Kati ya vitu ambavyo mpka leo vinanipa shida ni kushindwa kujua ni mechanism gani iko ndani ya risasi (bullet) kiasi cha kuua kwa kasi, kwa sababu kuna vitu mfano kisu ni kikubwa kinaweza kukita ndani ya mwili wa binadam still mtu akawa hai kwa muda fulani kuliko majeruhi wa risasi....tafadhali wenye Kujua
Sent from my HUAWEI TIT-U02 using JamiiForums mobile app
Iko hivi,
Kuna bunduki za aina tatu; kwanza shot gun, semiautomatic na automatic gun.
Hizo shotgun ni bunduki za kizamani kama gobore au wanazotumia kiwindia.
Semiautomatic ni kama vile Semiautomatic riffle (SAR) ambazo hutumika sana kwenye gwaride.
Automatic zinatumika zaidi vitani, kama SMG, AK47, G3, Uzi gun etc.
Zipo za masafa marefu kama LMG (zenye risasi za mikanda) etc
Sasa zinavyofanya kazi nadhani ndio swali lako. Kwenye automatic ndio Mpango mzima.
Risasi zinakaa kwenye magazine (kama 30-40). Hatua ya kwanza inavuta cocking handle ili kuweka risasi chamber, pili unafungua usalama, hapo unaweza kuweka rapid au moja moja.
Hatua ya tatu unafyatua.
Sasa unapofyatua ile trigger kuna vitendo vinne vinafanyika kwa sekunde moja.
Kwanza baruti iliyomo kwenye ganda la risasi italipuka na kusababisha risasi iende mbele.
Mlipuko ule husababisha cocking handle iliyoshikwa na spring irudi nyuma na kuchota risasi nyingine kutoka kwenye magazine na kuiweka chamber huku lile ganda la risasi iliyolipuka likiruka nje. Mapigo hayo huendelea mithili ya machine hadi uachie trigger.
Hiyo ndio maana ya automatic.
Uchawi wote uko kwenye baruti inapolipuka na ndio inayotoa sauti kali. Risasi ina uwezo wa kuua ndani ya meter 100.