Ni maswali gani unahisi hayajibiki duniani?

Ni maswali gani unahisi hayajibiki duniani?

1.Nani ni mmiliki wa logo ya copy right?
2.Ukiwa mwezini ukiangalia juu unaona nini?

Swali lako number mbili, jibu ni panda juu ya ghorofa halafu angalia juu, utakachokiona ndio hicho kinaonekana kwa alie enda mwezini
 
Mungu aliwaumba Adamu na Eva ambao wakawazaa Kaini na Abeli.

Mbona watu waliendelea kuzaliana wakati kaini na abel walikuwa wanaume?

Basi ina maana kulikuwa na watu wengine zaidi ya kaini na abeli walokuwepo

Mbona hatujaambiwa watoto wengine?
Lakini eva aliendelea kuzaa wa jinsia nyingine
 
Ni ishara gani itakayotofautisha kati ya siku na siku na utatambuaje kwa mfano kuwa leo ni Alhamisi?
 
Mungu aliupenda ulimwengu hadi akamtuma mwanae wa pekee, kama alitupenda sana kwanini hakuzuia dhambi duniani?

ALIZUIA ILA HATUKUA WATII KUFUATA MAELEKEZO, LAKINI BADO HADI SASA ANAIZUIA DHAMBI NDIO MAANA AKALIWEKA NENO LAKE. (NENO LA MUNGU)

NA NINI CHA KUFANYA ILI KUMPENDEZA, NA NINI TUSIFANYE (ambacho ndio dhambi sasa)
 
Mfano
1. Kuna nini kinaendelea baada ya kifo.?
2. Mwenyezi Mungu alitokea wapi?
3. Je kuna Mungu?
4. Chanzo cha dunia ni nini?
5. Nani alianzisha muda?
6. Dunia na heavenly bodies nyingine zinawezaje kuelea angani?
7. Nini chanzo cha gravitational force?
 
Mtoto wa nyoka ni nyoka mbona Mtoto wa kuku anaanzia yai
 
Back
Top Bottom