Mkuu mi nipo chama hiki huku,chama hicho hakinihusuKwa sababu unahusu katiba ya chadema maandishi hayaonekani, si unaona mlivo sasa
Kwani huko ccm timua timua hakunaga?Mkuu Babati, mimi nimeizungumzia sana katiba ya Chadema, angalia tarehe za mabandiko haya
Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa
Wanabodi, Uendeshaji wa vyama vya siasa nchini, unaongozwa na sheria, taratibu na kanuni. Ikithibitika pasipo shaka kuwa chama fulani, kinakiuka sheria, taratibu na kanuni, kinapaswa kuwajibishwa, kuadhibiwa hata kufutwa, kutegemeana na tuhuma halisi!. Miongoni mwa masharti ya usajili wa...www.jamiiforums.com
Fukuza Fukuza ya Uanachama: Kumbe Katiba ya CHADEMA ina makosa?
Wanabodi, Baada ya kuenea kwa uvumi wa timua timua nyingine Chadema, ambapo inasemekana kikao cha Bavicha, kimewavua uanachama wa Bavicha, wanachama wake watatu ambako kuvuliwa huko uanachama wa Bavicha, kutapelekea wanachama hao kupoteza sifa za uanachama wa Chadema automatically kwa mujibu...www.jamiiforums.com
P
Umemlisha maneno,Pasco hawaezi kuwa kilaza nmna huyo." Ili CHADEMA tuwaamini kuwa AGENDA yao ya Kudai Katiba Mpya ina Mashiko na wana Hoja ya Msingi hebu wao kama Chama waanze Kwanza kuonyesha kuwa wanaheshimu Katiba ndani ya Chama chao ambapo kuna uvunjifu mkubwa tu wa Katiba " Pascal Mayalla
Nukuu hii nimeitoa baada ya Kumsikia na Kumtizama jana Usiku Star Tv akiwa Mgeni rasmi kwa Dar es Salaam katika Kipindi kilichokuwa Kinasimamiwa na Mtozi Aloyce Nyanda.
Najua hapa JamiiForums kuna wana CHADEMA wengi tu na wale walio Neutral kama Mimi Krav Maga hivyo kwa pamoja ama tutaweza Kukubaliana nae au Kumpinga kwa Hoja.
Na wakati mnamjibu mwana CCM Pascal Mayalla kumbukeni kuwa huyu ni Msomi wa Fani nyingi nchini Tanzania za Habari na Sheria, Mjasiriamali mkubwa, Mjuaji wa Mambo mengi nchini Tanzania, Member Mkongwe JamiiForums, Mwanasiasa mwenye Mafanikio na Mtu mwenye Network kubwa sana ya Viongozi ( Watawala ) wa Tanzania hii na huenda hata katika Teuzi zijazo za DC au DED safari hii akawemo.
Hili ndio tatizo kubwa la chadema kujihisi kwamba mna akili,maono na ujuvi wa kila kitu hata kama hamnazoTatizo la Pascal na wengine wengini kutokuona mbali. Kwanza ya yote, katiba tunayoiongolea ni katiba ya nchi sio ya CHADEMA. Tumeona mapungufu ya hii katiba kipindi cha Magufuli na jinsi alivyoitumia kuminya haki za watu.
CHADEMA kutofuata katiba yao hakuwazuii Watanzania kupata katiba mpya; zaidi ya yote, CHADEMA ni chama kidogo na kichanga ukifananisha na taifa la Tanzania.