Ni matumaini yangu wana CHADEMA wote si tu mmemsikia bali mmemuelewa vyema tu Kada wa CCM Pascal Mayalla

Ni matumaini yangu wana CHADEMA wote si tu mmemsikia bali mmemuelewa vyema tu Kada wa CCM Pascal Mayalla

Tatizo la Pascal na wengine wengini kutokuona mbali. Kwanza ya yote, katiba tunayoiongolea ni katiba ya nchi sio ya CHADEMA. Tumeona mapungufu ya hii katiba kipindi cha Magufuli na jinsi alivyoitumia kuminya haki za watu.

CHADEMA kutofuata katiba yao hakuwazuii Watanzania kupata katiba mpya; zaidi ya yote, CHADEMA ni chama kidogo na kichanga ukifananisha na taifa la Tanzania.
 
Mkuu Babati, mimi nimeizungumzia sana katiba ya Chadema, angalia tarehe za mabandiko haya

P
Kwani huko ccm timua timua hakunaga?
 
" Ili CHADEMA tuwaamini kuwa AGENDA yao ya Kudai Katiba Mpya ina Mashiko na wana Hoja ya Msingi hebu wao kama Chama waanze Kwanza kuonyesha kuwa wanaheshimu Katiba ndani ya Chama chao ambapo kuna uvunjifu mkubwa tu wa Katiba " Pascal Mayalla

Nukuu hii nimeitoa baada ya Kumsikia na Kumtizama jana Usiku Star Tv akiwa Mgeni rasmi kwa Dar es Salaam katika Kipindi kilichokuwa Kinasimamiwa na Mtozi Aloyce Nyanda.

Najua hapa JamiiForums kuna wana CHADEMA wengi tu na wale walio Neutral kama Mimi Krav Maga hivyo kwa pamoja ama tutaweza Kukubaliana nae au Kumpinga kwa Hoja.

Na wakati mnamjibu mwana CCM Pascal Mayalla kumbukeni kuwa huyu ni Msomi wa Fani nyingi nchini Tanzania za Habari na Sheria, Mjasiriamali mkubwa, Mjuaji wa Mambo mengi nchini Tanzania, Member Mkongwe JamiiForums, Mwanasiasa mwenye Mafanikio na Mtu mwenye Network kubwa sana ya Viongozi ( Watawala ) wa Tanzania hii na huenda hata katika Teuzi zijazo za DC au DED safari hii akawemo.
Umemlisha maneno,Pasco hawaezi kuwa kilaza nmna huyo.
Kuwa suala la katiba sio la CHADEMA suala la katiba Ni la watanzania wore hata Pasco na Wana CCM wenye akili.
Hayo sio maneno ya Pasco nimjuaye.
 
Tatizo la Pascal na wengine wengini kutokuona mbali. Kwanza ya yote, katiba tunayoiongolea ni katiba ya nchi sio ya CHADEMA. Tumeona mapungufu ya hii katiba kipindi cha Magufuli na jinsi alivyoitumia kuminya haki za watu.

CHADEMA kutofuata katiba yao hakuwazuii Watanzania kupata katiba mpya; zaidi ya yote, CHADEMA ni chama kidogo na kichanga ukifananisha na taifa la Tanzania.
Hili ndio tatizo kubwa la chadema kujihisi kwamba mna akili,maono na ujuvi wa kila kitu hata kama hamnazo
 
Takataka
IMG-20210530-WA0013.jpg
 
Back
Top Bottom