Ni mechanism gani iko ndani ya risasi (bullet) kiasi cha kuua kwa kasi?

Asante, jf kituo cha ujuzi
 
Nafikiri sheria zinakataza kutumia risasi zenye sumu.
 
Mmmh kumbe
 

Nimetumia lugha rahisi ,huwa zipo juu ya mfupa wa nyonga au chini ya mbavu kwa nyuma
 
Watu wengi hawaijui risasi, hiwa wanafikiri ni silver au lead kidogo naomba niwatoe tongo tongo:
Kuna aina nyingi ya risasi kwa ajili ya matumizi mbalimbali, lakini ambazo hutumika kuulia binadamu kwa ndani huwa ni kipande cha chuma ambacho kimefanyiwa coating ya copper, lead au nickel. Ganda ndilo huwa limebeba mripuko na kichwa ndio kinachosafiri na kwenda kwenye target.
Hapo kwenye hizo picha, ni risasi na inavyokaa kwenye silaha hicho kichwa huelekea mbele na nyuma ya ganda kuna ka sehemu ambako ndio kuna kiwashio ambacho huwasha baruti ya kwenye risasi, kutokana na aina na wingi wa baruti inayokuwemo kwenye ganda, ndio inayoipa kasi ya kutoka kwa spidi kali [supersonic].[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]

sent from my Samsung smart tv using JamiiForums
 
Mtuambie na jinsi ya kukwepa risasi,maana tunaona tu kwenye movie


Risasi haikwepwi kwa sarakasi wala mazingaombwe ya habari za vita ya maji maji 1905-1907 .

Risasi inakwepwa kwa njia mbili tu
1. Labda ulale kabla haijafyatuliwa. Mfano, Ukiona mtu anainua silaha ili akulenge basi lala faster hapo unaweza ukaikwepa risasi .

Japo , itategemeana na uwezo wako wa kulala kabla haijaachiliwa pia na uwezo wa mpigaji maana mpigaji akiwa na uwezo hata ukilala faster anaweza akapiga ya juu ikakudondokea ulipolala kisha ukalala daima .

2.kujikinga kwenye sehemu ambayo risasi haiwezi kupenya mfano, bullet proof vest au miamba/mawe magumu.

Bila hivyo, you're a dead body or badly injured.
 
Hapana , sababu kuu ni pressure effect to the body tissues resulted from conversion of kinetic energy.
Ndio maana mtu akipigwa risasi ya mkono ,ataendelea kua hai kwa muda mrefu kwa kadri upotevu wa damu utakavyokuwa umedhibitiwa Lakini ukipigwa risasi ya kifua au uti wa mgongo au kichwa , you won't make it for sufficient time to survive
Ndio maana katika treatment protocol ya bullet wounds hakuna kipengele cha poison decontamination
 
Wewe umeleza kwa lugha rahisi na umeeleweka vizuri sana.Very good.
Sasa kuna wengine wanakuja hadi na ma formula ya physics humu,ila hakuna kitu wanajua.
 
Risasi imejengwa ktk sehem kuu 5,

1-balut .
Balut ni chemical maalum iliotengenezwa kitaalam ,chemical hiyo inaweza kua unyevu au ukavu lakini inalipuka.

2-ganda la risasi.

3-prima.
Ni ile sehem ya kitako cha risasi,

4-cutredge case.
Ni ile sehem risasi ilipounganishwa kati ya kichwa na mwili,

5-properant .
Kichwa cha risasi chenyewe.

Kwenye bunduki kuna vitu muhimu vinavyoshugulika na risasi kulipuka.ambavyo ni ,
Firelling pin,msumari.
Spring leaf. inayokamata huo msumali kwenye mitambo ya triger ,
Unapovuta kockinghandel,msumari unakaa tayari,ukivuta trigger spring inasukuma msumari kwa kasi na kugonga kwenye kitako cha risasi na risasi hainabudi kulipuka na kichwa cha risasi na mwili vinaachana kwa kasi ,mwili wa risas unabaki na kichwa kinatoka nje kwa kasi kwa kufuata mtutu.SMG inatembea kwa sekunde mita 540 umbali wa kutua mita 2160.

TAHADHARI .
RISASI SIO LAZIMA IWEKWE KWENYE BUNDUKI PEKEE NDIO ILIPUKE.UKIOKOTA KITU NAMNA KIYO KISALIMISHE HARAKA KWENYE VYOMBO VYA USALAMA ,MAANA HATA UKIIWEKA KWENYE MOTO ITALIPUKA KWA HARAKA SANA,NA KWAVILE ITAKUA HAINA UELEKEO KAMA MTUTU BASI KUNA HATARI YA KUKUDHURU WEWE MWENYEWE AU HATA WA KALIBUYAKO.
 
Kuna zile bunduki za kuwindia unaweka kipisi cha nyondo Milimita 16 kama sikosei, akikufumua ya kifua uti wa mgongo una banduka, akikufumua ya kichwa ubongo unatoka na kuruka umbali wa kilomita 6....
DUUH!
 
Umenikumbusha mbali sana return spring mechanism (R. S. M)

SIJUI KESHO.
 
Mkuu risasi HAINA sumu ila kwa case ya huyo jamaa inawezekana akawa alipata INFECTION(MAAMBUKIZI) Kupiyia kwny majeraha ya hiyo risasi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali langu nililo uliza juu ya wale wanaoishi na risasi mwilini huwa inakuwaje? Nini kutokea mpaka hiyo risasi ishindwe kupenya mpaka nje Kama ilivyoelezewa na wadau hapo kuhusu kasi na nguvu ya mkito wake.

Kama ina sumu habari , Je inakuwaje mtu aishi na sumu habari ya risasi mwilini tena kwa miaka kadhaa.??
 
Mkuu kula like,kuna watu wanaelezea risasi inapokua imetoka kwa speed lkn hawajaelezea nn kinasababisha risasi iwe na speed ambayo inaweza kua haraka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukran mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…