" Ili CHADEMA tuwaamini kuwa AGENDA yao ya Kudai Katiba Mpya ina Mashiko na wana Hoja ya Msingi hebu wao kama Chama waanze Kwanza kuonyesha kuwa wanaheshimu Katiba ndani ya Chama chao ambapo kuna uvunjifu mkubwa tu wa Katiba " Pascal Mayalla
Nukuu hii nimeitoa baada ya Kumsikia na Kumtizama jana Usiku Star Tv akiwa Mgeni rasmi kwa Dar es Salaam katika Kipindi kilichokuwa Kinasimamiwa na Mtozi Aloyce Nyanda.
Mkuu
Krav Maga, kwanza asante kwa hoja hii.
Hoja iliyokuwa mezani jana ni hitaji la Katiba mpya, jee tumshinikize Mama Samia, lazima utupe katiba mpya au tumpe muda zaidi.
Hoja zangu ni hitaji la katiba mpya ni hitaji genuine, tena nikasema katiba mpya Tanzania sio kuwa inahitajika leo, katiba mpya ilihitajika toka juzi, jana na leo. Nikasema, kwa miaka 30, Tanzania imekuwa chini ya mfumo wa chama kimoja, na katiba iliyopo ya mwaka 1977, ni katiba ya chama kimoja, hivyo tulipoanzisha mfumo wa vyama vingi, tulipaswa tubadili katiba na kuwa na katiba ya vyama vingi. Kilichofanyika ni katiba ile ile ya chama kimoja, ikaongezewa kiraka cha vyama vingi, lakini mfumo ni ule ule wa chama kimoja, hivyo bila mabadiliko ya katiba, CCM itatawala Tanzania milele.
Suala la Katiba lililetwa kwa hisani tuu ya uungwana wa JK, halikuwemo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM.
Nikaishauri Chadema, badala ya kususa na kupiga kelele tuu, wajifunze tabia ya kufuata sheria, taratibu na kanuni katika kudai haki zao, na kwa kuanzia, charity begins at home, kwa Chadema kuanza kufuata katiba yake katika timua timua za wanachama wao.
Kwa msiofahamu utaratibu wa Chadema kutimua wanachama wake, karibuni mitaa hii
Wanabodi, Hili ni bandiko la wito kwa Chadema na ushauri wa bure, kiwatendee haki wanachama wake, ili ifikapo Octoba 2015, Watanzania waiaminie Chadema kuwa itawatendea haki Watanzania. Kitendo cha kutowatendea haki wanachama wake, kutapelekea wanachama hao kunyanyasika na kulia machozi ya ndani...
Baada ya Chadema kufuata katiba yao ndipo watu organize Watanzania kudai katiba mpya. Nikawasisitiza, kwa vile hoja ya katiba ilikuwepo kwenye ilani ya uchaguzi ya 2015- 2020, lakini very unfortunately katiba haikuwa ni kipaumbele cha JPM na hawakumshinikiza JPM, na sasa hoja ya katiba mpya haipo tena kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 - 2025, then wasimshinikize Samia kuendelea na mchakato, bali wajenge hoja zenye mashiko, halafu Samia akiingia huruma na kufanya uungwana kama wa Kikwete, ndipo Tanzania itapata katiba mpya.
Kitendo cha Chadema kususa, sio tuu ni wastage of time, but Chadema is bed ridden on its deathbed, if it won't change its strategies, it is going to die and soon it will be 6ft under!.
P