Ni matumaini yangu wana CHADEMA wote si tu mmemsikia bali mmemuelewa vyema tu Kada wa CCM Pascal Mayalla

Ni matumaini yangu wana CHADEMA wote si tu mmemsikia bali mmemuelewa vyema tu Kada wa CCM Pascal Mayalla

Nashukuru leo Paschal pale Star TV amekiri kwamba alipata misukosuko sn baada ya kuuliza swali la katiba pale ikulu, pia vyombo vya habari vilibanwa vibaya sn wakati wa dikteta. Hapo nimemwelewa mengine haya tuachane nayo maana katiba mpya siyo ajili ya CHADEMA pekee ni ya watanzania wote.
Mayala.ni mganga njaa tu, mbona hajatoa kipengele kilichovunjwa?

Mayala ni kada wa CCM na aligombea ubunge kura za maoni! Ndio yale yale ya wana Ccm kuipa promo Chadema.

Adili na mambo ya chama chake
 
Mkuu katiba mpya siyo ajili ya CHADEMA ni hitaji la watanzania wote, tusiona na vyama, viongozi wa dini, wasiokuwa na dini na hata CCM kwenyewe, uliona mtu mmoja alikuwa MUNGU mtu mpaka alikuwa anaingilia uhuru wa watu eti kuvaa barakao mbele yake ni kosa, lakini MUNGU siyo mpumbavu akatuondolea ile balaa japo bado kuna masalia kama Ndugai, Mwigulu, Olesabaya, Hapi, Mnyeti, Makonda n.K
 
Mayala.ni mganga njaa tu, mbona hajatoa kipengele kilichovunjwa?

Mayala ni kada wa CCM na aligombea ubunge kura za maoni! Ndio yale yale ya wana Ccm kuipa promo Chadema.

Adili na mambo ya chama chake
Paschal inabidi kabla ya 2018 alikuwa ni mwandishi wa habari ukimuona kwenye TV hata kama una kula inabidi uache kwanza kula umsikilize, sijui shetani gani amekuja kumpitia hapo katikati amebaki Doto Bulendu pekee sijui ndiyo anaitwa hivyo
 
Mtanisamehe labda uelewa wangu ni mdogo.
Nilichoelewa kwamba CHADEMA kama chama cha siasa basi kipo chini ya msimamizi wa vyama vya siasa ambaye amepewa mamlaka ya kuweza kushugulikia matatizo yote ya vyama vya siasa na hata kukifuta chama.
Hoja yangu ni kwamba kama CHADEMA wanakiuka Katiba yao je huyo msimamizi wa vyama vya kisiasa alichukua au amechukua hatua gani mpaka leo hii.
Kushindwa kwa msajili wa vyama vya kisiasa kuwachukulia hatua CHADEMA inaonyesha wazi kuwa Katiba yetu ya nchi ambayo imempa mamlaka msajili kusimamia vyama vya siasa haipo sawa inaitaji marekebisho Mana hakuna mtu au chama chochote ambacho kipo juu ya Katiba.
Pili, hauwezi kufananisha Katiba ya nchi na Katiba ya chama, Yani ni kusema kwamba kwa vile Katiba ya CHADEMA haijafika basi katiba ya nchi hisibadilishe, au udhaifu wa Katiba ya CHADEMA madhara yake ni kwa wanachama wake ila udhaifu wa Katiba ya nchi madhara yake ni kwa wananchi wote.
Nahisi kuwa hapo hoja ya uyo bro ilibidi iwe je tunaitaji mabadiliko ya Katiba au la. Na sio kutumia madhaifu ya chama kuficha hoja ya msingi.
Uko vizuri hadi umemshinda aliyeleta mada naona atagundua kuwa alileta utopolo hapa
 
Nashukuru leo Paschal pale Star TV amekiri kwamba alipata misukosuko sn baada ya kuuliza swali la katiba pale ikulu, pia vyombo vya habari vilibanwa vibaya sn wakati wa dikteta. Hapo nimemwelewa mengine haya tuachane nayo maana katiba mpya siyo ajili ya CHADEMA pekee ni ya watanzania wote.
Mayala.ni mganga njaa tu, mbona hajatoa kipengele kilichovunjwa?

Mayala ni kada wa CCM na aligombea ubunge kura za maoni! Ndio yale yale ya wana Ccm kuipa promo Chadema.

Adili na mambo ya chama chake
 
Mayala.ni mganga njaa tu, mbona hajatoa kipengele kilichovunjwa?

Mayala ni kada wa CCM
Adili na mambo ya chama chake
Karibu mitaa hii usome vipengele.

P
 
Theme kubwa nnayoiona kwenye hili andiko ni udhaifu wa chadema kama vile ndio chama pekee pembeni ya ccm mpaka chadema iwe kishikizi cha hoja ya katiba mpya kwamba chadema isipofanya au isipofanyiwa jambo fulani hoja ya katiba mpya haina mashiko au haifai. Niseme tu kuwa pamoja na kujitanabaisha kama muumini wa katiba mpya na faida zake, andiko hili limekuwa la kujiegemeza kwenye siasa za chama kimoja kama taasisi.

