche wa kutupenyezea mizigo bandarini kwa nusu bei tutateseka Sana maana hapo alibaba au kwenye xampuni za China kitu kinakuwa ni laki kikufika bandarini ndo unachanganyikiwa kwa kodi
Sio kweli mashine hazitozwi kodi nyingi kama bidhaa zingine.
Kwasababu zinachukuliwa kama zina boost ukuaji wa viwanda.

Mashine hazitozwi import duty, zinatozwa railway levy, na vat na gharama zingine kwa uchache.

Niliwahi import machine fulani kutoka US na huo ndio mchanganuo niliopigiana hesabu na watu wa custom japo ilikua kwa ndege.

Kwa bandarini nadhani mawakala wanachukua pia percentage yao kwenye clearance.

Kwa wale wanaotumia cargo forwarders wakina gnm nadhani wanao gharama zao za usafiri zina cover process za clearance za mzigo wako pindi unapofika.

Kuna kitu cha muhimu sana
Kuna mdau Covax hapo juu kazungumzia, usikimbilie kununua mashine pasipo kujua upatikanaji wa spares na urahisi wa matengenezo, mashine zote zinahitaji maintenance mana vipuri huchoka na kuhitaji replacement, sasa ukienda kichwa kichwa umeagiza mashine biashara imechachamaa wateja wamekolea mashine inapata shida utajua hujui.

Cha mwisho mashine nyingi za mchina ni bei ya chini kwasababu wanaunda kwa kutumia vifaa hafifu, hii haina maana hawana vifaa imara isipokua wanapunguza gharama za uzalishaji ili waipate hiyo ela yako ndogo.

Mashine nzuri zipo ila ni gharama.
 
Hapo wire hizo zinazalishwa hapa nchini au zinatoka nje?
Hapo ndo kwenye changamoto hapa ndani ni shida sana kuzipata na kama unavyojua watz wengi wanapenda wafanye wao tu hawapendi wengine waingie huko waliko
 
Nahitaji mashine ya kuchakata ngozi za mbuzi na za ng'ombe.

Nitaipata wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…