Imesemwa mahali fulani au labda halijasemwa kuwa Habari ya katiba mpya sio jambo la chama fulani kama taasisi. Sio hata jambo la mtu mmoja mmoja hili hata mwandishi afikiri kuwa mapungufu ya taasisi fulani ndio yanaathiri umuhimu wa kuwepo katiba mpya au utekelezaji wake au ufanisi wake kwa sababu ya lolote lililo dhaifu ndani ya taasisi fulani. Ninasema andiko hili ni la kibinafsi kisiasa zaidi kwa uandishi wake wa kuilaumu na kuyalaumu mapungufu chadema pekee. Hata kama vyama vya siasa navyo ni kishikizi basi ungeainisha mapungufu ya vyama vingine vya siasa, viwe tawala au vinginevyo yanavyochangia kutopatikana katiba mpya. Nasikia huyu mwandishi ni mwandishi nguli.

Ningetegemea katika andiko hili angetushirikisha maoni yake kuhusu madhaifu ya ADC, ya TLP, ya CUF au ya UDP. Lakini ningetegemea kuwa kwa kiasi kikubwa angetoa maoni kuhusu mapungufu ya chama tawala ambayo ndicho mfaidika mkubwa wa katiba hii iliyopo. Namna hiyo mleta andiko angekuwa 'balanced' kama walivyo waandishi nguli.

Anaposema JK alisukumwa na hisani kuwezesha mchakato wa kupata katiba mpya mpaka hapo ulipofikia anakuwavna mtazamo hafifu wa kudhani ilikuwa hisani. Jambo la katiba lilikuwa na bado ni jambo linalomhusu JK kama mtanzania na alipolileta hakuwa anapanga kuyainua au kuyaboresha mazingira na maisha ya vyama vya upinzani na si kufanya kile watanzania 60M+ wanachokihitaji, yeye akiwamo. Watanzania wanahitaji katiba mpya sio kwa hisani. Wanaihitaji kwa sababu ndio inayowafaa na ni haki yao.

Leo unawaona watanzania kama wanaweza kuhitaji kitu na namna pekee ya kujipatia ni kwa kupitia hisani ya mtu binafsi. Lakini unafikiri hali hiyo itadumu milele. Mambo si hukoma? Sasa kwanini yasikome wakati watanzania wote wamefanikiwa. Huyu mwandishi angetoa maoni kuhusu uchoyo wa chama tawala zaidi kutowezesha mchakato wa kupata katiba mpya eti kwa sababu matokeo ya muda mfupi ni chenyewe kuendelea kutawala.

Kama mtawala hicho chama kina mapungufu kuliko kizio kingine chochote.
Mwandishi ameilaumu sana cdm lakini Kuna mtu amewahi kufikiri kuwa mapungufu ya cdm ni matokeo ya katiba isiyoainisha huendeshwa unaofaa wa vyama vya siasa? Unaweza kudhani katiba ya chama tawala ni bora sana lakini ukionyeshwa matobo iliyonayo hutaamini unachokiona.

Ni dhaifu sana. Sasa nani ajuaye kuwa matobo hayo yanasababishwa na udhaifu wa katiba uliopo. Kwa nini sasa mtu ailaumu chadema kwa kutopatikana kwa katiba.
Mwenye uwezo amshauri mwandishi nguli kuwa bora kuliko anavyosemwa maana najitahidi kuuona unguli nashindwa
 
Mkuu Babati, mimi nimeizungumzia sana katiba ya Chadema, angalia tarehe za mabandiko haya

P
Kwani hitaji la katiba mpya ni la wananchi au Chadema
 
Kwani hitaji la katiba mpya ni la wananchi au Chadema
Katiba ni ya wananchi na hitaji la katiba mpya ni hitaji la wananchi, ila ili kuipata hiyo katiba mpya ni mchakato wa kujenga hoja zenye nguvu ya hoja na sio hoja za nguvu.

Chadema wameamua kutumia hoja za nguvu, kupiga kelele na kususa ili kushinikiza, down the drain, they will go...6ft under!.
P
 
Msajili wa vyama anasemaje kwani. Mbona hakifuti chama au adhabu au karipio kama uliyoyasema hapa Yana ukweli.
 
Katiba ni ya wananchi na hitaji la katiba mpya ni hitaji la wananchi, ila ili kuipata hiyo katiba mpya ni mchakato wa kujenga hoja zenye nguvu ya hoja na sio hoja za nguvu.

Chadema wameamua kutumia hoja za nguvu, kupiga kelele na kususa ili kushinikiza, down the drain, they will go...6ft under!.
P
Sawa kabisa katiba ni yetu wananchi na nihitaji letu wananchi, sasa ni wapi tupate majukwaa sahihi ya kudai katiba mpya
 
Back
Top Bottom